Rais Samia anakuza utalii wetu kupitia 'The Royal Tour’

Chee4

Member
Joined
May 17, 2021
Posts
35
Reaction score
125
Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameanza kurekodi kipindi maarufu cha 'The Royal Tour' kwa lengo la kuitangaza Tanzania kwenye Sekta ya Utalii, Biashara na Uwekezaji.

Faida ya Mhe. Rais kurekodi Kipindi cha 'The Royal Tour'

● Kipindi kitarushwa kwenye Mabara na Nchi Kubwa kama Marekani, Ulaya, Asia na Afrika hivyo Tanzania itapata Watalii wengi kutoka maeneo hayo.

● Taasisi nyingi za Masuala ya Utalii na Uwekezaji za Kimataifa zenye wafuasi wengi watapata kuijua vizuri Tanzania na dira ya kiongozi Mkuu wa Nchi kwenye masuala ya biashara na uwekezaji.

● Itatambulisha Utamaduni na Mila za Makabila yaliyopo Tanzania.

● Kipindi hicho kitakua kikirushwa kwenye Ndege za Kimataifa ambazo husafirisha abiria Duniani kote.

● Viongozi mbalimbali walishawahi kurekodi kipindi cha 'The Royal Tour' akiwemo Rais Paul Kagame, Waziri Mkuu wa New Zealand Hellen Clark, Rais wa Mexico Felipe Calderon na Rais Samia ni sehemu ya viongozi hao.

Hakika Tanzania Yetu sasa Inaenda Kimataifa kwa Maono haya aliyonayo Mhe. Rais sasa tutafikia lengo la kupata Watalii Milioni 5 kwa mwaka.

#TanzaniaSalamaNaSamia
 
Hata hili la kesi ya Ugaidi wa Mbowe na kuzuia sehemu Haki kikatiba demokrasia limemtangaza Mama Kama kiongozi imara mfuasi wa Mwendazake. Kama taifa tuache ujinga na unafiki.
 
Kitakachoitangaza Tanzania pamoja na vivutio vyake vya utalii ni demokrasia,uhuru wa watu pamoja na utawala bora.

Nchi ambayo Serekali imeitangazia dunia kuwa ina gaidi hatari sana(yaani Freeman Mbowe)itawezaje kuvutia wawekezaji pamoja na watalii?

Tuweke taasisi na mifumo yetu sawa kwanza ndipo Dunia itatuamini.

Umeelewa Bwana mleta uzi?
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassani yupo ziarani Zanzibar ( Pemba) ikiwa ni muendelezo wa ushiriki wake kurekodi kipindi cha Royal Tour

Amepokelewa na Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Mwinyi
 
Kichwa cha habari hakikupaswa kuwa TAARIFA MUHIMU, umuhimu wa hii taarifa ni upi? Muhimu kwa nani?
 
Kitakachoitangaza Tanzania pamoja na vivutio vyake vya utalii ni demokrasia,uhuru wa watu pamoja na utawala bora.

Nchi ambayo Serekali imeitangazia dunia kuwa ina gaidi hatari sana(yaani Freeman Mbowe)itawezaje kuvutia wawekezaji pamoja na watalii?

Tuweke taasisi na mifumo yetu sawa kwanza ndipo Dunia itatuamini.

Umeelewa Bwana mleta uzi?

Mbowe ni Gaidi Gaidiiiiiiiiiii
 
Sisi tunangaza kuwa Mwenyekiti wa chama cabupinzani ni gaidi, labda watakuja watalii kutoka Kabul na Syria.
 
Mbowe ni Gaidi Gaidiiiiiiiiiii
Gaidi lilitokea CCM😁😁😁
kGayQ.jpg
An8VB.jpg
AQNUPo.jpg
2904506_IMG_0151.jpg
M2myW.jpg
 
Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameanza kurekodi kipindi maarufu cha 'The Royal Tour' kwa lengo la kuitangaza Tanzania kwenye Sekta ya Utalii, Biashara na Uwekezaji.

Faida ya Mhe. Rais kurekodi Kipindi cha 'The Royal Tour'

●Kipindi kitarushwa kwenye Mabara na Nchi Kubwa kama Marekani, Ulaya, Asia na Afrika hivyo Tanzania itapata Watalii wengi kutoka maeneo hayo.

● Taasisi nyingi za Masuala ya Utalii na Uwekezaji za Kimataifa zenye wafuasi wengi watapata kuijua vizuri Tanzania na dira ya kiongozi Mkuu wa Nchi kwenye masuala ya biashara na uwekezaji.

● Itatambulisha Utamaduni na Mila za Makabila yaliyopo Tanzania.

● Kipindi hicho kitakua kikirushwa kwenye Ndege za Kimataifa ambazo husafirisha abiria Duniani kote.

● Viongozi mbalimbali walishawahi kurekodi kipindi cha 'The Royal Tour' akiwemo Rais Paul Kagame, Waziri Mkuu wa New Zealand Hellen Clark, Rais wa Mexico Felipe Calderon na Rais Samia ni sehemu ya viongozi hao.

Hakika Tanzania Yetu sasa Inaenda Kimataifa kwa Maono haya aliyonayo Mhe. Rais sasa tutafikia lengo la kupata Watalii Milioni 5 kwa mwaka.

#TanzaniaSalamaNaSamia
Mpaka hapo tayari ameshakosea kwa kujiinua; hivi utalii unahusu matajiri, watu maarufu na viongozi pekee ambao wanauwezo kulipia?

'The Royal Tour' maana yake isiyorasmi ni ziara ya kifalme au kimalkia....aibu sana

Huwezi kuutangaza utalii wa Tanzania ikiwemo utamaduni, mila na desturi zake kwa jukwaa la kifalme au kimalkia ambapo wataofuatilia zaidi ni wenye hadhi yako tu wengine watakaa pembeni

"Why can't we brand ourselves in the manner that really impresses who we are naturally blessed?
 
Pk alifanya kitu kama hiki akishirikiana na actor Morgan freeman watu walisifia sana...
Huku wakiponda wizara utali bongo,
Mama anafanya sahv wabongo wanaponda

Siku zote nasema wabongo mpaka leo
Hatujuwi tunataka nini??

Ova
 
Kweli kabisa tunatendewa wema lakini siku zote hatuna shukrani, cjui nini tufanyiwe sisi watanzania turidhike
 
Back
Top Bottom