Rais Samia anafahamu changamoto ya umeme nchini, tuombe mvua zinyeshe. Hata yeye anaumia

Lengo lako upate teuzi. Na hautapata
kamwe, maana uchawa wako ni wa kiwango Cha kushtua hata kwa yule unayemsifia anakuona mnafiki, maana unasifia uongo.
Mimi Hakuna nilipoongelea habari za uteuzi hapa na Wala hii siyo barua ya maombi na Wala huwa siandiki hapa barua ya maombi , Bali huandika hapa Kama jukwaa huru la kutoa mawazo yangu, lakini pia Ni Bora ungeeleza kinagaubaga huo uongo nilipoandika hapa ili nipate nafasi ya kujibu hoja kuliko ulivyoandika jumla jumla tu pasipo hoja ya msingi
 
Hahahaha Leo umeweka na namba ya simu, kuna siku nilikwambia ukajifanya utaki naona Leo umeweka

Pia Acha kumsemea Rais kuna siku utakuja kupata matatizo

Unamuongelea Rais kama mtu tu wa mtaani unamwandika Kwa mambo ambayo Huna fact nayo

Urais sio Mtu ni taasisi na ina wasemaji wake
Huyo ni "Gerson Msigwa" akiwa Mbozi.😂😂😂😂
 
Mimi Hakuna nilipoongelea habari za uteuzi hapa na Wala hii siyo barua ya maombi na Wala huwa siandiki hapa barua ya maombi , Bali huandika hapa Kama jukwaa huru la kutoa mawazo yangu, lakini pia Ni Bora ungeeleza kinagaubaga huo uongo nilipoandika hapa ili nipate nafasi ya kujibu hoja kuliko ulivyoandika jumla jumla tu pasipo hoja ya msingi
Ila kwa kujitoa ufahamu haujambo.😂😂😂😂
 
Mimi nashangaa waziri ameshindwa kujibu swali la takwimu, ila wewe mpiga debe usiye na access unaropoka tu.
Mimi siropoki Bali naongea ukweli na Wala pia Waziri hajashindwa kujibu swali Kama u avyotaka kupotosha hapa maana Waziri ametoa takwimu kulingana na namna zinavyokusanywa na watalaamu
 
Huyo ni wa kumwonea huruma. Anafikiri kwa kuongea mambo ya Rais atapata teuzi.
Naona akili yako na mawazo yako yote umeyaegesha katika uteuzi na kushindwa kujadili hoja kwa kuwa umepofushwa na habari za uteuzi
 
Mimi siropoki Bali naongea ukweli na Wala pia Waziri hajashindwa kujibu swali Kama u avyotaka kupotosha hapa maana Waziri ametoa takwimu kulingana na namna zinavyokusanywa na watalaamu
Siyo lazima kujionesha unajua na kuweza kila kitu.Wakati mwingine uwe unatulia na kusoma tu wanayoandika wenzio.Unajua hadi unapitiliza?
 
Mwanasiasa anayekimbillia kwenye tufanye maombi ni yule asiyetaka kuwajibika. Upungufu wa Megawatt 300 tunaingia kwenye mgao! Kulikuwa na haja gani ya kununua madege, kwanini hatuwekeza zaidi ya kwenye umeme wa gesi utoshe mahitaji yetu?
 
Msukuma sifa yake ni kumiliki baiskeli,kucheza chagulaga,kilimo cha kufa na kuzikana na kutumia wali kama mboga.Hayo mengine labda alazimishwe.
 
Mwanasiasa anayekimbillia kwenye tufanye maombi ni yule asiyetaka kuwajibika. Upungufu wa Megawatt 300 tunaingia kwenye mgao! Kulikuwa na haja gani ya kununua madege, kwanini hatuwekeza zaidi ya kwenye umeme wa gesi utoshe mahitaji yetu?
Hatupaswi kutegemea chanzo kimoja pekee Cha Nishati yetu ya umeme, hata tukitumia umeme wa gas bado tutauhitaji umeme wa maji pia ambao Ni nafuu Sana kigharama, hata mataifa makubwa bado yanaendelea kutumia vyanzo mchanganyiko katika uzalishaji wa umeme ikiwepo huu wa maji
 
Siyo lazima kujionesha unajua na kuweza kila kitu.Wakati mwingine uwe unatulia na kusoma tu wanayoandika wenzio.Unajua hadi unapitiliza?
Nasoma mengi tu humu yanayoandikwa na wengine kwa kadri ya uwezo wangu na kwa kadri navyopata muda na kuwa na salio la kuingia humu, hata kwa wanaonikosoa kwa hoja Napo pia natazama uzito wa hoja zao na kwa wanao nitukana hao Sina shida nao maana najuwa Ni kushindwa kukabili hoja ndiko kunakokuwa kunawatesa
 
Sawa.Ila uwe unaandika kwa punctuation.Maelezo marefu hivyo kwa mstari mmoja bila hata nukta?Luca acha vituko!
 
Hatupaswi kutegemea chanzo kimoja pekee Cha Nishati yetu ya umeme, hata tukitumia umeme wa gas bado tutauhitaji umeme wa maji pia ambao Ni nafuu Sana kigharama, hata mataifa makubwa bado yanaendelea kutumia vyanzo mchanganyiko katika uzalishaji wa umeme ikiwepo huu wa maji
Hakuna anayekataa kuwa tunahitaji mchanganyiko wa vyanzo vya umeme, swali ni kwanini tunategemea chanzo ambayo kinaathiriwa na upatikanaji wa mvua? Na kwanini tulitumia mabilioni kununua ndege wakati tungeweza kutengeneza Kinyerezi nyingine kama 3 kwa hizo pesa na kuondoka kabisa kwenye hii challenge?

Tuna shida ya priorities sio resources
 
Back
Top Bottom