Rais Samia anakubali kuwa Rais Magufuli aliambukizwa UVIKO-19?

Rais Samia anakubali kuwa Rais Magufuli aliambukizwa UVIKO-19?

Duh!
" President John Magufuli who denied COVID-19 existed"

huu mstari mmoja umetumiwa na vianzo vikubwa vya habari duniani.

Binafsi sijaona lini au wapi amesema ' hakuna COVID-19'. Kwa uelewa wangu COVID-19 ni kirusi.
Niliyowahi kusikia, ni pale aliposema "...kinaweza kufa na joto..." Najiuliza, imekuwaje waandishi wa habari hawakuona au kusikia hayo?

Kwanini walitumia maneno hayo wakijuwa kwamba siyo kweli alikataa uwepo wa Kirusi?

Huyo muuliza maswali aidha kwa makusudi au la, Je aliamini yaliyoenea mitandaoni na baadae kwenye vyombo vikubwa vya habari ni ya kweli?

Sina majibu, ila ninachojua na alichokataa ni uwepo wa "Pandemic" na sio uwepo wa kirusi. Nina uhakika hatukuwa na vigezo vya kutamka kuwa Tanzania tuna Pandemic.

....mategemeo yangu yalikuwa Mh Raisi angeweza kutatua kinzani hiyo lakini nilichopata ni "yeah"
I am disappointed.
 
Mimi sijaona shida yeyote hapo. Rais hajasema wala muuliza swalinhajauliza kuwa Mzee alikufa kwa Covid bali 'kupatwa' (contract). Ilw pia kila mtu apaswa kujua kuwa, kuww chemist haikufanyi wewe kutopata maambukizi. Na ndio maana madaktari wakubwa nao huambukizwa. Kwa hiyo huyo jamaa aliuliza kwa namna ya kushangaa sio kwa namna ya kuhitaji jibu toka kwa Mh. Rais. Ndio maana Mama alijibu tu simply yeah..ili aendelee kama kuna jambo zaidi. Contextually huwezi kuchukulia kuwa that was a confirmation. Kutingisha kichwa au matumizi ya maneno yeah au okay okay..ktk oral communication hayamaanishi muda wote kuwa unakubali anachosema 100 100 bali nibkuonesha tu sapoti ktk mazungumzo.
 
Hapo sioni tatizo,maana kama ni kweli yeye hakuwa kiongozi wa Kwanza kuambukizwa covid.wapo viongozi wengi akiwemo waziri mkuu wa uingereza
 
Hiki hapa ni kipande kifupi cha video kutoka kwenye filamu ya Royal tour ambapo Samia anaulizwa kama Magufuli aliambukizwa Corona na yeye kujibu ndiyo.

Anakiri hilo kwenye sekunde ya 18.

NANUKUU:

Peter: In all honest your predecessor (Magufuli) was not a big friend of Vaccines and of the Science.

Samia: No he's a scientist.

Peter: Even worst!

Samia: He is a chemist… he was a chemist.

Peter: He was a chemist?

Samia: Yes

Peter: Who contracted COVID?

Samia: YEAH!

View attachment 2203911
Ukiangalia sura ya Raisi anaonekana ana wasi wasi hatari,ubongo na mdomo havipo kwenye sincronization,kapigwa swali,kapewa comment kabla ya ubongo hauja dadavua na kuchakata,mdomo ukasema ndio,imeisha hiyo!!!!,"he was chemist who contracted COVID"?
Hapa angekuwa ana komand nzuri ya kizungu Ili bidi afunguke amwage point kadhaa na bla blaa nyingi!!lakini wapi!
Akaingia mkenge,hakutegemea kusema ndio,basi lilimponyoka tu,
Kwa watu ambao hawajuhi jinsi Raisi anatakiwa awe na ajibu,waangalie wakati Mkapa anahojiwa na Jeff koinage kule Kenya,waone comand ya kizungu ilivyo muhimu
 
Sijasema popote ukweli ufichwe, nimesema Rais afundishwe jinsi ya kuongea, asije kukoseakosea kwenye mambo mengi mengine tu kwa kimbelembele cha kujibu harakaharaka.

Jua kusoma kwa ufahamu.
Wewe ni mpumbavu unayetaka kila mtu awaze na afikirie kila unachoandika wewe ni sahihi

Umekosa maarifa na ufahamu wa mambo, Unachokifahamu wewe tambua Wengine walianza kukitambua kabla yako na kuweka kwenye maandishi

Rais ni mamlaka, Na kwa Tanzania lazima ufahamu umpende au Usipende Rais ndie Sheria, Kanuni na taratibu

Kwa mfumo wa Tanzania wa sasa hakuna mwenye nguvu ya kumsema na kumkosoa Rais hiyo ndio Tanzania

Sheria ya kumuweka mtu Kizuizini bado Rais anayo na haijafutwa Tanzania, Anaweza kukupeleka jela daima

Sasa wewe unataka wasaidizi wake wamwambie Rais Jamaa hakupata corona wakati Yeye alikuwepo kama Makamu wake wa Rais

Hakuna Rais alipokosea kuwa Jamaa alipata korona

Thibitisha hapa kwa vyeti kuwa hakuwa na korona

Je wewe una akili?
 
