Rais Samia anafahamu changamoto ya umeme nchini, tuombe mvua zinyeshe. Hata yeye anaumia

Rais Samia anafahamu changamoto ya umeme nchini, tuombe mvua zinyeshe. Hata yeye anaumia

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu kumekuwa na malalamiko juu ya changamoto ya umeme Hapa Nchini, Hali iliyosababishwa kwa kiasi kikubwa na Hali ya ukame iliyoikumba nchi yetu na kupelekea kupungua kwa kina Cha maji katika mabwawa yetu ya kuzalishia umeme, Sote tunafahamu umuhimu wa umeme katika uchumi wetu, umuhimu wa umeme katika shughuli za kijasiriamali, umuhimu wa umeme katika uzalishaji wa bidhàa za viwandani, Tunafahamu umeme ndio kila kitu hapa nchini katika shughuli karibu zote za kiuzalishaji, umeme ndio uwekezaji wenyewe kwa wawekezaji,wafanyabiashara,wamiliki wa viwanda,

Umeme unamgusa kila mtu na kila mmoja kuanzia wajasiriamali wadogo Hadi wafanyabiashara wakubwa, huku chini kabisa utawakuta vinyozi, watu wa gereji, watu wakuchomelea mageti, madirisha n.k, watengeneza barafu wote wanategemea umeme, wauza vinywaji vya baridi, wauza samaki wabichi, n.k. umeme ndio ajira kwa vijana walio wengi , umeme ndio kula ya watu, ndio Ada za watu, ndio chanzo Cha michango kwa Wana vicoba, ndio Ada za watoto shule, ndio maisha ya wengi, Umeme ndio Taa ya Taifa Na Ndio Mwanga Wa nchi yetu

Hii ndio sababu unaona suala hili linamgusa kila mtu na kumuumiza kila mtu, ndio sababu ya kuona kila eneo watu wakiwa wamekaa wakisubiri umeme uwake, ndio sababu ya kuona watu wakiwa wanyonge na wapweke wakisubiri umeme,ndio sababu unaona watu wakiwa wanaendelea kumwangaliaa na kumsikiliza mh Rais wetu mpendwa na kipenzi Cha watanzania juu ya suala hili la umeme, ndio sababu ya kuona watanzania wakiendelea kuomba Mvua inyeshe ili isaidie kupunguza changamoto hii

Ikumbukwe kuwa Ni watanzania wachache Sana wenye uwezo wa kuweza kununua na kutumia jenereta, ndio sababu ya kuona miji ikiwa kimya pale panapokuwa pamekatika umeme, Ndio sababu ya kuona shughuli zote zinazotegemea umeme zikiwa zimesimama pale umeme unapokuwa umekatika

Jambo pekee tunalopaswa kulifahamu watanzania ni kuwa Rais wetu mpendwa Mama Samia analifahamu suala hili,anaumizwa na suala hili,anasononeshwa na suala hili, anateswa na suala hili la umeme, ana huzunishwa na suala Hilo, analia na suala hili, anakosa usingizi kwa suala hili ,anahangaika huku na kule kwa suala hili, hakai Alipo kwa suala hili,anatoa maelekezo muda wote juu ya suala hili, analia na watanzania na anapata maumivu tuyapatayo watanzania lakini yeye kwa kuwa Ni kiongozi wetu anakwenda mbele yetu hatua kadhaa kutatua tatizo hili,ndio sababu ya kuona serikali ikiweka mkakati wa kuamua kutumia Hadi gas kuzalisha umeme ili kupunguza makali,

Watanzania Tuendelee kumwamini Rais wetu, Tuendelee kuwa na Subira, Tuendelee kumsikiliza, Tuendelee kumtia moyo katika wakati huu wa mapambano, Tuendelee kuwa naye bega kwa bega, Tuendelee kumwomba Mwenyezi Mungu Atupatie mvua nyingi zenye baraka na Neema zisizo na madhara kwa maisha yetu Wala kuleta maafa na uharibifu wa Miundombinu, Rais wetu anayo dhamira njema na Taifa letu,Ni mzalendo aliyeiva na anayeipenda nchi yake

Rais wetu Hapendi Wala kufurahishwa na Hali hii, hapendi kuona watanzania tukiwa gizani,hapendi kuona akifanya juhudi kubwa za kuvutia wawekezaji halafu waanze kupata changamoto ya umeme,anajuwa Jambo Hilo litawakatisha tamaa wawekezaji,anajuwa ukosefu wa umeme utasababisha bidhàa kupanda Bei hasa pale zinapozalishwa kwa kutumia mafuta, anatambua Jambo hili litapunguza na kuyumbisha uchumi wa Kaya nyingi na kupelekea Hali ya umaskini wa kipato, maana hata Mimi Nina mdogo wangu Ni Fundi kuchomelea lakini mpaka Sasa anashindwa kupata hela kutokana na changamoto hii, hata hivyo bado Anayo Imani na serikali ya mama Samia Kama ilivyo kwangu na watanzania wote tulivyo na imani na Rais wetu mpendwa Mama Samia Suluhu Hassan,Hivyo Rais wetu Mama Samia hawezi kukubali watanzania Tuwe wanyonge,ndio sababu ya kuona namna serikali ikipambana juu ya suala hili

