Rais Samia ana nia njema Watanzania wapate haki, ila Watanzania hawajui Haki! Je, Tumsaidie kuelimisha umma Katiba, Sheria na Haki au?

- Lissu kulipwa haki zake ni stahili yake, hilo halihitaji huruma ya jicho la kizanzibari,
Serikali inafanya kazi kwa mfumo wa maandishi kwa kutumia sheria, taratibu na kanuni, utaratibu wa matibabu nje ya nchi kwa mtumishi wa umma, lazima apate authorization ya serikali, Lissu alikwenda kutibiwa Nairobi na Belgium kinyume cha utaratibu, hivyo the government had a bonafide genuine justification ya kugoma kumlipia. Hivyo kiserikali Lissu alikuwa ni mtoro kazini, japo kila mtu aliona kilichomtokea Lissu, but no one did a due process na kwenda kuripoti kazini kwaķe, hivyo ulipofika muda prescribed na kanuni ofisi ya Bunge ikafanya a due process na kumfuta kazi hivyo kupoteza haki zake zote!.

Alichofanya Mama Samia ni kutumia utu na sio sheria taratibu na kanuni. Kisheria taratibu na kanuni, Lissu alikuwa hana haki, lakini Mama Samia akatumia utu kuwa hata kama taarifa rasmi haikupelekwa Bungeni kiofisi, lakini ni kweli Lissu alishambuliwa kweli alilazwa Nairobi na baadaye Belgium, na kuamuru alipwe haki zake zote na kulipiwa matibabu yote!. Huu ni wema na Lissu alimshukuru sana Samia.
lakini la Mbowe kugharimiwa safari za nje bado nataka ushahidi,
Maadam aliyetoa pesa akasema na aliyepokea pesa hajasema who M I kusema?.
na Lissu kurudi nchini nae nataka ushahidi wa kulipiwa nauli, naona umeshaanza kuingiza maslahi ya CCM yako hapa.
Sijasema Lissu kalipiwa nauli, nimesema usikute!, kama Mbowe kalipiwa trip ya overseas, why not Lissu?.
Hapo ulipolazimisha wale wanawake 19 waendelee kuwa wanachama halali wa Chadema ndio imebidi nicheke tu, naamini haya yatakuwa maagizo mmepewa makada wote ili kukibeba chama chenu.
Amini usiamini mimi Pasco mayalla situmiki na yeyote, amini nakuambia wabunge hao bado ni wanachama hai na halali wa Chadema mpaka hapo Mahakama itakavyo tamka otherwise.

Kwenye hili la hawa mashujaa 19, mimi nasimama nao hadi haki itendeke.
Uanachama kwenye vyama vya siasa uko regulated kisheria, kikanuni, na kiutaratibu, haufukuzi mwanachama wako kama unafukuza mbwa!.
Maadam Chadema inao utaratibu wa nidhamu kwa mujibu wa katiba yake, kwanini hawakufuata utaratibu wa nidhamu wa katiba yake?!.

Kwa mujibu wa katiba ya Chadema, mamlaka ya nidhamu ya NKM Zitto ni Baraza Kuu, CC ya Chadema ilipata wapi mamlaka ya kumtimua Zitto?. Zitto alikimbilia mahakamani kesi akashindwa kwa legal technicalities na sio kwa haki!. Matokeo yake ni Chadema kama chama kimekula bakora za karma za kutosha kutoka wabunge zaidi ya 50 hadi mbunge mmoja wa ngama!. Na viongozi waliohusika na kumtimua Zitto, kila mmoja wao amekula bakora zake za karma za kutosha individually.

CC ya Chadema sio mamlaka ya nidhamu ya Halima Mdee!, mamlaka yake ya nidhamu ni Baraza Kuu, CC ya Chadema imepata wapi mamlaka ya kumtimua Halima Mdee?.
Ninachojua; bunge halipo juu ya maamuzi ya vikao halali vya Chadema.
Ni kweli Bunge haliko juu ya maamuzi halali ya vikao halali vya Chadema, kwa vile kwa sasa kesi iko mahakamani, this is not for me or for you kuusema uhalali wa vikao vile ambayo mimi niliieta Kangaroo court, let the court speak!.
P
 
Magufuli alisema msaliti wa nchi hatakiwi kuishi na baada ya masaa machache nikapigwa risasi ~~~~~ Lisu.

Kumbe anajijua kabisa ni msaliti
 
Unataka usisemwe kama hayati Magufuli? Basi kaa kimya, acha kuandika mambo ya kichawa. Ukiandika tu lazima turuke na wewe, lazima UJIBIWE ipasavyo. Mwanasheria gani wewe usiyejua umuhimu wa Katiba imara na yenye maslahi kwa wote?
 
