Azim Sokoine
JF-Expert Member
- Aug 20, 2014
- 1,443
- 2,643
ChristianHalafu mtu anakuja kutudanganya hapa eti ni mmachame!
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu amemteua aliyekuwa mtangazaji wa BBC, Zuhura Yunus kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu akimrithi Jaffar Haniu. Mwezi uliopita Zuhura aliaga BBC na hakusema anapoelekea.
Haniu aliyerithi kijiti kutoka kwa Gerson Msigwa Juni mwaka jana atapangiwa kazi nyingine akihudumu kwenye ofisi hiyo kwa miezi saba.
Wanawake oyeee, mpaka maji yaitwe mma.. Tunasubiri matokeo kutoka Dodoma japo tunayajua
======
Zuhura Yunus ni mwanamke wa kwanza kutangaza kipindi cha Kiswahili cha televisheni BBC, Dira ya Dunia akihudumu kwenye shirika hilo kwa miaka 14. Zuhura alijiunga na BBC Swahili mwaka 2008 akiwa mtangazaji na mtayarishaji wa matangazo. Alijulikana kwa wasikilizaji wa BBC Swahili kuwa mtangazaji kinara wa matangazao ya redio, Dira ya Dunia, Zuhura ameripoti na kutangaza uchaguzi wa Tanzania mwaka 2010.
Kabla ya kujiunga na BBC, Zuhura alifanya kazi ya utangazaji katika vipindi mbalimbali vya redio ya Times FM na Uhuru FM nchini Tanzania. Mwaka 2002 Zuhura alishinda tuzo ya Habari ya Ishi nchini Tanzania kutokana na ripoti ya HIV/Aids. Pia amefanya kazi ya uandishi wa habari katika gazeti la The Citizen newspaper.
Mwaka jana Zuhura aliandika kitabu chake cha wasifu wa Biubwa Amour Zahor, mwanaharakati mwanamke wa kisiasa wakati wa mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964.
Zuhura katika utumishi wake amewahoji viongozi wa Afrika kama vile Rais wa zamani wa Tanzania, Jakaya Kikwete kama sehemu ya taarifa kuhusu biashara haramu ya wanyama pori pamoja na Rais wa Uganda Yoweri Museveni. Mahojiano aliyoyafanya na mgombea urais wa upinzani, Edward Lowassa mwaka 2015 yalizua gumzo katika vyombo vya habari nchini.
Zuhura ni muhitimu wa shahada ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Mbale IUIU, Uganda na ana shahada ya Uzamili ya Mawasiliano ya Vyombo vya Habari kutoka Chuo Kikuu cha Leicester, Uingereza.
Soon nae atapewa post,ni swala la muda tu avumilie!!Pascal Mayalla anaendelea kupiga picha daraja la Tanzanite na kupost
Charles Hillary nae ni muislam ,Mwaka wa Waislamu huu, Ndugu yangu Jaffar Haniu kakosea wapi? Sitaki kuamini kakubali kirahisi hivyo kuacha yale mapochopocho mix kuku sambusa wa ikulu.
Mwezake Msigwa tangu afutwe kazi ikulu siku hizi kapauka kweli, Ikulu ikulu tu.
Msigwa si msemaji tena wa serikali? Mzee unaonekana ni mpika majungu mno! Hupendi kupata kwa nwenzako.Mwaka wa Waislamu huu, Ndugu yangu Jaffar Haniu kakosea wapi? Sitaki kuamini kakubali kirahisi hivyo kuacha yale mapochopocho mix kuku sambusa wa ikulu.
Mwezake Msigwa tangu afutwe kazi ikulu siku hizi kapauka kweli, Ikulu ikulu tu.
Hiyo lugha watz wengi hawaijui na hawataki kujifunzaHajui kiingereza fasaha
Huwezi kuwa mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais halafu lugha haipandi, Hatoshi tu
Ataenda kuwa RAS simiyu kunamtosha
[emoji851][emoji851],yaani watu wanasaka weakness kona zote yaani,,,,Kuuliza sio ujinga hivi bongo uraia pacha usharuhusiwa? Dada yetu ni raia wa uingereza alizaliwa kule au imekaaje hii
Vitabu vitakatifu hajiwahi kumpa mwanamke kipaumbele katika kuongoza.Mungu hakumuumba awe kichwa...Huo ndio ukweli na nikwasababu za kiroho zaidi..ndio maana hata nchi za kiislam Ni marufuku...
Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Mkuu believe me,lile shati ni laana na ikiwa ameingia humo ana % chache sana ku-perfome akaonekana bora zaidi (japo alomweka pale kwa kukubali kwake kwenda anavyotaka yeye atamuona bora)Hongera sasa atumie uleule weledi alokua nao BBC akilegea aka akavaa shati la kijani atapoteza heshima yake .
[emoji851][emoji851],yaani watu wanasaka weakness kona zote yaani,,,,
Kwa hiyo wakiwa wasukuma kunawafanya wasiwe wakristo, unafikiri hakuna waislam ambao ni wasukuma...udini hautufikishi kokote