Rais Samia ana hali mbaya kuelekea 2025, Wana-CCM wanatamani wapinzani wapewe nchi. Anaweza asipate hata 30% ya kura

Rais Samia ana hali mbaya kuelekea 2025, Wana-CCM wanatamani wapinzani wapewe nchi. Anaweza asipate hata 30% ya kura

Bro

Unamanisha kweli unachosema. Au na wewe umeshaingia kwenye orodha ya chawa. Nenda mtaani zungumza na wananchi. U don't need anya research methodology. Amka nenda mtaa wowote uliopo ongea na hao wanachi. Ukitoka hapo kamwambie mama ukweli!
Hao wananchi wametapakaa nchi nzima kuanzia kusini mpaka kaskazini, sio kwamba mawazo ya mtaani kwa maana yako wewe ndio yanawakilisha kila sehemu ya TZ. Kuna mengi anayafanya SSH na yanagusa maisha ya kawaida kabisa ya kila mtu.

Na huyu ni mrithi wa JPM, ni chama kile kile hawezi kwenda tofauti na watangulizi wake tukumbuke juu ya ukweli huo.

Msipende kuita watu chawa kisa wanatofautiana mawazo na namna mnavyofikiri. Msikimbilie kudhalilisha watu wenye maoni tofauti na yale ya kwenu, mawazo hupingwa na yale yenye mantiki zaidi huwa hayapigwi virungu.
 
Tangu nianze kufuatilia siass za nchi hii, sijawahi ona kiongozi wa CCM alie madarakani akikataliwa, kupingwa na kuongezewa vivyo sivyo kama Mama yetu wa leo.

Kwanini hali hii?

1. Mama kulinganishwa na Mwendazake

Mama kulinganishwa na Mwendazake na hapa ndipo hata baadhi ya wana-CCM wanapoungana na watanzania wengine kumuhukumu na kumuona hatoshi na wanaona ni bora 2025 watafute mgombea mwingine vinginevyo ni bora wachague mpinzani.

Kwanini Mwendazake anamgharimu?
Wakati wa Mwendazake, kuna kundi kubwa la watanzania waliamini wizi na ufisadi vilikuwa vimekomeshwa/ vimedhibitiwa jambo ambalo halikuwa kweli kwa asilimia 100.

Mwendazake alidhibiti vyombo vya habar, alidhibiti Bunge, mitandao na vyanzo vingine vya kupashana habari matokeo yske tuhuma za wizi na ufisadi Wakati wa Mwendazake havikupata nafasi.

Kingine ni Mwendazake kutumia media kuendesha propaganda za kumsifu na kumtukuza mambo ambayo sasa hayapo kwa kiwango kile na hivyo kuleta tofauti kubwa ya kimtazamo kati ya Mama na Mwendazake.

2. Kundi la Sukuma gang
Hili kundi ni kundi la watu wanaonekana kuwa na chuki dhidi ya huyu Mama na ndio wanachangia sana kuonyesha kuwa Mama hatoshi sababu tu hawampendi. Ni kama hawakuta Mama amrithi Mwendazake na hivyo kutumia madhaifu ya Mama kummaliza kisiasa mbele ya umma.

Na kama Mama angeshindwa kuendeleza miradi iliyoachwa na Mwendazake, basi hili kundi lingepata cha kusema na lingekuwa kinara katika kuwaongoza watu wamkatae Mama hiyo 2025.

Mama akijitahidi kukamilisha Miradi yote iliyoachwa na Mwendazake, basi atafanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza nguvu za hili kundi mitandaoni na kwingineko

3. Madai kuwa Mzee wa Msoga ana influence katika uongozi wake
Madai haya ni moja ya mambo ambayo yanamgharimu sana Mama hasa ikizingatiwa Mzee wa Msoga anachukuliwa kama mtu alieacha rushwa na ufisadi vikatamalaki sana katika nchi hii.

Hivyo, madai kuwa Mama anafanya baahi ya mambo kwa influence ya Mzee wa Msoga, madai haya yanamgharimu sana kisiasa na 2025 atakuja kuona matokeo yake.

4. Madhaifu binafsi ya Mama
Madhaifu au mapungu haya ni pamoja na haya na kukithiri kwa tozo katika awamu yake, kauli za kuruhusu watu wale kulingana na urefu wa kamba zao, kushindwa kudhibiti mfumuko wa bei, kuhamisha wamasai kule Loliondo, safari za mara kwa mara nje ya nchi, kauli zake za majukwaani na mambo mengineyo.

5. Jinsia yake
Ukweli mwingine unatokana na mila na desturi zetu plus mtazamo potofu wa jumla kwa baadhi ya watu kuwa Mwanamke hafai kushika nafasi kama hio hivyo ni bora wakati ukifika, tumuweke mtu mwingine

6. Wanawake kutopendana
Madai kuwa wanawake huwa hawapendani, yanaweza kuchangia anguko la Mama na Wanawake wengi kwa sasa ni miongoni mwa watanzania wanaomuo Mama hatoshi.

Hivyo, kwa ujumla hayo ndio mambo yanayomgharimu Mama kwa sasa na ndio yatamgharimu vibaya sana 2025 na anaweza asipate hata asilimia 30 ya kura zote.

Ukitaka kuamini haya nayosema juu ya kukubalika au kutokubalika kwa Mama, fanya tu kautafiti kasiko rasimi kwa kuhoji tu watu mbalimbali utagundua wengi wanampinga na kutorodhishwa na uongozi wake wakiwemo hata watu wa chama chake.

Hivyo, wapinzani wakijipanga vizuri 2025 na tukawa na Tume Huru, basi uwezekano wa wapinzani kushinda uchaguzi ni mkubwa mno kuanzia kwenye uraisi mpaka ubunge.
Sisi watanzania tusio na vyama lazima tumchague tupo na Rais Samia Suluhu mpaka 2030 hii haina kupinga
 
Back
Top Bottom