Haya mambo mengine Rais inabidi akae na wataalam wamfundishe kwamba maswali mengine inabidi kuchukua sekunde kadhaa kwanza kufikiri kabla ya kujibu.
Ubongo huo anao? Kwa ufupi motheri ni slow learner anayetaka kutuaminisha kwamba naye ni genius!
 
Hiki hapa ni kipande kifupi cha video kutoka kwenye filamu ya Royal tour ambapo Samia anaulizwa kama Magufuli aliambukizwa Corona na yeye kujibu ndiyo.

Anakiri hilo kwenye sekunde ya 18.

NANUKUU:

Peter: In all honest your predecessor (Magufuli) was not a big friend of Vaccines and of the Science.

Samia: No he's a scientist.

Peter: Even worst!

Samia: He is a chemist… he was a chemist.

Peter: He was a chemist?

Samia: Yes

Peter: Who contracted COVID?

Samia: YEAH!

View attachment 2203911
Sisi tunaojua ukweli kuwa mlimuua sasa mmekuwa mnaangaika kuficha ukweli ila sasa mnaanza kuweweseka kwa kauli mbili mbili ukweli utajulikana tu.kuhusu kovidi kila mtz aliugua hata sa100 na kikwete waliugua na kuugua covid ndiyo kinga yenyewe tuliyo opata watz. KUUGUA COVID SIYO KUFA KWA COVID JPM ALIKUWA MGONJWA HATA KABLA YA KUWA RAIS ILA SISI TUNAJUA ALIMALIZIWA KITANDANI ILI KUSINGIZIA UGONJWA
 
... mdogo mdogo MATAGA & Co; wataelewa tu. Ubishi mwingi akili punje ya haradali. Kauli rasmi kutoka kwa Rais na Amri Jeshi Mkuu vyombo vya ulinzi na usalama ambaye taarifa zote za taifa hili ziko mikononi mwake! Nani anapinga kauli ya Amiri Jeshi Mkuu?
Lisu alisema wakamuwakia sasa wabishie amri majeshi mkuu tuone
 
..kwa sasa hivi Serikali inatakiwa IKANUSHE hiki tulichosikia ktk Filamu.

..Dr.Abbas, Gerson Msigwa, Zuhura Yunus, hawakutimiza wajibu wao ktk hili.

..haijalishi kama Jpm alikufa kwa covid au la, video ya namna hii haikutakiwa ionekane na hilo ni jukumu la hao watatu hapo juu.
Kabisa kabisa, kwakua Mh. Rais ataambiwa alilidanganya taifa. Hawa wasaidizi buana sijui kwanini wana mpotosha Rais hivi!
 
..kilitakiwa kihakikiwe ile kisitoke public, na huo ni wajibu wa Dr.Abbas, Msigwa, na Zuhura Yunus.

..suala la Jpm kuambukizwa Covid lilitakiwa libakie kuwa SIRI ya wakubwa huko serikalini.
Mbona juzi hapa tumeambiwa makomo wa Rais wa USA kaambukizwa? Hakuna siri ktk hili. Swala la kafa na nini hiki ni kingine na ishasemwa alikuwa na issue ya umeme wa moyo JPM.
 
Ukweli ni kwamba tunaosikiliza mazungumzo ya rais huyu, utagundua jinsi alivyo hysterical anapokuwa na wazungu. Hapo huyo mzungu ndo anasema ... contracted COVID.. Yeye anaishia kusema YES hata kabla ya sentensi haijafika mwisho. Ni papala za furaha ya kuzungumza na mzungu. Kumbuka anapohojiwa na waafrika anakuwa mwamba mkorofi bila sababu; Ref. mahojiano yake na Kikeke wa BBC.
You nailed...tuna kihelehele sana kwa wazungu...! Na wao wanajua tu wajinga..wanatusanifu sana.
 
Rais ni mamlaka, Na kwa Tanzania lazima ufahamu umpende au Usipende Rais ndie Sheria, Kanuni na taratibu

Kwa mfumo wa Tanzania wa sasa hakuna mwenye nguvu ya kumsema na kumkosoa Rais hiyo ndio Tanzania
Duuuh! Unahorojoka mwenyewe kama katapila linalovuja oil.

Huna hata wasiwasi masikini!
 
Ni wazi tu phase ya kwanza mwaka 2020 alikimbia kijijini kwao.

Ya pili alijitahidi akabidi arudi mjini.

Tukatae au tukubali negligence yake kuhusu huu ugonjwa ilicost watu sana .

Yeye anawambia watu wachape kazi huku yeye akakimbilia kijinini mwezi March hadi May 2020

Huko waliko jifungia kulitokea nini
 
Back
Top Bottom