Mwisho Tuendelee kupeana Elimu juu ya utunzaji wa mazingira yetu ,misitu yetu ,vyanzo vyetu vya maji, tusiharibu na kuchoma hovyo misitu yetu, lakini kubwa kuliko Tuendelee kumwomba mwenyezi Mungu Atupatie Mvua katika Taifa letu, Tupige magoti kila mmoja kwa Imani yetu na tujinyenyekezi na kujongea mbele zake,Tanzania yetu chini ya uongozi shupavu wa Mama Samia Ni salama na imara Sana ,Ni Tulivu na yenye amani na usalama wa kutosha ,Tumwamini Rais wetu na Tuwe na Subira maana ni kiongozi mwenye huruma upendo na Shupavu Sana

Kazi iendeleee,mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.: 0742-676627
 
Ndugu zangu kumekuwa na malalamiko juu ya changamoto ya umeme Hapa Nchini, Hali iliyosababishwa kwa kiasi kikubwa ndwa na kipenzi Cha watanzania juu ya suala hili la umeme, ndio sababu ya kuona watanzania wakiendelea kuomba Mvua inyeshe ili isaidie kupunguza changamoto hii

Mwisho Tuendelee kupeana Elimu juu ya utunzaji wa mazingira yetu ,misitu yetu ,vyanzo vyetu vya maji,tusiharibu na kuchoma hovyo misitu yetu, lakini kubwa kuliko Tuendelee kumwomba mwenyezi Mungu Atupatie Mvua katika Taifa letu, Tupige magoti kila mmoja kwa Imani yetu na tujinyenyekezi na kujongea mbele zake,Tanzania yetu chini ya uongozi shupavu wa Mama Samia Ni salama na imara Sana ,Ni Tulivu na yenye amani na usalama wa kutosha ,Tumwamini Rais wetu na Tuwe na Subira maana ni kiongozi mwenye huruma upendo na Shupavu Sana

Kazi iendeleee,mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.: 0742-676627

Hahahaha Leo umeweka na namba ya simu, kuna siku nilikwambia ukajifanya utaki naona Leo umeweka

Pia Acha kumsemea Rais kuna siku utakuja kupata matatizo

Unamuongelea Rais kama mtu tu wa mtaani unamwandika Kwa mambo ambayo Huna fact nayo

Urais sio Mtu ni taasisi na ina wasemaji wake
 
Kwa hiyo kwa akili yako unafikiri mh Rais anapenda umeme usiwepo hapa nchini? Au ulitaka kusema Nini mkuu
 
Ww ni msemaji wa taasisi ya urais? Au unaongea Kwa mamlaka gani?
Dhamira ya mh Rais ipo wazi na ambapo amekuwa akieleza wazi juu ya suala hili la umeme na masula mengine mengi yaliyo katika ilani ya ccm
 
wewee humpendi Rais unajifanya mjuaji zaidi anakuona wewe ni mjinga unajipendekeza kwenye hamna tumia akili yako unajenga hoja za kipuuzi tu huna lolote mwanaume acha kujipendekeza Rais mwenyewe anakuona mshamba Sana
 
Naona hunajenga hoja ukaeleweka badala take imebaki umepaniki tu,ukitulia njoo tena na hoja yenye mashiko halafu nitakujibu kwa utulivu hekima busara na upendo
 
Dhamira ya mh Rais ipo wazi na ambapo amekuwa akieleza wazi juu ya suala hili la umeme na masula mengine mengi yaliyo katika ilani ya ccm

Ww ni msemaji wa ilani ya ccm ? Au ww ni msemaji wa taasisi ya urais wa tanzania? Au unayasema hayo Kwa mamlaka gani?

Huo uchawa wenu wa kijinga utakuja kuwatokea puani

Unatoa maelezo ya rais wa kama Nani?
 
Kwani ilani ya CCM unafikiri ipo uvunguni? Unafikiri haijulikani umesema Nini katika kila secta? Unafikiri kazi na wajibu wa mwanachama wa CCM Ni upi? Unafikiri ilani ya CCM ililenga kumnufaisha Rais wa nchi gani?
 
Mimi nashangaa waziri ameshindwa kujibu swali la takwimu, ila wewe mpiga debe usiye na access unaropoka tu.
 
Ww ni msemaji wa ilani ya ccm ? Au ww ni msemaji wa taasisi ya urais wa tanzania? Au unayasema hayo Kwa mamlaka gani?

Huo uchawa wenu wa kijinga utakuja kuwatokea puani

Unatoa maelezo ya rais wa kama Nani?

Huyo ni wa kumwonea huruma. Anafikiri kwa kuongea mambo ya Rais atapata teuzi.
 
Back
Top Bottom