Rais Samia anaongelea matiti, tena ya Wanawake wenzake?

Rais Samia anaongelea matiti, tena ya Wanawake wenzake?

Ana point isipokuwa kaiwakilisha katika muktadha usio sahihi...

Ukitaka kuchukua nia ya matamshi yake na kuachana na mengineyo, utamuelewa...

Ingawaje ni suala la yeye kujifunza namna ya kuchagua maneno ya kuongea mbele ya umma haswa linapokuja suala la maumbile n.k...
 
Juzi nilimlalamikia Ayo kuwa anaweza kuwa amemnukuu vibaya nikaomba nipewe video. Leo Mkuu Ngabu mmeniwekea. Nimeamini alisema. Mama kweli amefungulia nchi. Maelezo yake yanazungumza mengi! Mungu atatulinda .
 
Rais anaongelea matiti tena ya wanawake wenzake?

This is beyond shameful, beyond embarrassing, and downright beyond the pale. Cringeworthy.

I’m at a loss for words!!
View attachment 1905556

hapana kaka rudi kaangalie tena clip vizuri inaonekana ulikuwa una foward bila umakini wowote, alikuwa anajaribu kuwakingia kifua ili mbeleni wawe na maisha bora
 
Yaan hapo ni udhalilishaji wa hali ya juu,

Kila mtu huchagua kile kimfaacho, kumsema binti mwanamichezo ati ana flatchest na amekakamaa kama mwanaume hatoweza kuolewa ni dhahiri shahiri hapendi wanawake wawe wana michezo lakini pia wajihisi wao ni wabaya na hawapendezi machoni mwa watu, (Psychological Torture)

Mama hapo amekosea sana, hakupaswa atoe comment ya namna hiyo kwa wanawake wenzie, Ndoa ni sharia lakini sio lazima kwa baadhi ya wengine.
 
Sio siri she overspoke.

Michezo wameipenda wenyewe waachwe hata kama wakifanana na Caster Semenya.

Ht km mfuko wa michezo ufanyeje hawana uwezo wa kuwatafutia ndoa.
wanawake wazuri wangapi hawana ndoa?
Ndoa ni zaidi ya mwili....ndoa ni majaliwa ndoa ni suala binafsi
 
You're using a lot of meaningless words in a disjointed pattern.

To you and to the one you admire, shaming specific individuals in public is what represents "standing the truth"? whatever that means!
Samia alikosea Sana kutaja sababu kwamba mamlaka ziwasaidie kwa sababu hawavutii kwa wanaume na wako flat hata ukiwaweka na wanaume huwezi tofautisha!

Ila angeomba mamlaka ziwatunze kwa sababu wameleta sifa taifa angekuwa sahihi.

Nadhani Ni malezi ya kidini ndo yamefanya atoe comment ya kijinga bila kufikiria yeye Ni rais.
 
Hahaha. Mama anashangaza alikuwa anaongea vile kwa faida ya nani? Hajui kama amewatesa kisaikolojia wale wanawake?
Mheshimiwa rais Samia Suluhu Hassan, Kwa unyenyekevu na kwa heshima kubwa naomba niseme yafuatayo, nikiamini sikuvunjia heshima rais wangu.

Mhe. rais Samia, maneno uliyoyasema ni mazito na ya kumshushia hadhi mwanamke, kwanza huku bara tunajali utu na hatujawahi kukubali wanawake wetu, ambao ni mama zetu, dada zetu, wake zetu na watoto wetu wawe ni chombo cha kutumiwa na wanaume kujifurahisha.....Hiyo mheshimiwa ni BIG NO! Siyo utamaduni wetu, sijui labda huko visiwani, wanawake kwetu si lazima waolewe ndiyo maana utakuta wanawake wengi huku bara wanajitegemea wenyewe kiakili na kiuchumi.

