Rais Samia anahitaji kikao na Kikwete kisha Mbowe

Rais Samia anahitaji kikao na Kikwete kisha Mbowe

Mzee Rufiji

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2024
Posts
261
Reaction score
395
6761d0a183360bc3e29dc0ba687fc2e4

Rais Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete. Picha na Maktaba​




Januari 24, 2024, Chadema walifanya maandamano makubwa Dar es Salaam. Yalikuwa maandamano ya amani, yaliyoandika rekodi Tanzania. Serikali iliridhia, polisi walishirikiana na viongozi wa Chadema, kuratibu usalama.

Maandamano yalifanyika. Polisi walifanya kazi yao. Hakukuwa na uvunjifu wa amani. Chadema walifikisha ujumbe wao, nchi ikabaki salama. Yalikuwa maandamano ya kupinga miswada ya Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, vilevile Sheria ya Vyama vya Siasa 2023.

Ujumbe mwingine wa maandamano ulikuwa kuishinikiza Serikali kusikiliza maoni ya wananchi kuhusu gharama za maisha. Kufanyika kwa maandamano hayo, mshindi wa jumla alikuwa Rais Samia Suluhu Hassan.
Yalifuata maandamano mengine Mwanza, Arusha, Mbeya na Iringa. Hakukuwa na tatizo lolote. Chadema walifanikiwa. Rais Samia alibeba alama zote, kuionesha dunia kwamba Tanzania demokrasia imetamalaki. Kila mpenda demokrasia alipenda jinsi hali ilivyokuwa.

Septemba 23, 2024, ikiwa ni miezi nane kasoro siku moja baadaye, Chadema walipanga kufanya maandamano mengine, yenye ujumbe wa kupinga utekaji na mauaji ya watu. Agosti 8, 2024, mjumbe wa sekretarieti ya Chadema, Ali Mohammed Kibao, alikutwa ameuawa na mwili wake kumwagiwa tindikali.

Septemba 6, 2024, Tegeta, Dar es Salaam, Ali akiwa anasafiri kuelekea Tanga, alishushwa kwenye basi la abiria na watu wenye bunduki, inaodaiwa walijitambulisha kuwa maofisa wa polisi. Walimfunga pingu na kuondoka naye. Siku mbili baadaye, mwili wa Ali ulikutwa Ununio akiwa tayari ameshauawa.

Mbali na kifo hicho, Chadema wana malalamiko ya kuchukuliwa kwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema (Bavicha), Wilaya ya Temeke, Deusdedith Soka na wenzake wawili, Jacob Mlay na Frank Mbise. Hadi sasa hawajulikani walipo. Na si kitambo kirefu, mwanaharakati Edgar Mwakabela “Sativa”, alikutwa ametelekezwa msituni Katavi, akiwa ameumizwa kwa kiasi kikubwa.

Huo ni mfano wa masuala ambayo Chadema walipanga kuandamana ili kushinikiza uchunguzi. Tofauti na ilivyokuwa Januari 2024, maandamano ya Septemba 24, polisi waliyapinga, kisha walitumia nguvu kubwa kuyadhibiti. Katika hekaheka za kudhibiti waandamanaji, polisi walikamata hadi wasio na hatia, wakiwemo waandishi wa habari

Kwa udhibiti wa maandamo ya Septemba 23, Chadema wameshinda, maana ujumbe wao umefika mbali zaidi. Nguvu kubwa iliyotumiwa na polisi, inajenga maswali mengi. Majibu yake kwa sehemu kubwa yanafafanua kiini cha maandamano. Na hayo ndiyo mafanikio ya Chadema. Ujumbe umefika. Januari ilikuwa chanya kwa Rais Samia, kwamba ni kiongozi mwanademokrasia na anayejiamini. Septemba, imekuwa hasi kwa Rais Samia, kidemokrasia. Zaidi, swali linakuwa ni kwa nini wanaotaka kufikisha ujumbe wa mauaji na utekaji wazuiwe? Nini kinafichwa?

