Rais Samia amteua Zuhura Yunus kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu kupangiwa kazi nyingine

Rais Samia amteua Zuhura Yunus kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu kupangiwa kazi nyingine

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu amemteua aliyekuwa mtangazaji wa BBC, Zuhura Yunus kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu akimrithi Jaffar Haniu. Mwezi uliopita Zuhura aliaga BBC na hakusema anapoelekea.

Haniu aliyerithi kijiti kutoka kwa Gerson Msigwa Juni mwaka jana atapangiwa kazi nyingine akihudumu kwenye ofisi hiyo kwa miezi saba.

Wanawake oyeee, mpaka maji yaitwe mma.. Tunasubiri matokeo kutoka Dodoma japo tunayajua


======

Zuhura Yunus ni mwanamke wa kwanza kutangaza kipindi cha Kiswahili cha televisheni BBC, Dira ya Dunia akihudumu kwenye shirika hilo kwa miaka 14. Zuhura alijiunga na BBC Swahili mwaka 2008 akiwa mtangazaji na mtayarishaji wa matangazo. Alijulikana kwa wasikilizaji wa BBC Swahili kuwa mtangazaji kinara wa matangazao ya redio, Dira ya Dunia, Zuhura ameripoti na kutangaza uchaguzi wa Tanzania mwaka 2010.

Kabla ya kujiunga na BBC, Zuhura alifanya kazi ya utangazaji katika vipindi mbalimbali vya redio ya Times FM na Uhuru FM nchini Tanzania. Mwaka 2002 Zuhura alishinda tuzo ya Habari ya Ishi nchini Tanzania kutokana na ripoti ya HIV/Aids. Pia amefanya kazi ya uandishi wa habari katika gazeti la The Citizen newspaper.

Mwaka jana Zuhura aliandika kitabu chake cha wasifu wa Biubwa Amour Zahor, mwanaharakati mwanamke wa kisiasa wakati wa mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964.

Zuhura katika utumishi wake amewahoji viongozi wa Afrika kama vile Rais wa zamani wa Tanzania, Jakaya Kikwete kama sehemu ya taarifa kuhusu biashara haramu ya wanyama pori pamoja na Rais wa Uganda Yoweri Museveni. Mahojiano aliyoyafanya na mgombea urais wa upinzani, Edward Lowassa mwaka 2015 yalizua gumzo katika vyombo vya habari nchini.

Zuhura ni muhitimu wa shahada ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Mbale IUIU, Uganda na ana shahada ya Uzamili ya Mawasiliano ya Vyombo vya Habari kutoka Chuo Kikuu cha Leicester, Uingereza.

Zuhura Yunus kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, amepasiwa mpira na Charles Hillary ambaye alifanyia mpango kwenda BBC.​

Sasa Charles Hillary ni Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu,zanzibar.​

Kwahiyo hii dana dana inachezwa bila watanzania kuunganisha matukio.​

Hillary kapelekwa zenji akitokea bara na Yunus kaletwa bara akitokea zenji. Hii imechezwa kupumbaza wabongo.​

 
Mwaka wa Waislamu huu, Ndugu yangu Jaffar Haniu kakosea wapi? Sitaki kuamini kakubali kirahisi hivyo kuacha yale mapochopocho mix kuku sambusa wa ikulu.

Mwezake Msigwa tangu afutwe kazi ikulu siku hizi kapauka kweli, Ikulu ikulu tu.
Charles Hillary nae ni muislam ,
Na Jaffar Haniu nae mkiristo kumbe?
 
Mwaka wa Waislamu huu, Ndugu yangu Jaffar Haniu kakosea wapi? Sitaki kuamini kakubali kirahisi hivyo kuacha yale mapochopocho mix kuku sambusa wa ikulu.

Mwezake Msigwa tangu afutwe kazi ikulu siku hizi kapauka kweli, Ikulu ikulu tu.
Msigwa si msemaji tena wa serikali? Mzee unaonekana ni mpika majungu mno! Hupendi kupata kwa nwenzako.
 
Hajui kiingereza fasaha

Huwezi kuwa mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais halafu lugha haipandi, Hatoshi tu

Ataenda kuwa RAS simiyu kunamtosha
Hiyo lugha watz wengi hawaijui na hawataki kujifunza
 
Mama yupo vizuri anaangalia mbali, kujaza midume ikulu mingine haina adabu, Bravo kuliona hilo.
 
Kuuliza sio ujinga hivi bongo uraia pacha usharuhusiwa? Dada yetu ni raia wa uingereza alizaliwa kule au imekaaje hii
 
Kuuliza sio ujinga hivi bongo uraia pacha usharuhusiwa? Dada yetu ni raia wa uingereza alizaliwa kule au imekaaje hii
[emoji851][emoji851],yaani watu wanasaka weakness kona zote yaani,,,,
 
Vitabu vitakatifu hajiwahi kumpa mwanamke kipaumbele katika kuongoza.Mungu hakumuumba awe kichwa...Huo ndio ukweli na nikwasababu za kiroho zaidi..ndio maana hata nchi za kiislam Ni marufuku...

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app

Tanzania Sio nchi ya kiislam. Unfortunately hivo vitabu vyako vimeandikwa na watu kama wewe waliokuwa na maslahi yao .

Huwezi kuniambia mwanamke hawezi kuongoza , mwanamke ndiyo aliyemzaa mwanaume , Na kumfundisha na kumpa elimu na kumtengeneza na kuwa mwanaume, na kumfundisha na kuwa na maadili

Leo unasemaje mwanamke hawezi kuongoza , are you mad !

hawezi kuongoza eti sababu za kiroho, hiyo roho umeshawahi kuiona? .... hizi mambo ni za kizamani na zipigwe vita .

Kila mtu anaweza kuongoza akipata nafasi. Nchi za kiarabu my foot. Kuna nchi mabedui na ignorant kama za kiarabu ?

mwanamke Tu kusoma ni tabu , kuendesha gari ni Ishu .... nyie ndio mnaamini hao watu ....Shame

Mama Teua hata Mkuu wa mwanajeshi mwanamke... Sisi tutatwii wewe ndio mmiliki .. na Tanzania yote na vilivyomo ni mali yako

Sema utakalo tunatekeleza
 
Hongera sasa atumie uleule weledi alokua nao BBC akilegea aka akavaa shati la kijani atapoteza heshima yake .
Mkuu believe me,lile shati ni laana na ikiwa ameingia humo ana % chache sana ku-perfome akaonekana bora zaidi (japo alomweka pale kwa kukubali kwake kwenda anavyotaka yeye atamuona bora)
 
Back
Top Bottom