Rais Samia anakuza utalii wetu kupitia 'The Royal Tour’

RAIS SAMIA ANAKUZA UTALII WETU KUPITIA 'THE ROYAL TOUR'


Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameanza kurekodi kipindi maarufu cha 'The Royal Tour' kwa lengo la kuitangaza Tanzania kwenye Sekta ya Utalii, Biashara na Uwekezaji.


Faida ya Mhe. Rais kurekodi Kipindi cha 'The Royal Tour'

●Kipindi kitarushwa kwenye Mabara na Nchi Kubwa kama Marekani, Ulaya, Asia na Afrika hivyo Tanzania itapata Watalii wengi kutoka maeneo hayo.

● Taasisi nyingi za Masuala ya Utalii na Uwekezaji za Kimataifa zenye wafuasi wengi watapata kuijua vizuri Tanzania na dira ya kiongozi Mkuu wa Nchi kwenye masuala ya biashara na uwekezaji.

● Itatambulisha Utamaduni na Mila za Makabila yaliyopo Tanzania.

● Kipindi hicho kitakua kikirushwa kwenye Ndege za Kimataifa ambazo husafirisha abiria Duniani kote.

● Viongozi mbalimbali walishawahi kurekodi kipindi cha 'The Royal Tour' akiwemo Rais Paul Kagame, Waziri Mkuu wa New Zealand Hellen Clark, Rais wa Mexico Felipe Calderon na Rais Samia ni sehemu ya viongozi hao.

Hakika Tanzania Yetu sasa Inaenda Kimataifa kwa Maono haya aliyonayo Mhe. Rais sasa tutafikia lengo la kupata Watalii Milioni 5 kwa mwaka.

#TanzaniaSalamaNaSamia



 
Btw hivi na ile 'Tanzania Safari Channel' imefikia wapi.... wakati mwingine drama za matumizi mengine yasiyo na tija bongo, huwa haziishi na inabidi kuwa wapole tu....
 
Btw hivi na ile 'Tanzania Safari Channel' imefikia wapi.... wakati mwingine drama za matumizi mengine yasiyo na tija bongo, huwa haziishi na inabidi kuwa wapole tu....
Channel ipo ila kuna mtua anataka kutengeneza 'legacy' yake kama alivyokuwa anafanya Nyalandu ambapo hata pamoja na jitihada hizo zene thamani hakluna mapato yoyote yaliyopatikana kwa nchi.
 
Ningekuwa mimi ni mshauri, wala nisingemshauri afanye mambo haya. Hizo pesa angepeleka kujenga chuo cha kimataifa cha teknolojia.

Kuna mengi ya kufanya ya taasisi ya urais, hayo angebariki tu, wengine huko waendelee kufanya.

Lakini yawezekana anatuzuga. Kiti kimekuwa cha moto, kaamua kwenda kula bata kwanza.
 
Naunga mkono hoja
Nimetoa mchango wangu wa mabandiko mawili kuhusu uzinduzi wa filamu ya Royal Tour.
Bandiko la kwanza ni hili

Na bandiko la pili ni hili

Nautakia uzinduzi mwema wa Royal Tour siku ya Jumatatu ya Pasaka.
Paskali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…