Ni kweli kabisa alisema hayo maneno. Akiwa kama kiongozi wa nchi, tena Mwanamke hakupaswa kabisa kutamka hayo maneno dhidi ya Wanawake wenzake tena mbele ya vijana wa Kiume.
Kauli tata za viongozi huwa zinaleta ukakasi sana hasa kwa Wazungu. Kumbukeni yule Kiongozi wa Olympic kule Japan alivyoshambuliwa mpaka akajiuzulu baada ya kusema "wanawake wana ongea sana".
Kwa maneno hayo hata kama yalikuwa na ukweli lakini yalichukuliwa kuwa ni dharau kwa wanawake.
Sasa Madam SSH naye amesikika akisema, "wachezaji wanawake wanasura ngumu sana, ukimpeleka nyumbani Bi mkubwa atakushangaa na kukuuliza huyu ni mwanaume mwenzio au mwanamke"?
Ki ukweli Madam alikosea sana kusema hivyo. Naamini ataomba radhi maana Wazungu watamshikia bango mbaya. Ingekuwa ni nchi za wenzetu angeshajiuzulu.
Tutarajie FIFA womens org kutoa tamko kali sana kulaani matamshi ya Madam President SSH.
Swali la kujiuliza, hakuna watu wa kumwandikia hotuba Rais Samia?????