Rais Samia amvaa Ndugai. Asema, "Huwezi kuamini mtu mzima ana-argue tozo na mkopo wa Trilioni 1.3"

Rais Samia amvaa Ndugai. Asema, "Huwezi kuamini mtu mzima ana-argue tozo na mkopo wa Trilioni 1.3"

Rais Samia Suluhu Hassan amesema ni Uhuru wa Mtu kusema chochote, lakini inashangaza Mtu anayetegemewa kushirikiana na Serikali kwenye safari ya maendeleo 'kuargue' kuhusu Tozo na Mkopo wa Trilioni 1.3 kwasababu taarifa zote za Uchumi zinapita kwake akisema, "Ni homa (fever) ya 2025, wasameheni"

Ameongeza, "Huwezi kuamini mtu mzima na unaenda kuargue tozo na mkopo wa Trilioni 1.3 kama kwamba ndio kwamba inatokea Tanzania wakati toka tunapata Uhuru ni Mikopo kwenda mbele. Na katika Mikopo yote huu ni mkopo mzuri zaidi"

Sasa labda na hio return on investment its about time to rethink our strategy...., Huyu Mama Kuendelea kushikia Bango hii issue inamfanya kuonekana petty..... Ingawa sio mbaya kujibu hoja (ila hoja hujibiwa kwa hoja na sio vioja)
 
Kwa hotuba ya leo ya Samia kama Ndugai asipojiuzulu basi hana akili timamu na anatumikia tumbo lake tu. Samia amesema wazi kuwa kilichomsukuma Ndugai kupinga mikopo ni Uchaguzi Mkuu wa 2025. Aidha amesema wale wote wanasioweza kwenda pamoja na yeye katika kuwaletea wananchi maendeleo atawaondoa katika serikali ya ili wapate muda wa kutosha kujiandaa na uchaguzi wa 2025!

Ndugai sio serikali kaka
 
Rais Samia Suluhu Hassan amesema ni Uhuru wa Mtu kusema chochote, lakini inashangaza Mtu anayetegemewa kushirikiana na Serikali kwenye safari ya maendeleo 'kuargue' kuhusu Tozo na Mkopo wa Trilioni 1.3 kwasababu taarifa zote za Uchumi zinapita kwake akisema, "Ni homa (fever) ya 2025, wasameheni"

Ameongeza, "Huwezi kuamini mtu mzima na unaenda kuargue tozo na mkopo wa Trilioni 1.3 kama kwamba ndio kwamba inatokea Tanzania wakati toka tunapata Uhuru ni Mikopo kwenda mbele. Na katika Mikopo yote huu ni mkopo mzuri zaidi"
Ndugai atakunywa sumu, hali yake ni mbaya sana
 
Ndugai kama Spika, ka mtu binafsi, ka mbunge na kama kiongpzi ndani ya CCM, uovu wake, kama walivyo wenzake, ni mwingi, na umewaathiri sana Watanzania negatively.

Hata hivyo, hakuna mwanadamu mwenye kiapo na uovu. Kama Ndugai ameamua kujutia uovu wake na kutaka kuweka alama itakayokumbukwa katika nchi hii, asaidie kupatikana kwa misingi na mifumo bora ya kiutawala. Na hilo, hakikisho lake lipo kwenye katiba.

Kwa kuanzia, Bunge likatae unafiki wa Serikali, unaowekwa kwenye mswada wa mabadiliko ya katiba. Mswada huo ni upuuzi na kiinimacho. Bunge liukatae, na kuitaka Serikali kupeleka mswada wenye dhamira njema.

Uundwaji wa Tume Huru ya Uchaguzi kwa kuwatumia wateule wa Rais kupendekeza majina ya wajumbe wa Tume ya Uchaguzi kwa Rais, ni ujinga, upuuzi na kukosa hekima na uadilifu kwa waliouandaa huo mswada. Bunge liukatae, kwa sababu ni mswada wa kijinga kabisa.
 
Back
Top Bottom