Rais Samia amvaa Ndugai. Asema, "Huwezi kuamini mtu mzima ana-argue tozo na mkopo wa Trilioni 1.3"

Rais Samia amvaa Ndugai. Asema, "Huwezi kuamini mtu mzima ana-argue tozo na mkopo wa Trilioni 1.3"

Hicho ndo kitu pekee nilichotaraji kutoka kwa Mama. Ningeshangaa asingefanya hivyo. Ila hapo kwenye Mabadiliko asiishie kwenye baraza la mawaziri ashuke chini kwenye Makatibu, wakurugenze na wakuu mbalimbali wa Idara na taasisi. Huku chini ndo hawamsaidii kabisa na wanafanya hila za wazi kumuangusha. Piga kazi Mama tupo bega kwa bega hadi kieleweke
Huko kwa makatibu wakuu na wakurugenzi si alishabadilisha? Au abadilishe tena?
 
Tozo+kodi+Mikopo+vitu kupanda bei
 
Rais Samia Suluhu Hassan amesema ni Uhuru wa Mtu kusema chochote, lakini inashangaza Mtu anayetegemewa kushirikiana na Serikali kwenye safari ya maendeleo 'kuargue' kuhusu Tozo na Mkopo wa Trilioni 1.3 kwasababu taarifa zote za Uchumi zinapita kwake akisema, "Ni homa (fever) ya 2025, wasameheni"

Ameongeza, "Huwezi kuamini mtu mzima na unaenda kuargue tozo na mkopo wa Trilioni 1.3 kama kwamba ndio kwamba inatokea Tanzania wakati toka tunapata Uhuru ni Mikopo kwenda mbele. Na katika Mikopo yote huu ni mkopo mzuri zaidi"
Watanzania na Viongozi wetu tunafurahia mkopo na kuimba kbs.
 
Mama lazima alalame , maana ameshajua kuna watu chamani wanna lengo lao 2025, sasa anataka kupambana nao .
 
Anaendelea vizur anakula ugali wake taratibu. Vip huko kwako, yule mliwa na mafunza anasemaje?!!
Mliwa na mafunza yupi tena?

Maana ninavyojua ni kwmba sasa hivi mnapumua baada ya kuonewa sana kwa miaka 5.
 
Ndugai atakunywa sumu, hali yake ni mbaya sana

DB44574B-7442-4A42-8E71-E8D3593BF2B3.jpeg
 
Mliwa na mafunza yupi tena?

Maana ninavyojua ni kwmba sasa hivi mnapumua baada ya kuonewa sana kwa miaka 5.
Dah kumbe makijani ndo mnampa presha Samia? Na ungamo lote lile bado mmekataliwa?
 
Utabiri watimia?

Rais Samia amesema baada ya kuapishwa kuiongoza nchi, kuna mtu alimuambia kuwa anayeweza kumsumbua katika uongozi wake sio kutoka upinzani.

“Hapa inanikumbusha hadithi moja, kuna mtu mmoja nilipotwishwa huu mzigo akanitafuta alivyonipata akaniambia; mama nimekuja kukupa hongera lakini pole, nikamwambia napokea” amesema Rais Samia na kuendelea;

“Akanipa mawaidha mengiii akaniambia; lakini nataka nikuambie atakayekusumbua katika kazi yako na uongozi wako ni shati la kijani mwenzio wala sio mpinzani, huyo ndiye atakayekusumbua” amesimulia

“Shati la kijani mwenzio anayetizama mbele mwaka 2025-2030 huyu ndiye atakayekusumbua” anasimulia Rais akisema yameshatokea

“Nataka niwaambie ndicho kinachotokea, kwa sababu huwezi kufikiria mtu mliyemuamini, mshika muhimili aende akaseimame aseme yale, ni stress ya 2025” amesema
 
Alitakiwa amute na asimamie alichokiamini kama alikuwa na uhakika na hoja alizoibua kuhusiana na suala la mikopo. Kitendo cha kujitokeza na kutaka asamehewe kwa kutaka, kulazimishwa, kutokuusoma mchezo vizuri ama hata kwa kulazimishwa ndio kilifungua na kimefungua njia ya yeye kusimangwa.
 
Dah kumbe makijani ndo mnampa presha Samia? Na ungamo lote lile bado mmekataliwa?
Ujumbe wa Ndugai ulikuwa unauma, kuchoma na kukera ndio sababu unaona Hangaya kapanic namna ile!

Ule ujumbe wa Ndugai utaishi hadi 2025
 
Kwa hotuba ya leo ya Samia kama Ndugai asipojiuzulu basi hana akili timamu na anatumikia tumbo lake tu. Samia amesema wazi kuwa kilichomsukuma Ndugai kupinga mikopo ni Uchaguzi Mkuu wa 2025...
Ndugai ana fursa ya kuandika hostoria kwa bara ala Africa. Atapata heshima kubwa sana kama atajiuzulu sasa kwa sababu ya kushidwa kuelewana na Raisi wake kuliko kukomaa na kubakia madarakani bila maelewano ya serikali
 
Back
Top Bottom