Rais Samia amtimua Hanafi Hassan Msabaha, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara kisa wananchi kurudisha Kadi za CCM

Rais Samia amtimua Hanafi Hassan Msabaha, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara kisa wananchi kurudisha Kadi za CCM

Raisi wa jamhuri ya muungano wa tanzania Dk Samia suluhu hassan akiwa mkoani pwani amesisitiza viongozi kuwa wabunifu na kutosubiria maelekezo kutoka juu hata hivyo amemtumbua mkuu wa wa wilaya ya mtwara baada ya wananchi kurudisha kadi za chama kwa kisingizio kuwa kuna upinzani mkali wilayani humo ,chanzo cha kutumbuliwa ndoo hicho kwa hiyo hana imani naye tena[emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji41][emoji41][emoji41][emoji41]View attachment 2730337
Heh..!!

Wamechanganyikiwa walah!
 
Hii nimeiona ITV habari. Mama kakasirika mkuu wa wilaya kufanya uzembe kwa wananchi kurudisha kadi za chama kisa Mtwara wengi ni upinzani.

My Take: Tuendelee kupambana!

=========

Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kumuondoa kazini Hanafi Hassan Msabaha wakati akifunga mafunzo ya uongozi kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala katika Shule ya Uongozi Kibaha

Akieleza sababu zilizopelekea uamuzi huo Rais Samia amesema Mkuu huyo wa Wilaya amekuwa akipokea hongo na kuhamisha Miradi inapotakiwa kwenda na kuipelekea sehemu isiyohitajika, kitendo kilichofanya Wananchi kukerwa na kurudisha Kadi za Chama

Amesema hawezi kustahimili kuona Kadi za Chama zinarudishwa wakati Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wapo na walipoulizwa, Wakuu hao walijibu kuwa eneo hilo lina Wapinzani wengi

Zikiwa zimepita siku nne tangu baadhi ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa Kijiji cha Lyowa Wilaya ya Mtwara warudishe kadi zao za chama kushinikiza Serikali kumaliza shule ya sekondari kijijini kwao, hatimaye Rais Samia Suluhu Hassan amesema atawafuta kazi Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa eneo hilo kwa kushindwa kusikiliza kero za wananchi.

Rais Samia ametangaza dhamira hiyo mkoani Pwani leo, Jumapili Agosti 27, 2023 alipohutubia hafla ya kufunga mafunzo ya uongozi kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa, yaliyofanyika katika Taasisi ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere, Kibaha mkoani humo. “Mkuu wa Wilaya anahongwa, mradi anaacha kwenda unakotakiwa anapeleka usipotakiwa, kiasi kwamba wananchi wanafika kurudisha kadi za chama, sisi huku tuna haja kubwa mmetuacha fedha mmepeleka kule na kadi zenu hizo. ALSO READ Rais Samia kuwafuta kazi DC, DED Mtwara

Kitaifa 30 min ago Rais Samia kuwafuta kazi DC, DED Mtwara

Kitaifa 30 min ago “Sina imani na Mkuu wa Wilaya anayesababisha kadi zirudishwe, Mtwara, Mkuu wa Wilaya yako sijui Hanafi (Msabaha) namtimua leo siwezi kustahimili kadi za chama zinarudishwa, nini Mkuu wa Wilaya yupo DED yupo yeye na DED wake,” amesema. Chanzo Wakati Rais Samia akiyasema hayo leo, Mwananchi Digital ilifika katika Kijiji cha Lyowo Jumatano Agosti 23, 2023 na kufanya mahojiano na wananchi hao kujua sababu za kurudisha kadi hizo.

Ally Mtambulwa mkazi wa kijiji hicho amesema wamerudisha kadi hizo kutokana na kutoridhishwa na maamuzi ya Serikali juu ya umaliziaji wa shule kijijini kwao huku akidai fedha zilizoletwa na Serikali kwaajili ya ujenzi wa shule ya kata zikipelekwa katika kijiji jirani kwa ajili ya ujenzi wa shule nyingine. “Hizi kadi tunazirudisha kwa Mkuu wa Mkoa, hatuko tayari kuona fedha zinakuja za shule lakini zinapelekwa kijiji kingine wakati sisi tumejenga kwa nguvu hatujapewa hata shilingi kumi kwanini tusisaidiwe?,”alihoji.

“Tumeshindwa na siasa kadi tunazo mfukoni tunazirudisha leo tena kwa Mkuu wa Mkoa, tumefunga ofisi ya mtendaji kwakuwa tuliishirikisha Serikali kwa kila hatua kwa nini ilituacha tumejenga sekondari madarasa matano, choo na ofisi ya walimu na walipopata fedha za ujenzi wakazipeleka kwingine ambako kuna madarasa mawili tu kwanini hawaji tukamalizia ujenzi wa shule hii?,” aliuliza Mtambulwa. Naye Asha Issa mkazi wa kijiji cha Lyowa amesema kuwa awali walianza ujenzi kwa kujitolea na walifikia hatua nzuri ambapo imebakia sehemu ndogo iweze kukamilika hivyo kuhitaji msaada wa serikali. “Sisi hatuna maneno mengi watoto wetu hawataenda shule wala kazi hazitafanyika tunahitaji mpaka tujue sekondari yetu inakalimikaje na kwanini sekondari ya kata isijengwe hapa?,”alihoji Asha.

