Je, Kadi ni Muhimu kuliko ripoti ya CAG?
Tangu Rais Samia ameingia Madarakani,kumekuwa na taarifa nyingi sana kuhusu ufisadi mkubwa sana unaoendelea kufanywa katika taasisi na miradi mingi ya kitaifa.Ikiwa pia ni katika halmashauri za majiji,Mikoa na Wilaya.
Hii ni kutokana na ripoti ya Mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali CAG. Kwa miaka miwili mfululizo kama sikosei.
Sasa basi,la kushangaza ni kwamba tangu ripoti hizo za mabilioni kwa matrilioni ya upotevu wa pesa za serikali kutolewa na CAG.
Hatujawahi kumuona au kumsikia Mh Rais Samia akichukua hatua za kuwawajibisha wahusika na hatimae kuweza kuwafikisha kwenye vyombo vya kisheria ili hatua stahiki za kinidhamu na kijinai ziweze kuchukuliwa
Kama sikosei mara ya mwisho tulimkariri Mh Rais akiishia kusema hao ni Wezi wa mali za umma ni "Stupid"
Badae hayo yalipita na maisha yameendelea,bila kusikia kauli ya Rais kuhusiana na ubadhirifu huo.
Mpaka sasa ilipoibuka ya huko Mtwara. Ambapo limetokea tukio hili.
Kwamba.
Wananchi wamerudisha kadi za CCM kisa ni kutoridhishwa na watendaji wa serikali katika mojawapo ya wilaya mkoani humo.
Sasa ndio tumemuona mama ametoka rasmi na kuanza kuwatumbua viongozi wa kiserikali. Kama DC,DED na wengine watakaofuatia.
Sitaki kuingia kutafuta mchawi kwa huko Mtwara.
Ila najiuliza tu kwamba!
Je!
Kwa yeye Mheshimiwa Rais JMT.
Hata ma-trilioni yanayoibiwa kila uchao na huku akipewa taarifa kuanzia ukarabati wa MV Magogoni huko Mombasa Kenya, kwa thamani inayozidi bei ya kununulia kivuko chenyewe.
Na mpaka sasa yuko kimya!
Ripoti za CAG.mpaka sasa yuko kimya!
Madawa ya kulevya yaliyokamatwa Mtwara na mpaka sasa kimya!
Na sasa kashfa ya mkataba wa DP-WORLD ametamka tena kwenye
Hadhara ya waumini kanisani kwamba "amekaa kimya na ataendelea kukaa kimya"
Mambo yaliyonyamaziwa ni mengi sana mpaka sasa!
Lakini kurudishwa kadi ameshindwa kukaa kimya sababu wamegusa maslahi yake.
Sababu kurudishwa kadi ni kifo kwa CCM ambayo ndiyo mzizi na nguzo kuu kwa U- Rais wake!
Kwamba hayo mengine hayamhusu sababu wanatekeleza maelekezo ya kula urefu wa kamba yake au?
Tumueleweje Mheshimiwa Rais wetu wa JMT?
Eeh Mola Inusuru Tanzania [emoji1241] [emoji813]
View attachment 2732155