Kwa taarifa yako watumishi wote wa umma wanalipa kodi isipokuwa Rais pekee. Na hili ni takwa la Katiba yetu.
Kodi zipo za aina nyingi ikiwemo kundi la direct na indirect taxes. Direct tax ni Income tax inayolipwa kwa mfumo wa PAYE, yaani Pay As You Earn, Hii ni % ya mshahara wako. Hivyo, mwajiriwa yeyote Katika sekta yeyote iwe ya umma au binafsi wanalipa hii kodi.
Kodi zinazoitwa indirect taxes zinatozwa kwenye bidhaa. Hivyo kila unaponunua bidhaa unalipa kodi hii uwe ni mtumishi au siyo mtumishi wa umma. Katika kundI hili kuna excise duties, nk ambazo zinatozwa advalorem au vinginevyo. Isitoshe, kuna mfumo wa VAT ambao nao una maelezo yake. Itoshe tu kwa leo kukufumbua hayo. Elimika.