Rais Samia amteua Zuhura Yunus kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu kupangiwa kazi nyingine

Rais Samia amteua Zuhura Yunus kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu kupangiwa kazi nyingine

si kweli lugha anaijua sana kasoma HGL Ilboru secondary kule Ilboru hawapelekwi vilaza acha uongo.walikuwa na Ayubu Lyoba enzi hizooo.kipindi hicho walikuwa wanasoma watu cream hivyo usipotoshe watu humu umlaumu kwa jingine na si lugha ya kiingereza.

kiingereza kuongea kinaingiliana vipi na HGL...we hioni tuna maprofesa na Madr hawajui kiEnglish... kiEnglish kama lugha nyingine hakiangalia ukichwa wako bali kinaangalia juhudi zako kwenye kuijua lugha mfano makuzi na shile ulozosoma utotoni au juhudi zako za ukubwani...
 
Nchi yetu imeharibika sana. Hakuiharibu Samia. Samia anaendeleza tu sera za CCM. Aliyeanzisha ni yule alikuwa anateua Wasukuma wenzie na kupeleka miradi ya kimkakati ya kitaifa kijijini kwake.
Mtakufa midomo wazi kwa ajili ya chuki na kushindwa kuvumilia.Kumbe WAKIRISITO ni wepesi kiasi hiki.
emoji13.png
emoji13.png
emoji13.png
emoji13.png

Wakumbushe walipokuwa wakiteuliwa wao sisi tuliamua kufanya biashara ,mziki,mpira na vitu vingine na walisema kwa sababu hatujasoma sasa mbona upande wa pili vilio vimeanza asubuhi mapema?
 
Na hii umeikosa Bwana Pascal

Wonders shall never end


Siamini Kinachotokea hapa uwanjani, Pascal Mayalla anawekwa benchi tena
Pascal Mayala kama hakuteuliwa awamu iliyopita zama hizi ndio haiwezekani hata jina lake kupendekezwa kupelekwa mezani kwa Saa 100

Dini na asili yake Pascal ni kikwazo

Zama hizi ili upate teuzi kilaini inabidi uwe na sifa mojawapo kati ya hizi: (i) Mwislamu, (ii) Mzanzibari, & (iii) Unatokea ukanda wa Pwani
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu amemteua aliyekuwa mtangazaji wa BBC, Zuhura Yunus kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu akimrithi Jaffar Haniu. Mwezi uliopita Zuhura aliaga BBC na hakusema anapoelekea.

Haniu aliyerithi kijiti kutoka kwa Gerson Msigwa Juni mwaka jana atapangiwa kazi nyingine akihudumu kwenye ofisi hiyo kwa miezi saba.

Wanawake oyeee, mpaka maji yaitwe mma.. Tunasubiri matokeo kutoka Dodoma japo tunayajua


======

Zuhura Yunus ni mwanamke wa kwanza kutangaza kipindi cha Kiswahili cha televisheni BBC, Dira ya Dunia akihudumu kwenye shirika hilo kwa miaka 14. Zuhura alijiunga na BBC Swahili mwaka 2008 akiwa mtangazaji na mtayarishaji wa matangazo. Alijulikana kwa wasikilizaji wa BBC Swahili kuwa mtangazaji kinara wa matangazao ya redio, Dira ya Dunia, Zuhura ameripoti na kutangaza uchaguzi wa Tanzania mwaka 2010.

Kabla ya kujiunga na BBC, Zuhura alifanya kazi ya utangazaji katika vipindi mbalimbali vya redio ya Times FM na Uhuru FM nchini Tanzania. Mwaka 2002 Zuhura alishinda tuzo ya Habari ya Ishi nchini Tanzania kutokana na ripoti ya HIV/Aids. Pia amefanya kazi ya uandishi wa habari katika gazeti la The Citizen newspaper.

Mwaka jana Zuhura aliandika kitabu chake cha wasifu wa Biubwa Amour Zahor, mwanaharakati mwanamke wa kisiasa wakati wa mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964.

Zuhura katika utumishi wake amewahoji viongozi wa Afrika kama vile Rais wa zamani wa Tanzania, Jakaya Kikwete kama sehemu ya taarifa kuhusu biashara haramu ya wanyama pori pamoja na Rais wa Uganda Yoweri Museveni. Mahojiano aliyoyafanya na mgombea urais wa upinzani, Edward Lowassa mwaka 2015 yalizua gumzo katika vyombo vya habari nchini.

Zuhura ni muhitimu wa shahada ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Mbale IUIU, Uganda na ana shahada ya Uzamili ya Mawasiliano ya Vyombo vya Habari kutoka Chuo Kikuu cha Leicester, Uingereza.

Naona BBC products wanazidi kuupiga mwingi kwenye ofisi za wazenj.

Charlea Hilary yupo ikulu na sasa Zuhura yupo ikulu akitafuna koroshow.
 
Wakumbushe walipokuwa wakiteuliwa wao sisi tuliamua kufanya biashara ,mziki,mpira na vitu vingine na walisema kwa sababu hatujasoma sasa mbona upande wa pili vilio vimeanza asubuhi mapema?

Watu wanalalamikia vitu ambavyo hawawezi kubadili wala kuvipata

Wakati walipokua wanalalamika oooh wachaga hawapewi nafasi wametengwa, wachaga wenyewe walikua busy kuongeza nafasi ya kutanua wigo wao kwenye kazi zao binafsi
 
Nimehoji tu kama katenguliwa muislamu why asipewe mkristo hiyo nafasi? Anarudishwa muislamu haya mambo huwa kuna ku alternate akifeli muislamu anawekwa mkiristo.
Unafeli wapi mkuu wangu Nyboma..this is not you...utendaji wa mtu haupimwi kwa dini yake, mkuu! kama Haniu ameharibu sio kwa sababu ya dini yake, na kama akingepewa "mkristo" na kufanya vizuri sio kwa sabau ya dini yake!
 
Mwaka wa Waislamu huu, Ndugu yangu Jaffar Haniu kakosea wapi? Sitaki kuamini kakubali kirahisi hivyo kuacha yale mapochopocho mix kuku sambusa wa ikulu.

Mwezake Msigwa tangu afutwe kazi ikulu siku hizi kapauka kweli, Ikulu ikulu tu.
Jafari ni jina la kikristu au kiislam?
 
Ile haikuwa awamu ya Wakristo. Ilikuwa awamu ya Wasukuma ambao hawakuwa Waislamu ila walikuwa Wakristo. Acha watu waseme ukweli wao wa moyoni. Na zote ni serikali za CCM. Na hata wakati wa Magufuli tulipigia kelele kuhusu teuzi za akina Maduhu, Masanja, Maganga... Usijifanye haukuwepo.
Kwa hiyo wakiwa wasukuma kunawafanya wasiwe wakristo, unafikiri hakuna waislam ambao ni wasukuma...udini hautufikishi kokote
 
Back
Top Bottom