Rais Samia anafahamu changamoto ya umeme nchini, tuombe mvua zinyeshe. Hata yeye anaumia

Uhuru wako sio Kwa kumsemea rahisi wa inchi

Kuwa mkristo hakukupi mamlaka ya kuusemea ukristo

Kuwa mtanzania hakukupi mamlaka ya kila ukiamka asubuh umeshiba maandazi unaongea mambo ya rais Kwa lugha nyepesi kabisa
Nifundishe lugha ngumu Kama unaona lugha nayotumia Ni nyepesi
 
Trab na Trat
 
Ww unamsemea kama Nani? Mwakilishi wake? Msemaji wake? Au msemaji wa taasisi ya urais?

Tukusikilize ww au shaka au msigwa au zuhura?
Hakuna mahali niliposema Mimi Ni msemaji wa Rais au Serikali
 
Mimi naongea ukweli na siyo kutetea uozo maana serikali ya mama Samia Ni serikali sikivu na nyenyekevu kwa watanzania
Utumwa wa fikra kwa kumpa sifa chanya mtu anayefanya matendo hasi ni uharifu na unastahili adhabu kwa mjibu wa sheria. Hajawahi kufanya vizuri, hafanya vizuri na hatakuja kufanya vizuri kwa vyovyote vile kama sio kuwaneemesha wenye matumbo na kuwaacha wananchi walio wengi wakiteseka bila faraja halisia.
 
Lengo lako upate teuzi. Na hautapata
kamwe, maana uchawa wako ni wa kiwango Cha kushtua hata kwa yule unayemsifia anakuona mnafiki, maana unasifia uongo.
Mkuu bado hatujakombolewa kofikra
Hapa Ni jukwaa huru kwa ajili ya kutoa mawazo yetu kwa ujenzi wa Taifa letu,
Mawazo ndo unaacha na namba ya simu?? Au pengine umechelewa kuijua mitandao.
 
Kama Suluhisho ni kuomba Next Time tumchague Mchungaji au Sheikh, Pasta au Padre au Mpiga Ramli..., ili atuongoze vizuri kwenye maombi..., Au asipwepo yoyote pale juu hizo Kodi tupeleke kwenye nyumba za Ibada kuwaongezea Sadaka / Motisha
 
Acha chuki zako kwa mh Rais, kwamba hujaona maendeleo yaliyofanywa na mh Rais katika secta zote? Hujaona ujenzi wa vituo vya Afya? Hujaona ujenzi wa shule na vyumba vya madarasa,hujaona utoaji wa Elimu bure mpaka kidato Cha sita? Hujaona ongezeko la bajeti katika wizara zote Kama ilivyo katika kilimo? Hujaona utolewaji wa mbolea za Ruzuku? Eneo gani ambalo halijaguswa kiutendaji na mh Rais? Acha chuki zako na hata hivyo umechelewa Sana maana watanzania wanamuunga mkono Rais na kumkubali utendaji kazi wake
 
Wanaomuunga mkono ni Pwani maeneo ya Chalinze, Mkuranga, Kigoma na wafanyabiashara wakubwa wasio waaminifu ambao ni asilimia 15% ukiwemo wewe na wanufaika wa kulamba asali

Asilimia 85% wana jambo lao wewe endelea kupoteza muda wa kusifia hewa
 
Tatizo kipindi mambo ni magumu, ajira, mfumuko wa Bei, ajali, mgao wa maji, mgao wa umeme , rushwa nk bado wewe huoni hizo changamoto umebaki kusifia ujinga. Kisa Tumbo lako unaona shida zinazowapata wananchi hazikuhusu. Punguza unafiki.
 
Ulaya Mungu haishi huko hivyo wao changamoto zote hawaombi ila wao wanatengeneza vifaa vya kuzalisha umeme.
 
Kwa hiyo kwa akili yako unafikiri mh Rais anapenda umeme usiwepo hapa nchini? Au ulitaka kusema Nini mkuu

Kama ili umeme uwepo ni lazima tuombe mvua inyeshe, yeye anakuwa rais na kulipiwa kila kitu kwa kodi za wananchi ili iweje? Kwanini yeye tunayemlipa asiende kuomba hiyo mvua ili tupate umeme.
 
Kama ili umeme uwepo ni lazima tuombe mvua inyeshe, yeye anakuwa rais na kulipiwa kila kitu kwa kodi za wananchi ili iweje? Kwanini yeye tunayemlipa asiende kuomba hiyo mvua ili tupate umeme.
Tindo Kwani huzioni juhudi za serikali katika kushughulika na changamoto hii, na kwa Sasa Kuna mikakati ya muda mfupi ,wa Kati na mrefu wa kuumaliza kero hii Kama ambavyo tumekuwa tukielezwa na serikali yetu inayoongozwa na mama Samia, Tuwewavumilivu na wenye Subira na Tuiamini serikali yetu, itatuvusha hata katika hili hasa kwa kuzingatia kuwa mvua zimeshaanza kunyesha katika baadhi ya maeneo hapa nchini, kila changamoto huja na somo,hata katika hili naamini serikali yetu imejifunza Jambo hususani katika vile vyanzo vya Nishati yetu ya umeme
 
Ulaya Mungu haishi huko hivyo wao changamoto zote hawaombi ila wao wanatengeneza vifaa vya kuzalisha umeme.
Hata ulaya walipitia haya tunayopitia leo, na katika mapito hayo walikuwa wanajifunza kwa kila pito watakalo pitia, hata sisi tutavuka na kuvushwa na serikali yetu Hii shupavu ya Mama Samia
 

Changamoto za umeme nchi hii ni zaidi ya miongo mitatu, na chama kilichotutia hasara kwenye upande huo ni hiki hiki. Sasa unapoweka maandashi marefu kuleta excuse za kijinga sijui unaaminisha nini. Ww sio mpambe wa kwanza kumsifia rais aliyeko madarakani hapa jukwaani. Walikuwepo wenzio na walikuwa na porojo hizihizi kama ww.
 
Tatizo kipindi mambo ni magumu, ajira, mfumuko wa Bei, ajali, mgao wa maji, mgao wa umeme , rushwa nk bado wewe huoni hizo changamoto umebaki kusifia ujinga. Kisa Tumbo lako unaona shida zinazowapata wananchi hazikuhusu. Punguza unafiki.
Hakuna kero ambayo haishughulikiwi na serikali hii,hakuna changamoto inayofumbiwa macho, kila kitu kinapewa uzito wa kipekeee na nguvu ya kutosha, suala la mfumuko wa Bei Tuliona serikali yetu ikitoa Ruzuku ya billion Mia moja kila mwezi katika mafuta na billion Mia moja hamsini katika mbolea,Tuiamini serikali yetu na Tuwe na Subira tutavuka tu salama
 
Tindo Nakuomba umuamini Rais wetu, mama Samia anazungumza kilicho katika moyo wake na kutenda alichokizungumza, Huyu Ni Rais wa vitendo na matendo , lakini pia lazima Tufahamu kuwa Mahitaji ya umeme yanaongezeka kila Siku kutokana na kuimarika kwa uchumi wetu na kuongezeka kwa shughuli za uzalishaji zinazotegemea umeme, ndio maana serikali inafanya kazi ya kuongeza upatikanaji wa umeme kila Siku na katika maeneo tofauti tofauti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…