Rais Samia Suluhu Hassan amesema ni Uhuru wa Mtu kusema chochote, lakini inashangaza Mtu anayetegemewa kushirikiana na Serikali kwenye safari ya maendeleo 'kuargue' kuhusu Tozo na Mkopo wa Trilioni 1.3 kwasababu taarifa zote za Uchumi zinapita kwake akisema, "Ni homa (fever) ya 2025, wasameheni"
Ameongeza, "Huwezi kuamini mtu mzima na unaenda kuargue tozo na mkopo wa Trilioni 1.3 kama kwamba ndio kwamba inatokea Tanzania wakati toka tunapata Uhuru ni Mikopo kwenda mbele. Na katika Mikopo yote huu ni mkopo mzuri zaidi"