Rais Samia amvaa Ndugai. Asema, "Huwezi kuamini mtu mzima ana-argue tozo na mkopo wa Trilioni 1.3"

Rais Samia amvaa Ndugai. Asema, "Huwezi kuamini mtu mzima ana-argue tozo na mkopo wa Trilioni 1.3"

Rais Samia Suluhu Hassan amesema ni Uhuru wa Mtu kusema chochote, lakini inashangaza Mtu anayetegemewa kushirikiana na Serikali kwenye safari ya maendeleo 'kuargue' kuhusu Tozo na Mkopo wa Trilioni 1.3 kwasababu taarifa zote za Uchumi zinapita kwake akisema, "Ni homa (fever) ya 2025, wasameheni"

Ameongeza, "Huwezi kuamini mtu mzima na unaenda kuargue tozo na mkopo wa Trilioni 1.3 kama kwamba ndio kwamba inatokea Tanzania wakati toka tunapata Uhuru ni Mikopo kwenda mbele. Na katika Mikopo yote huu ni mkopo mzuri zaidi"
Ni udhaifu mkubwa Sana kumshambulia ndugai I'll hali aliomba msamaha.Hii imetumiwa Kama defence,nahisi Kuna Mambo mazito Sana yanafichwa kwenye hi mikopo.ameshambuliwa ili kumpoteza.na kuopoteza hoja yake aliyoibeba.
 
Both ndungai na Majaliwa wafanye chap kesho asubuhi watangaze kujiuzulu maana soon wataumbuka.
Kwenye hiyo speech ukifatilia utagundua Samia anawachanganya wote ndugai na majaliwa kwenye hili seke-seke.
Anasema bunge la kina kasimu😂😁😀
 
Rais Samia Suluhu Hassan amesema ni Uhuru wa Mtu kusema chochote, lakini inashangaza Mtu anayetegemewa kushirikiana na Serikali kwenye safari ya maendeleo 'kuargue' kuhusu Tozo na Mkopo wa Trilioni 1.3 kwasababu taarifa zote za Uchumi zinapita kwake akisema, "Ni homa (fever) ya 2025, wasameheni"

Ameongeza, "Huwezi kuamini mtu mzima na unaenda kuargue tozo na mkopo wa Trilioni 1.3 kama kwamba ndio kwamba inatokea Tanzania wakati toka tunapata Uhuru ni Mikopo kwenda mbele. Na katika Mikopo yote huu ni mkopo mzuri zaidi"
Kosa anaenda kulifanya Mama ni kufanya mabadiko na kuwaweka kando anao dai wana stress ya 2025..hili kundi linaenda kukua sana linaenda kupambana kiukweli kuliko hata walivyo kuwa ndani ya serkali..
Mama angawaacha na kuwaita kwa pamoja kuonya bila wananchi kujua..
 
Eti Sasa michambo yoote ya nini.ni udhaifu mkubwa Sana.Anapaswa aheshimu nafasi ya ndugai kama Spika.
Ndugai ni mnafiki, kaomba msamaha wa kinafki ili kutuliza mambo huku akitafuta wakati mzuri wa kushambulia tena..sasa mama keshamgundua na kaamua hakuna kumpa chance tena huyu mnafiki..ni kumwaga mafuta ya taa shimon na kuwasha kiberiti mpaka nguchiro atoke mwenyewe shimon
 
Kiukwel mgogo angetulia tuu Sasa kamuomba msamaha shungi girl kajaa kichwaa

Nb mihimili ilioyobaki mahakama na bunge hamna kitu ni bora tubadili katiba ziwe wizara akuna cha mihimili hapo ni upuuz tu na majoho yao
 
