Leo Rais Samia Suluhu ametusisitiza wananchi kutumia nishati safi ya kupikia ili tuondokane na madhara yatokanayo na nishati isiyo safi lakini pia amegusia suala la maji ambalo linawatesa sana wakazi wa Dar es salaam, Amesema
Lengo la kutoa elimu na kusisitiza matumizi ya nishati safi ya kupikia na kwenda kumtua Mama mzigo wa kuni kichwani.
Lakini pia Rais Samia Suluhu ameongezea kua "Tuliweka lengo nikiwa Makamu wa Rais kumtua Mama ndoo kichwani nina furaha kusema kwamba nime-cover kwa asilimia 80% ndani ya Tanzania ukiacha 'effects' hizi za mabadiliko ya tabia ya nchi, Ukame unaotuandama lakini 'coverage' ya upatikanaji wa maji Tanzania ni asilimia 80%. Nitajisikia fahari ikifika 2032 Tanzania hii iwe na Nishati safi kwa asilimia 90 kama sio zote"
Pia Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amosi Makalla amesema katika kukabiliana na mgao wa maji unaoendelea Dar es salaam, usiku wa leo zitaingizwa lita Milioni 70 za maji kutoka kigamboni katika visima 12 ili kupunguza ukali wa mgao wa maji.
Rais Samia Suluhu anaendelea kufanya jitihada za kumtua mama ndoo kichwani na kumtua mama kuni kichwani