Rais Samia amteua Zuhura Yunus kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu kupangiwa kazi nyingine

Mwaka wa Waislamu huu, Ndugu yangu Jaffar Haniu kakosea wapi? Sitaki kuamini kakubali kirahisi hivyo kuacha yale mapochopocho mix kuku sambusa wa ikulu.

Mwezake Msigwa tangu afutwe kazi ikulu siku hizi kapauka kweli, Ikulu ikulu tu.
Haniu alishindwa kuichangamsha kurugenzi yake, anatakiwa kuwa pro active, kumbrand Rais na mambo anayofanya kwa Taifa,yeye alikuwa anasubiri hafla tu
 
Mwaka wa Waislamu huu, Ndugu yangu Jaffar Haniu kakosea wapi? Sitaki kuamini kakubali kirahisi hivyo kuacha yale mapochopocho mix kuku sambusa wa ikulu.

Mwezake Msigwa tangu afutwe kazi ikulu siku hizi kapauka kweli, Ikulu ikulu tu.
Hajakosea bro anapelekwa kwingine

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Alichalenji vipi na kuwa mpinzani wa serikali embu fafanua,BBC ni kutoa habari siyo mapambio.
 
Mawasiliano nayo muhimu, sio msingi mpaka unastaafu wewe upo danganyika tu, exposure nayo muhimu. Waandishi na wasomi wetu wengi communication skills ni changamoto, hata lugha fasaha ya kiswahili tu ni shida, kiingereza kinagonga ugokoni, swanglish ndio imejaa na mivyeti ya kukariri darasani.

Msome alama za nyakati, hizi ni zama nyengine na teuzi nyeti zinakwenda kimkakati.
Yaani msomi wa kitanzania, nchi ya waswahili, bado kwenye l anaweka r, kwenye m anaweka n, kwenye anakali sauti anapuyanga tu, Tafsida zero, tashtiti no where to be seen, hajui kishazi wala nahau ???

Hivi mumepata kuwasikia akina David Wakati, uncle J nyaisanga, Charles hillary, tido muhando , Chama Matata, Kipozi na huyu Zuhura Yunusu wanavyotohoa kiswahili na kiingereza?
Nendeni mkatafute clips zao na audio mkajifunze.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…