Unataka usisemwe kama hayati Magufuli? Basi kaa kimya,
Kuna watu wanashughuli mbali mbali za kuendesha maisha yao, hao ndio wanaweza kukaa kimya, lakini mimi kuongea ndio shughuli yangu ya kuendeshea maisha yangu hivyo siwezi kukaa kimya.
acha kuandika mambo ya kichawa. Ukiandika tu lazima turuke na wewe, lazima UJIBIWE ipasavyo.
Duh...!, naomba kuheshimu maoni yako, kwa vile mimi naandika hoja nyingi, kama unaziona ni za kichawa, huo ni mtazamo wako na nauheshimu, ila mtu ukijijua sio chawa na wala huandiki kichawa, akitokea mtu akakudhania chawa, na akakuita chawa, kuitwa huko chawa hakutakufanya uwe chawa!.
Mwanasheria gani wewe usiyejua umuhimu wa Katiba imara na yenye maslahi kwa wote?
Hivi ndivyo wanasheria wa Tanzania tulivyo, tuna wanasheria kibao manguli wabobezi na wabobevu lakini hawaijui katiba, hivyo mwanasheria mimi, nimeamua kuanza kwa kuwaelimisha wengine kuhusu katiba hivyo angalia hapa nimesema nini kuhusu katiba mpya Watanzania ni maneno maneno na kulialia, Vitendo 0. Katiba ni maneno tu! Je, 2023 tuendeleze maneno matupu na kulialia au tubadilike tufanye kitu? na sikuishia kusema, bali nimeendesha darasa Ijue Katiba ya JMT-1: Katiba ni Nini, ya Nani, ya Kazi Gani?. Msemo "Katiba Ndio Kila Kitu" Una Maana Gani?. Katiba Ina Umuhimu Gani?
P
 
Hoja za bandiko hili zimejibiwa na kampeni hii!. Uzinduzi wa Mama Samia Legal Aid Campaign - Sheria ya Ardhi ni ya Mwaka 1999 na Sio 1995
P
 
Ni kweli pia kwamba mwamko wa Watanzania kutafuta haki ni tatizo,
Mkuu Nguruvi3 , naunga mkono hoja kwamba mwamko wa Watanzania kutafuta haki ni tatizo, na kwa utafiti wangu, tatizo kubwa sio Watanzania hawajui kutafuta haki, bali Watanzania hawazijui haki zao!. Hawazijui haki zao kwasababu hawaijui katiba yao, na hawazijui sheria zao!. Hivyo kitu cha kwanza cha kuwasaidia Watanzania ni kuwaelimisha, elimu ya Katiba, Sheria, na haki, ili sasa ndipo wahamasishwe na wapate mwamko wa kuzidai haki zao.

Kwenye hili mimi nimejitolea
View: https://youtu.be/ZJIKhnZCf04?si=mk9eDysfE-QeSJRP
Naombeni mniunge mkono, na ikitokea fursa kuwaita kushiriki katika kipindi, jitokezeni bila mimi kusema huyu ndiye Nguruvi3 au huyu ndiye JokaKuu
P
 
Hatimaye hoja za bandiko hili zinakwenda kuwa implemented

View: https://youtu.be/ZJIKhnZCf04?si=IXfA8sZkNPxpaeZnP
 
Wanabodi,
Nimelipitia bandiko hili na kuumia sana kwa kilichotokea hadi kifo cha huyu Mzee Kibao wa Chadema, ameuliwa kwasababu wananchi hawajui haki zao!.
1. Police haruhusiwi kumkamata mtu yoyote bila kwanza kujitambulisha yeye ni nani na ametokea kituo gani kwa kuonyesha kitambulisho cha polisi.
2. Mtu anayekamatwa ana haki ya kusoma number ya kitambulisho na kuihakiki kwenye mfuko wa kushoto wa nguo ya polisi.
3. Wakija polisi ambao ni askari kanzu, hawa hawana uniform hivyo hawavai numbers, hawaruhusiwi kumkamata mtuhumiwa bila kuandamana na polisi wenye uniforms!.
4. Mtu yeyote kabla hajakamatwa lazima awe na arrest warrant na lazima aripoti ofisi ya serikali ya mtaa husika!, aonyeshe arrest warrant atasibdikizwa na mtendaji wa mtaa kuja kukukamata.
5. Baada ya polisi kujitambulisha kwa kuonyesha kitambulisho, kitu cha pili ni kuonyesha arrest warrant na kukumbia
6. "Uko chini ya ulinzi, lazima aseme unakamatwa kwa kutuhumiwa kwa kosa gani?.
7. Polisi atatamka maneno haya " You have the right to remain silent, anything you say may be used for you or against you before the court of law"
Hii maana yake una haki ya kunyamaza kimya, chochote utakachosema kinaweza kutumiwa kama ushahidi wa kukusaidia au kukuangamiza mahakamani!.
8. Kitu cha tatu atakueleza "you have the right to legal representation", una haki ya uwakilishi wa kisheria.
9. Hapo atatoa pingu na kukufunga.
10. Kisha polisi hao watawaeleza hao mashuhuda wanakupeleka kituo gani ili ndugu zako wakufuatilie!.

Na ukifikishwa kituoni kabla hujaandikishwa maelezo unaaelezwa haki zako ikiwemo haki ya legal representation.

Haki hizi zikifundishwa kwa wananchi, 'wasiojulikana' watapungua, watabaki tuu wale wa pyu pyu kama wa Lissu.

Paskali
 

Tutofautishe utekaji na ukamataji.

Ni wazi utekaji ni kinyume cha sheria ila ndiyo wanaoufanya.
 
HBD Rais Samia!.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…