Majibu ya Serikali Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Hassan Mmunda ambaye alisema ana siku tatu tangu wananchi wakatae kuongozwa nae huku akiiomba viongozi wa juu wafike kwa ajili ya usuluhishi wa jambo hilo. “Mimi nimetenguliwa siku tatu sasa (saba sasa) nawaomba viongozi wa Serikali waje tukae tuongee naona maendeleeo yamefanyika shule imejengwa lakini sasa shughuli za kiserikali zimesimama hii inaumiza hata watoto wetu wapo nyumbani hawaendi shule na ofisi zimefungwa,”alisema Mmunda

Mwananchi Jumatano Agosti 23, 2023 ilipomtafuta Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Hanafi Msabaha alisema Sh500 milioni walizopokea zitaenda kujenga shule mpya katika Kata ya Muungano na baada ya hapo wataimalizia ya Kijiji cha Lyowa. “Suala la shule kila sehemu walitaka shule ijengwe kwenye kijiji chao hivyo nikatumia busara ya kawaida baada ya kutembelea shule ya sekondari Lyowa ina eneo zuri kubwa limenyooka lakini tayari walikuwa na makubaliano waliyokaa katika vikao na kupitisha ujenzi wa shule ya kata katika kijiji cha Muungano,” alisema Msabaha.

View attachment 2730252
anawaza uchaguzi baddla ya kufanya kazi, kwa hiyo mkuu wa wilaya afanye kazi za ukada dah ajuza kaishiwa point
 
Raisi wa jamhuri ya muungano wa tanzania Dk Samia suluhu hassan akiwa mkoani pwani amesisitiza viongozi kuwa wabunifu na kutosubiria maelekezo kutoka juu hata hivyo amemtumbua mkuu wa wa wilaya ya mtwara baada ya wananchi kurudisha kadi za chama kwa kisingizio kuwa kuna upinzani mkali wilayani humo ,chanzo cha kutumbuliwa ndoo hicho kwa hiyo hana imani naye tena[emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji41][emoji41][emoji41][emoji41]View attachment 2730337
Ameongea kama Rais au Mwenyekiti?
 
Screenshot_20230827-181512.png

Kuna namna wateuliwa hawapendi kazi za kisiasa au wanalazinishwa kufanya kazi wasizozipenda.
 
matokeo ya waraka wa TEC yameanza kujitokeza, na bado watu hawarudishi kadi eti kisa DC, sababu kubwa ni wewe mkuu, hujaona tu. Unamwonea DC wa watu bure, mwecha ale urefu wa kamba yake kama unavyoinyelea bandari
DC ni matunda ya hayati JPM ya kunyanyapaa wapinzani, alidhani anamfurahisha mkuu wake wa kazi kumbe ameharibu.
 
Raisi wa jamhuri ya muungano wa tanzania Dk Samia suluhu hassan akiwa mkoani pwani amesisitiza viongozi kuwa wabunifu na kutosubiria maelekezo kutoka juu hata hivyo amemtumbua mkuu wa wa wilaya ya mtwara baada ya wananchi kurudisha kadi za chama kwa kisingizio kuwa kuna upinzani mkali wilayani humo ,chanzo cha kutumbuliwa ndoo hicho kwa hiyo hana imani naye tena[emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji41][emoji41][emoji41][emoji41]View attachment 2730337
Hii Kali! Unadhani kadi zinarudi kwasababu ya DC ? Wananchi Hawana Imani na Rais. Rais ukivuruga Hawa akina DC hawana cha kufanya. Hii ni rasharasha, masika ni mwakani na 2025 zitarudi nyingi mno
 
Samia ndie tatizo kuu nchi hii kwa sasa, hilo ndilo ninalofahamu.
 
Kwani haiwezekani kuwa hiyo ya hongo kuwa imewekwa ili kujustify kuondolewa kwake!!?
Mkuu yupi wa Wilaya hapokei hongo na rushwa!!??
DED yupi hapokei hongo na rushwa!!?
Kwa nini iwe wawili tu na si 10 au 100!!??
Sababu ya DC kufukuzwa ndio hizo hapo kwenye 'bold'....hayo ya kadi kurudishwa ni nyongeza tu.
 
Tusikae kimya sasa kusubiri miaka 10 ijayo Rais wetu aandike Kitabu cha kujutia kuingia mkataba huu mbovu wa Bandari, tumkosoe mapema ili akija kuandika kitabu hicho aseme nilishauriwa ila nilikataa Ushauri"-Baba Paroko wetu leo 27/08/2023
 
Ma DC wegi ni kitengo
Kitengo wa kuji expose, Kitengo bila nidhamu ni sawa na wa Buza tu.
Sasa kajitu kapo kwenye balehe kanaenda kumletea habari za ukitengo Kanali ambaye kwanza amekua commissioned na rais, pili ni mteule wa rais juu yake?
 
Back
Top Bottom