Ras Samia anahitaji ushauri
Rais wa nne wa Tanzania, Jakaya Kikwete katika mkutano wa Jukwaa la Uongozi Afrika (ALF), uliofanyika Septemba 2017, Boksburg, Johannesburg, Afrika Kusini, aliikuna na kuipatia vilivyo jumuiya ya wapenda demokrasia.

Kikwete, aliipa furaha zaidi jumuiya ya vyama vya upinzani barani Afrika, kutokana na mada aliyotoa, aliposema kuwa watawala hawapaswi kuwaona wapinzani wao kuwa ni maadui, badala yake wawachukulie ni washirika katika ujenzi wa utawala bora.

Kikwete alisema kuwa vyama tawala na vya upinzani si maadui. bali ni washindani. Kwamba uwepo wa wapinzani ni kuwasahihisha watawala pale wanapofanya makosa na kuwazindua wanapolala. Alichokizungumza kingine ni kuwa watu wa chama tawala wanaweza kutoona au kukosa ujasiri wa kuyasema makosa ya kiongozi wao aliye madarakani, hivyo wakawa wanaunga mkono makosa.

Mantiki hapo ni kuwa watawala badala ya kuwafurahia wanaowaunga mkono kwa kila jambo, wanapaswa kujitenga nao, maana huwapotosha kwa kuwavimbisha kichwa hata wanapovuruga.

Ni kwamba watawala badala ya kuwachukia na kuwanunia wapinzani wao, wanapaswa kuwategea sikio, maana ndio ambao wanawawezesha kuyajua makosa na namna ya kurekebisha.

Ujumbe wa Kikwete ni mwema kwa kila kiongozi Afrika, maana wengi huwachukulia wapinzani wao kuwa ni wapiga kelele, walalamikaji na wasioona jema lolote la Serikali. Kwa msingi huo, huamua kuziba masikio na kutotaka kusikia chochote kutoka kwa viongozi wa vyama pinzani.

Ni kupitia kauli hiyo ya Kikwete, ukijumlisha na mtindo wake wa uongozi wa miaka 10 akiwa Rais wa Tanzania, ndicho kishawishi kwamba Rais Samia anahitaji kuketi naye, watete, namna bora ya kuishi na wapinzani wa kisiasa, bila chuki. Kikwete, katika uongozi wake, alikuwa na utaratibu wa kuketi na wapinzani kila hali ya hewa ilipochafuka. Mikutano hiyo ilisaidia kusawazisha mambo na nchi kusonga kwa utulivu. Ni utaratibu mzuri kufuatwa na kila rais aliye madarakani.

Rais Samia anapaswa kufahamu kuwa nyakati za misuguano ya kisiasa, baina chama chake (CCM), dhidi ya vile vya upinzani, au wapinzani na vyombo vya dola, kuna uongo mwingi hutengenezwa. Yeye kama Mkuu wa Nchi, vilevile ndiye mlezi wa taifa, hivyo anapaswa kusikiliza makundi yote kwa ukaribu.

Rais Samia anahitaji kikao na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, pamoja na viongozi wengine wa upinzani. Awasikilize ili ajue wapi pa kushika. Ni makosa kusikiliza hoja za upande mmoja.

Kama Rais Samia aliweza kukubali kuwa mgeni rasmi kwenye kongamano la Siku ya Wanawake Duniani, lililoandaliwa na Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), haishindikani hata kidogo kufanya mikutano ya maridhiano na wapinzani.

Rais Samia kukutana na wapinzani haitakuwa kujishusha, bali itamjengea zaidi heshima. Hata sasa, jinsi kulivyo na malumbano ya kisiasa, vilevile misuguano ya vyama vya upinzani na dola, kuna maswali yanaulizwa bila majibu; mbona Rais Samia alikuwa anakwenda vema na wapinzani, nini kimembadilisha? Mbona aliwapatia wapinzani lakini sasa anasumbuana nao?

©Luqman Maloto
 
Mnataka maridhiano mengine baada ya kuchakazwa?
Chadema kumejaa wapumbavu
 
Yaani watu wafanye maandamano yenye anuani "Samia must go" halafu waachwe? Kamwe haitawezekana. Chadema ni chama cha hovyo tu. Kina watu wenye vichwa vibovu ambao hawapaswi kuwa treated friendly.
 
Back
Top Bottom