Hakuna yale mambo ya ujinga ujinga ya Taliban, yaani mke au dada au mama akienda sokoni au marikiti lazima afuatane na "male figure" hatuna ulazima huo. Kwa sisi wakristo ndoa ni muunganiko mtakatifu wa watu wawili, siyo mmoja awe mtumwa wa mwenziwe na siyo utamaduni wetu kudharau wanawake.

Ukienda hapo Kenya, utakuta akina mama wakubwa kiumri wakiendesha maisha yao bila kutegemea wanaume, na wana mitaji ya maana, huku bara pia, ndoa ni matokeo na wala siyo lazima uolewe ndiyo uwe na maisha. Kwa uliyoyasema kimsingi ni SEXUAL HARRASSMENT na unatakiwa uombe msamaha.

Samia chunga ulimi, usifuate unyanyasaji wa Magufuli wa kunyanyasa wanawake, wewe kama mwanamke heshimu wanawake ili uwe mfano kwa hilo kundi ambalo kwa nchi fukara na maskini ni "disadvantageous group" Kuna mambo mengi ambayo ninaamini wewe ukiwa serikalini na Magufuli mliyafanya, naanza kuamini unaweza kuwa ulikuwa sehemu ya kuwakandamiza wanawake kuwakataza kusoma wakiwa wajawazito hata kama wamebakwa, huku wanaume waliofanya hivyo vitendo wakiendelea na shule bila kuulizwa.

Mhe. rais, nchi yetu ni tofauti na Taliban, "WANAWAKE WANAYO HAKI, HAWAPASWI KUNYANYASWA HATA KIDOGO", mheshimiwa jitahidi uwe na simile kidogo
 
Sion kibaya alichozungumza.
Bhas tu mshamchukia.
Sijui akili zako, Ila kusema wale wadada wasaidiwe kwa sababu hawavutii kwa wanaume na wako flat hata ukiwaweka na wanaume huwezi tofautisha hivyo kuolewa baada ya kustaafu kucheza mpira itakuwa ngumu.

Huoni ubaya wa hii sababu ya kutaka wasaidiwe?
 
Shida ni kwamba, ucheshi anaufanya kama speech

Muda wote anaongea kama anasoma ngonjera
 
..
Screenshot_20210824-074314~2.jpg
 
Mheshimiwa rais Samia Suluhu Hassan, Kwa unyenyekevu na kwa heshima kubwa naomba niseme yafuatayo, nikiamini sikuvunjia heshima rais wangu.

Mhe. rais Samia, maneno uliyoyasema ni mazito na ya kumshushia hadhi mwanamke, kwanza huku bara tunajali utu na hatujawahi kukubali wanawake
Umeshamvunjia heshima kwa kumuandika rais badala ya Rais.

rais ni wa TFF nk..
 
Hiyo ndiyo hasara ya chama kutokuandaa mtu wa kuwa Rais. CCM hawakuwahi kujua kuwa huyu Mama wa kambo kuna siku anaweza kuwa Rais.
Suala la kumuandaa makamu wa rais kuwa rais kwa Tanzania halipo, refer chadema walipomteua Salim mwalimu kuwa makamu/mgombea mwenza je walimwandaa huyu kuwa rais? Angalau Samia amepitapita uongozi sehemu nyingi kuliko huyu wa certificate in journalism!
 
Suala la kumuandaa makamu wa rais kuwa rais kwa Tanzania halipo, refer chadema walipomteua Salim mwalimu kuwa makamu/mgombea mwenza je walimwandaa huyu kuwa rais? Angalau Samia amepitapita uongozi sehemu nyingi kuliko huyu wa certificate in journalism!
Kama chadema hawakumuandaa makamu wa rais kuja kuwa Rais haifanyi CCM kutokumuandaa makamu wa Rais kuja kuwa Rais liwe jambo sahihi.
 
Screenshot_20210824-075714~2.png


Amewazunguka wachezaji wake na kuwapiga chenga wenzake sasa anaelekea golini mwake akiukokota mpira kwa madaha.... Safi sana... Mama ana upiga mwingi sana.
 
Back
Top Bottom