Rais Samia amvaa Ndugai. Asema, "Huwezi kuamini mtu mzima ana-argue tozo na mkopo wa Trilioni 1.3"

Rais Samia amvaa Ndugai. Asema, "Huwezi kuamini mtu mzima ana-argue tozo na mkopo wa Trilioni 1.3"

Pamoja na yote kuhusu mikopo na tozo, ile kusema nchi itapigwa mnada ni kosa kubwa, Ina maana kwamba rais anauza nchi. Hakuna rais au kiongozi yeyote atakayeambiwa anauza nchi yake akubali. Vile vile kauli ya kuwa nchi itapigwa mnada ni uchochezi hasa inapotolewa na kiongozi anayetokana na chama tawala.
 
Kukopa siyo hiyari ni “lazima“ na “ukikopa“ kuna masharti ambayo ni lazima utimize kuna mengi ambayo yamejificha kama natural resources kuzipendelea Kampuni kutoka nchi zilizotoa fedha mfano sasa hivi Madini yetu ya Cobalt yanahitajika sana kwenye kutengeneza battery za electric cars hiyo ni mifano tu.
Na ndiyo maana Capitalist wanajificha nyuma vitu kama sijui mkopo wa kujenga madarasa na madawati lkn nyuma yake kuna mambo mengi sana.

Magufuli (RIP) alipokuwa anasema ni Vita ya Kiuchumi alimaanisha mambo kama hayo, yeye alikataa, kaingia huyu akafanya 180 degrees turn mara moja wala hakupoteza muda.

Deni la huo mkopo ni lazima lilipwe, sasa Bankers watazipataje fedha zao kutoka nchi masikiki kama yetu? Ndiyo hapo tozo inapokuja, kila mkopo una guarantee, tozo ndiyo guarantee yenyewe.
Magufuli hakukopa?,..
We jamaa unaongea nosense [emoji23]

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Rais Samia Suluhu Hassan amesema ni Uhuru wa Mtu kusema chochote, lakini inashangaza Mtu anayetegemewa kushirikiana na Serikali kwenye safari ya maendeleo 'kuargue' kuhusu Tozo na Mkopo wa Trilioni 1.3 kwasababu taarifa zote za Uchumi zinapita kwake akisema, "Ni homa (fever) ya 2025, wasameheni"

Ameongeza, "Huwezi kuamini mtu mzima na unaenda kuargue tozo na mkopo wa Trilioni 1.3 kama kwamba ndio kwamba inatokea Tanzania wakati toka tunapata Uhuru ni Mikopo kwenda mbele. Na katika Mikopo yote huu ni mkopo mzuri zaidi"
Thread 'Huenda adui Mkuu wa utawala wa Rais Samia akawa ni Spika Ndugai?' Huenda adui Mkuu wa utawala wa Rais Samia akawa ni Spika Ndugai?
 
Uhuru wa kutoa maoni, mama ajibu hoja sio mambo ya utu uzima, hoja ijibiwe Kwa hoja, tuache kupindisha na kukimbilia kujiudhuru huyu Wala yule, jibu hoja, sema mama nae hajiwezi tu kwani ukiwa mtu mzima ndo huhoji?
 
Kwakweli baada ya kuomba msamaha sikutegemea mtu mwingine aje na hii hii agenda...Huu si uungwana...Kama mtu kakosea na ameliona kosa lake ni busara kumwelewa na kusonga mbele
Itakua aliomba msamaha baada ya kutonywa kuhusu mkutano wa leo. Na ndo maana hata hakuhudhuria,,
Aliomba msamaha kinafig

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Kuna mtu atakopa aseme mkopo huu mbaya? Yeye kakopa lazima aseme katika mikopo yote mkopo huu wa tri 1.3 ndiyo mzuri zaidi.
 
Mwanzoni kabisa niliwasikia watu wakisema bunge ni dhaifu.


Spika kaongea kidogo tu watu wamemvaa tena.


Kwahiyo mnataka nini??


Halafu suala la Rais wa nchi kuendelea na hili suala la mikopo ni ufinyu wa akili.

Mtu ameshaomba radhi.

Yeye bado kashikilia bango.

Poor thinking capacity.
Mjomba hasira unajua inauma mtu unaemuamini halafu anakujakukusaliti na kuongea uwongo ili akuchafue uwonekane ufahi kwenywe jamii hivi kama yule mjinga pole pole kusema serikali hii ni ya mpito nawewe ndie boss wake utamchukuliaje kwa ufupi waache dharau
 
Mwambie Mama yako Samia kuwa hili suala lilishaisha na amechochoea na kuliamsha

Kama mtu ameomba radhi kwa kile kinachodaiwa kuwa ni ukosefu, basi jibu huwa ni moja tu kwa watu wenye maturity

You either not speak of it anymore au unasema tu ,Ndungai , Apology accepted !

Hiyo ndio maturity ya Akili kubwa; sio mambo ya kuchambana kama tupo kwenye Singeli la zuchu
Nakumbuka siku kinana anaomba msamaha,, lakini spana zikaendelea za akina musiba[emoji851][emoji851]

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Ninajua umuhimu wa katiba mpya,ila leo kupitia hotuba ya mh..nimeona zaidi umhimu huo wa katiba mpya
Nimesikiliza taarifa ya habari ya leo saa mbili usiku,nikasikia mahakama Nchini kenya imezuia agizo la serikali kuwa chanjo kuwa lamiza kwa kila mwananchi...nikatafakari kwahuku kwetu na katiba yetu hii,angeagiza mh. Rais kuwa chanjo ni lazima,alafu jambo lipelekwe mahakamani,ni nani huko Manama man I angekubali kukataa maagizo ya mh wakati kaona mhimili mwingine ulivofokewa leo?
kumbe katiba mpya ni mhimu itakayoweka utaratibu wa wakuu wa mihimili kupatikana bila kumhusisha Rais au ahusike kidogo sana na asiwe na nguvu yoyote dhidi yao baada ya wao kupatikana
Hivi huwa mnadhani nani atatuletea katiba?.


Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Kuna mtu atakopa aseme mkopo huu mbaya? Yeye kakopa lazima aseme katika mikopo yote mkopo huu wa tri 1.3 ndiyo mzuri zaidi.
Kumwamini mwanakijani ni sawa na kuamini maji kupanda mlima "naturally".
Jiwe alisema "tunajenga kwa pesa yetu ya ndani" huku Chief Hang Higher akisisitiza kwa kutikisa kichwa.
Leo anakiri ni mikopo kwenda mbele.
 
Kumwamini mwanakijani ni sawa na kuamini maji kupanda mlima "naturally".
Jiwe alisema "tunajenga kwa pesa yetu ya ndani" huku Chief Hang Higher akisisitiza kwa kutikisa kichwa.
Leo anakiri ni mikopo kwenda mbele.
Ajabu Sana. Anakopa na tozo juu
 
Serikali yake ituambie pesa za makusanyo ya tozo zinakwenda wapi mbona siku hizi hakuna update zozote?

Kwenye hii issue yake na Ndugai kwangu Ndugai ndie mshindi, yeye anafurahia ushindi anaodhani ameupata kwasababu tu kuna kundi kubwa la wanafiki nyuma yake wanaojali matumbo yao wako upande wake kwasababu ya mamlaka aliyonayo kama mkuu wa nchi, lakini hajashinda kwa nguvu ya hoja.
Ukweli mtupu huu.
 
Back
Top Bottom