Rais Samia anafanya kweli. Mashirika ya Umma kuwa ya Umma kiukweli

Kasi ya maendeleo anayofanya Rais samia kwa miaka hii miwili tuu haijawahi kufanywa na Raisi yeyote wa nchi hii tangu tupate uhuru. Zunguka vijijini ndio utaelewa namaanisha nini.
 
Kasi ya maendeleo anayofanya Rais samia kwa miaka hii miwili tuu haijawahi kufanywa na Raisi yeyote wa nchi hii tangu tupate uhuru. Zunguka vijijini ndio utaelewa namaanisha nini.
hebu tueleze, amefanya kitu gani kipya, ukiondoa vile alivyoanzisha magufuli au alivyovifanya magufuli. kuwa honest tu.
 
hebu tueleze, amefanya kitu gani kipya, ukiondoa vile alivyoanzisha magufuli au alivyovifanya magufuli. kuwa honest tu.
Simple tu, nipo maeneo yanayozalisha ufuta, mwaka huu tumeuza kwa bei ambayo hatujawahi kuifikia hata mwaka mmoja tsh 4100 kwa kilo moja ya ufuta. Pili tupo katika msimu wa mbaazi, tunauza kwa bei ya kihistoria tsh 2100 kwa kilo na tunatarajia itapanda zaidi minada ijayo(kipindi cha jiwe ilishuka thamani mpk tulikuwa tunauza kwa tsh 100, mpk wengine wakakata tamaa ya kulima hili zao). Tatu, kwa trend hii ya bei, tunatarajia makubwa zaidi kwenye korosho. Hapo sjaelezea bei za mahindi, maharage na nafaka zingine.

Mama ameleta maana halisi ya kilimo biashara. Yaani wangoni huwaambii kitu kuhusu mama Dk Samia.

Bado, sijagusia ajira lukuki alizozimwaga, kupandisha madaraja, nyongeza ya kudibua ya mishahara. Miradi ya afya, elimu,barabara,maji, umeme vijijini.
 
Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu
 
Haters hawapendi kusikia habari hizi.
 
Tatizo yanaongozwa kisiasa na makada wanaoteuliwa kiitikadi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…