Hiki hapa ni kipande kifupi cha video kutoka kwenye filamu ya Royal tour ambapo Samia anaulizwa kama Magufuli aliambukizwa Corona na yeye kujibu ndiyo.
Anakiri hilo kwenye sekunde ya 18.
NANUKUU:
Peter: In all honest your predecessor (Magufuli) was not a big friend of Vaccines and of the Science.
Samia: No he's a scientist.
Peter: Even worst!
Samia: He is a chemist… he was a chemist.
Peter: He was a chemist?
Samia: Yes
Peter: Who contracted COVID?
Samia:
YEAH!
View attachment 2203911
Nilifungua bandiko kuhusu tuhuma hiyo haionekani. Hii hapa kutoka kwa mchambuzi mmoja
MADAI YA SINEMA YA ROYAL TOUR NI KASHFA KUBWA! TUME HURU ICHUNGUZE UKWELI!
1) Niliposikia kwa mara ya kwanza kwamba hii Sinema ya Royal Tour (ambayo Rais wetu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ni Main Actor and Tour Guide) ina maneno haya kuhusu Kifo cha Rais John Pombe Magufuli nilistuka na sikuamini!
2) Kwa MAONI yangu hii inam-compromise sana Rais Samia ambaye ndiye aliyetutangazia Kifo cha Rais Magufuli na kutufahamisha kwamba kilichomuua Rais Magufuli ni Ugonjwa wa Moyo! Sasa haya ya COVID-19 yanatoka wapi tena?!
3) Najiuliza!
a) Hivi Rais Samia alikubalije kushiriki Sinema inayopotosha Taarifa ya Serikali kuhusu Jambo zito kama hili?!
b) Kwa nini hakudai hicho kipande kiondolewe?!!
4) Ntashangaa sana akitokea "Mtetea Chochote" akasema nae Rais Samia hakuiona na kujiridhisha na Script (if it is all acceptable) kabla ya Uzinduzi wa Movie huko Marekani! It would constitute a serious blunder. An act of gross incompetence on the part of Presidential Advisers (maana "Rais hakosei").
5) Kwa MAONI yangu, huyu anayeongea kwenye hii script ni "Spin Master", Utetezi wake umekaa kipuuzi na hauna mashiko. Ashakum si matusi.
6) Iwapo anachosema "Spin Master" ndiyo Hoja na Majibu ya Serikali (kwamba kilichosemwa kuhusu sababu ya Kifo cha Magufuli kuwa ni COVID-19 ni kauli ya Wanaharakati (ambao wanatajwa kwa Majina)), mimi BJC naomba kuuliza ifuatavyo:
Mbona sasa hawakusema (kwenye hiyo Sinema ya Royal Tour) kwamba "kuna na Watanzania wengi wengine (na hata Watu wa Nje) ambao wanaamini Rais Magufuli kauawa"?!
7) Ushahidi!
a) Rais Samia aliwahi kuwakemea kwa hasira wanaodai Rais Magufuli kauawa.
b) Rais Samia akasema wenye Ushahidi kwamba Rais Magufuli kauawa wampelekee.
8) Ushauri wa Bure!
a) Baada ya Sinema ya Royal Tour kulikoroga big time, ni wazi kwamba kumbe kweli
kuna umuhimu wa kuunda Tume Huru ya Kuchunguza Kifo cha Rais John Pombe Magufuli. Wadanganyika tunataka kujua kwa uhakika: Je, Rais Magufuli alikufa kwa Ugonjwa wa Moyo (ambao haukusababishwa na mkono wa Mtu), alikufa kwa COVID-19 au aliuwawa?! Na alikufa lini exactly?!
b) Naamini Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ataona umuhimu huu. Asipuuze hili, hasa ikizingatiwa kwamba yeye ndiye Main Actor and Main Guide in this movie that has come up with this act of not only gross disrespect for our late President but also explosive provocation directed towards our Nation and all Tanzanians!
c) Namshauri Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan awe mwangalifu sana kutambua kwamba Kifo cha Magufuli kimeligawanya Taifa... na hivyo afanye kazi ya ziada kutuunganisha badala ya kutugawa na kuruhusu Watu (na hasa) Viongozi kutonyesha vidonda kila kukicha!
9) Kauli Tata zimeshamiri Nchini na zinaleta taharuki kila kukicha!
10) Mfano wa Kauli Tata!
a) "...ile ilikuwa Nidhamu ya woga tu!"
b) "Nchi imeharibiwa sana hii!"
c) "Sasa tunairudisha Tanzania Duniani!"
d) N.k.
