Rais Samia anafahamu changamoto ya umeme nchini, tuombe mvua zinyeshe. Hata yeye anaumia

Wanaomuunga mkono ni Pwani maeneo ya Chalinze, Mkuranga, Kigoma na wafanyabiashara wakubwa wasio waaminifu ambao ni asilimia 15% ukiwemo wewe na wanufaika wa kulamba asali

Asilimia 85% wana jambo lao wewe endelea kupoteza muda wa kusifia hewa
Rais Mama SAMIA anaungwa mkono na mamillion ya watanzania,Kama sisi wakulima ndio hutwambii kitu kuhusu Rais Samia maana katufuta machozi katika kilimo na kulipa thamani jasho letu wakulima
 

Rudi shule ukajifunze propaganda au kawaambie hizo porojo wale wakulima wa huko bush wasiojua lolote.
 
Hata ulaya walipitia haya tunayopitia leo, na katika mapito hayo walikuwa wanajifunza kwa kila pito watakalo pitia, hata sisi tutavuka na kuvushwa na serikali yetu Hii shupavu ya Mama Samia
Sawa, sasa nenda chini ya mbuyu kaombe samaki wamwagike Msata.
 
Chawa unajitahidi komaaa kijana unaweza kuonekana kwa serikali hii ya mchongo.....ongeza bidii sema jifunze kujenga hoja na kasome sana vitabu ili uwe na content kichwani.
 
Hivi tunaujua ukame? Au tunataka Mungu atupitishie ukame walau wa miezi miwili tuu ili tuweze kuelewana. Tanzania hakuna ukame tusidanganyane, na tusiwe bendera fuata upepo. Vijana tuisaidie hii nchi tuache kusifia ujinga.
 
🤣🤣🤣🤣 Kazi kweli kweli
 
Ukame vipi wakati sababu tuliambiwa mitambo haikwenda service kipindi cha mwendazake
Suala la ukame ndilo.kwa kiasi kikubwa limepelekea kutokea kwa changamoto hii ya umeme, maana mitambo unakumbuka Kuna zile siku kadhaa tulielezwaga na serikali kuwa kutakuwa Kuna kuwa na mgao wa wastani ili kufanyia uboreshaji mitambo yake, lakini kabla hatujaa kaa sawa ndio ukame huu umekuja nao kutupiga,hata hivyo serikali ya mh Rais wetu inaendelea na jitihada za kutatua changamoto hii kwa njia mbadala wa vyanzo vya kuzalisha umeme
 
Mnatuhamasisha kuomba wakati nyie mnachofanya ni kuiba tu, kutotenda haki, na kuwadhurumu wanyonge; huyo Mungu anayesikiliza maombi ya watu kama ninyi ni mungu gani? Mungu wa kuchonga kwa miti au kufinyanga kwa udongo?
TUBUNI kwanza mkaziache dhambi zenu, ndipo maombi yenu yatasikiwa na kujibiwa.
 
Komaa hivyo hivyo mkuu, mtaani kugumu mno
 
Mzee umelipwa shillingi ngapi ? Kutengeneza huu Uzi.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…