Kimsingi amekosa sifa ya kuendelea kuwa kiongozi mkubwa wa kiwango hicho,na anatakiwa asaidiwe kwa kushuka kwenye nafasi hiyo,
Alifanya kosa kubwa kusimama hadharani kuitikisa mamlaka ya urais kitendo ambacho hakijawahi kufanywa na kiongozi yoyote anaejiambua nchini, alifanya Jambo jema Sana kuomba msamaha lakini akafanya kosa jingine kubwa zaidi kutaka kutuaminisha kwamba haikuwa vile Bali watu wa mtandao waliedit,Sasa Kama waliedit anataka msamaha wa Nini?!!,maana yake sisi sote tuliokasirishwa na kitendo chake hicho (akiwemo Mh.Rais wetu ) tunamuonea?! To me an apology is not accepted, it seems Bado anaendelea kutucheza shere watanzania, CCM tunaomba mtafakari Kama huyu mtu anatosha kuwa kiongozi wa watanzania,Hata naye ajipime Kama anatosha.
Hakika mamlaka kuu huwekwa na mwenyezi mungu na asiyethubutu kuamini hili na asubiri kudhalilika tu.
alafu kama mh. Rais angempongeza Job kwa kuomba msamaha,waweza kuta hapa ungemsifia mh. Rais kwa kuonesha uongozi na ushupavu na umahili mkubwa na maneno kama hayo...
yani ni sawa na wale alokuwa nao pale,ilipotangazwa umeme ni 27,000 walipiga vigelele wote na mh akiwemo,ila leo inasemwa elf 27 haiwezekani, wale wale tena wameshangalia hadi kwa kusimama na kupiga makofi
 
Mwanzoni kabisa niliwasikia watu wakisema bunge ni dhaifu.


Spika kaongea kidogo tu watu wamemvaa tena.


Kwahiyo mnataka nini??


Halafu suala la Rais wa nchi kuendelea na hili suala la mikopo ni ufinyu wa akili.

Mtu ameshaomba radhi.

Yeye bado kashikilia bango.

Poor thinking capacity.
Tumepigwa pale kuna dada yake hadija kopa full mipasho hakuna kiongozi
 
Hahaaaa!!!!hakika SUKUMA GANG ndembendembe
Kaa kwa kutulia, sasa hivi habari ya mjini ni andunje kushikishwa ukuta na bibi ushungi. Sukuma gang hamuamini kuwa Msoga line wamepindua meza. Hizi habari za gaidi fuatilia ww ili zikubebe kwenye mijadala humu ndani. Sasa hivi tunasikilizia kundi la dhalimu likishikishwa ukuta fullstop.
 
Ndugai muhuni. Hakukiri kosa na kusema eti watu walimdukua. Sasa mama kaushtukia huo uhuni akaamua ampe za uso.
Anajifanya kuomba msamah kimagumashi ili aachwe ajipange upya na genge lake wakiwa ndani kwa ndani.. vijana wa msoga wameshamshtukia, siasa siasani..msoga ndiko kilipo chuo cha mafunzo ya siasa za kuliana timing za ccm. Atagongwa na kitu kizito kichwan hatoamini.
 
Ninajua umuhimu wa katiba mpya,ila leo kupitia hotuba ya mh..nimeona zaidi umhimu huo wa katiba mpya
Nimesikiliza taarifa ya habari ya leo saa mbili usiku,nikasikia mahakama Nchini kenya imezuia agizo la serikali kuwa chanjo kuwa lamiza kwa kila mwananchi...nikatafakari kwahuku kwetu na katiba yetu hii,angeagiza mh. Rais kuwa chanjo ni lazima,alafu jambo lipelekwe mahakamani,ni nani huko Manama man I angekubali kukataa maagizo ya mh wakati kaona mhimili mwingine ulivofokewa leo?
kumbe katiba mpya ni mhimu itakayoweka utaratibu wa wakuu wa mihimili kupatikana bila kumhusisha Rais au ahusike kidogo sana na asiwe na nguvu yoyote dhidi yao baada ya wao kupatikana
 
Back
Top Bottom