Rais Samia ana hali mbaya kuelekea 2025, Wana-CCM wanatamani wapinzani wapewe nchi. Anaweza asipate hata 30% ya kura

Bro

Unamanisha kweli unachosema. Au na wewe umeshaingia kwenye orodha ya chawa. Nenda mtaani zungumza na wananchi. U don't need anya research methodology. Amka nenda mtaa wowote uliopo ongea na hao wanachi. Ukitoka hapo kamwambie mama ukweli!
Neno chawa limeanza awamu ya sita kama vile ni tabia ambayo awamu ya tano haikuwepo.

Hata wakati wa JPM walioulizwa walisema 'vyuma vimekaza' hivyo kauli au mawazo ya maisha kuwa magumu sio kielelezo halisi cha jitihada za serikali za kuondoa umaskini.

Miradi yote aliyoacha hayati JPM inaelekea kumalizika na kuna mipya ya awamu ya sita inaanza na itamalizika pia. Hakuna siku watu watahojiwa na kuridhishwa na serikali inayokuwepo madarakani.
 
 

Attachments

  • 75EEDDBC-EC82-4B9A-A63F-27F1413045A8.jpeg
    73.8 KB · Views: 2
Ni
Ni Kweli kabisa. Lakini unajua wakati wa JPM waliokuwa wanapiga kelele ni kina nani na kwa sababu zipi, na awamu hii wanaopiga kelele ni kina nani na kwa sababu zipi.
Kama huwezi kutofautisha hilo, napata mashaka Kama ni Philipo Bukililo yule au ama laa!
 
Atakayempa kura huyu kiongozi mzembe dhaifu asiye na akili inabidi ajitafakari sana
 
Umeme huu huu wa mgao au mwingine?? Kuna watu wajinga sana nchi huu
 
Ni Chama Dollar
Fitna , Ghiriba, Unafki Wote Wanaujua Hao
 
Atakayempa kura huyu kiongozi mzembe dhaifu asiye na akili inabidi

Umeme huu huu wa mgao au mwingine?? Kuna watu wajinga sana nchi huu
Mkuu mgao wa umeme upo Afrika ya Kusini na Malawi, uwe una tabia ya kufuatilia habari za mambo yanayoendelea nchi jirani zinazotuzunguka.

SSH anafanya kazi sana na hana propaganda kama watangulizi wake.
 
Apo kwenye sukuma gang kayataka mwenyewe kapangua safi yote ya sukuma gang af akaweka watu wa jk
 
Tupona Rais Samia Suluhu mpaka 2030
 
Juzi tu hapa Geita alipokuja Kinana walimwambiaa kabisa Samia hapendwi, mwanzoni kabisa mwa mwaka huu alikuja Shaka akasema Samia mitano tena wananzengo tena akina mama wa CCM wakasema NDOHOOOOO nilishangaa sana.
Kumbe yalishasemwa mengi
 
hakuna hata asilimia 5 ya wapiga kura kutoka mitandaoni endelea kupoteza muda , mama anapita Tena Kwa asilimia 89 narudia 89 na point kadhaa
 
ni lini ccm walitumia hesabu za kura halali toka sanduku ya kura kuingia ikulu
 
Hivyo, wapinzani wakijipanga vizuri 2025 na tukawa na Tume Huru, basi uwezekano wa wapinzani kushinda uchaguzi ni mkubwa mno kuanzia kwenye uraisi mpaka ubunge.
Hakutakuwa na Tume huru. CCM wataprint formu moja tu ya Mama. CCM watapora kama kawaida

Nothing changes. Kilichotokea 2005, 2010, 2015 na 2020 kitajirudia. If you keep doing the same thing, you will keep getting the same results.

Katiba mpya na Tume huru watu huwa hawapewi kwenye silver plate
 
Kwanza sio kweli kwamba mwendazake alikuwa anasifiwa tu. Kifo cha mwendazake kilivyopokelewa na jamii ina weza kukuthibitishia hilo labda pengine namna kifo kilivyopokelewa utuambie sio kweli ni watu walinunuliwa.

Mwendazake alisifiwa na kuamini sababu alitenda na vilionekana. Ndege zilizonunuliwa toka uhuru yeye alinunua ndege ndani ya muda mchache, meli zilizonunuliwa nyingine miaka 100 iliyopita ye alitengeneza kila mahali pamoja na vivuko, barabara na maji hata maeneo yaliyokuwa hayana ndoto za kuoata hizo huduma.

Alitoa elimu bure, akaongeza mikopo chuo kikuu na wanafunzi wakapata kwa wakati. Enzi zetu ilikuwa lazima muandamane ndio pesa inaingia.

Amekarabati shule na vyuo vikongwe, kajenga mahakama za wilaya na rufaa, hospitali, vituo vya afya.

Haya yote yamefanyika kwa macho na vinaonekana. Sasa ukisema alinunua vyombo vya habari ni hila, ghilba, chuki na husuda ambazo mtaamua kuzibeba wewe na wenzio.

Ila watanzania tunajua na dunia inajua na ndio wimbo wa Magu hautakoma midomoni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…