11) Kwa bahati mbaya sana, kauli zinazotolewa kila kukicha kumkandia na kumharibia jina Rais Magufuli zinachochea wasiwasi wa baadhi ya Watanzania! Kama nilivyosema, zinaleta taharuki. Baadhi ya Wadanganyika tunajiuliza:
a) Kwa nini wenzie waliomo Serikalini ndio wanaongoza Mashambulizi?!
b) Kwa nini Serikali ya Awamu ya 6 inaonekana ku-enjoy kuitupia Madongo Serikali ya Awamu ya 5?! Serikali ya Magufuli! Strangely, by more than 90% Serikali ya Awamu ya 6 ndiyo Serikali ya Awamu ya 5!! Rais wa sasa ndiye alikuwa Makamu wa Rais Magufuli (na Mshauri wake Mkuu), Makamu wa Rais wa sasa ndiye alikuwa Waziri wa Fedha, Waziri Mkuu yuleyule, Mkuu wa Usalama wa Taifa yuleyule, IGP yuleyule, CDF yuleyule, Jaji Mkuu yuleyule, n.k., n.k.
c) Kwa nini baadhi ya Viongozi wa Serikali ya Awamu ya 6 wanatoa matamshi ambayo yanaashiria kwamba kumbe (labda) walikuwa na Chuki kubwa kwa Rais, Mwenyekiti na Amiri Jeshi Mkuu wao, Rais Magufuli?!
d) Inakuwaje wale wote waliotofautiana na Rais Magufuli wamepandishwa vyeo na Kauli zao na Matendo yao yanaonyesha hawajutii walichofanya?! Ni kama vile wanatamba kwa "Ushujaa" wao wa Kupambana na Rais Magufuli?! Wote tunazikumbuka zile audio clips...!!
e) Kwa nini baadhi ya Viongozi wa "Matawi ya Juu" Nchini wako bize kumbomoa Magufuli and his Legacy! Hivi hii well-coordinated attempt at "Character Assassination" ina Lengo gani na Faida gani?! Imesababishwa na nini?!
f) Kwa nini Serikali na Chama hamumtetei Magufuli?! Saa zote ni Kimya au Mashambulizi tu! Why?!
g) Hivi mmesahau kwamba mwenzenu amepumzika na hana tena Uwezo wa Kujitetea?!
h) Hivi mmesahau kwamba Rais Magufuli ameacha Mke na Watoto ambao mnawaumiza sana kwa Mashambulizi yenu na/au Kimya chetu?! Kwa nini msiwaache walau wakauke machozi?! Hivi mnasahau kwamba wao ni Bin Adam na wanawashangaa sana, to say the least?!
12) Hivi ni sawa kweli kwamba Serikali, Chama Tawala, Wabunge, Mawaziri, Taasisi mbalimbali, Jumuia mbalimbali (mfano: UV-CCM, UWT, Wastaafu, n.k.)... wote mko kimya kabisa kila Hayati Magufuli anavyotukanwa na kudharirishwa?! Eti hata Viongozi wa Dini nao mko kimya! Mbona haiingii akilini?!
Unafiki huu, mmhuuu...! Au labda ni ukondoo tu...?! Au ni Guilty Consciousness...?!
13) Sasa kama Magufuli alikuwa Rais mbaya
kiasi hicho (which I don't believe anyway), inawezekanaje nyinyi Washirika wake wote muwe wasafi kiasi hicho cha kuthubutu kumtupia mawe mazito hivyo Mwenzenu?!
a) Collective Responsibility iko wapi?!
b) Hivi nyie wengine mnaponaje?!
c) Hivi mnajua kwamba kwenye Sheria za Kimataifa iliwekwa precedent kwenye Nuremberg Trials (baada ya Vita Kuu ya Dunia)?! Kesi za Washirika wa Hitler...! Kwa kifupi, Mahakama ya Kimataifa iliamua kwamba
Rais/Kiongozi Mkuu hawezi kuwa Shetani na Mawaziri/Wasaidizi wake wote wakawa Malaika...!! Never!
d) Mbona mnatufanya Wadanganyika Mafala?!
e) Mbona mnajichanganya hivyo?!
14) Narudia!
a) Wasiwasi na Hasira za Wadanganyika vinasababishwa na mengi.
b) Mungu anayajua Maovu yetu yote (sisi wote) na Hukumu zake!
c) Tusicheze na moto!
15) MUNGU IBARIKI TANZANIA!
BJC. DSM. 26.04.2022. 1924hrs.