Wahenga walisema "kadri unavyopambana kuufumbata mchanga ndivyo unavyozidi kudondoka".
Vivyo hivyo na kwa upande wa madaraka, kadri kiongozi anavyopambana na watu ili kuyalinda ndivyo anayozidi kujiongezea maadui na wapinzani wa madaraka yake.
Mwisho wa siku anajikuta kishapambana na kila mtu/kundi na hukuna tena wa kumuunga mkono.
Alipoingia tu ikulu rais Samia alipewa maneno kuwa wabaya wake ni akina Dr. Bashiru, Lukuvi, Ndugai na Kabudi......akawaondoa.
Haikupita muda akasafisha wateule waliojulikana kama wafuasi wa sukuma gang....akina Kalemani, Dotto James, Herry James, Angelina Mabula, n.k.
Sasa amekuja kugundua kuwa kundi lililokuwa likimpa ushauri nalo halina nia njema na hatima ya kiti chake. Ndiyo unaona timua timua ya maafisa usalama, wasaidizi wake ikulu pamoja na akina Kinana, Nape, Makamba , n.k na wengine watafuata.
Hivi sasa mama anatapatapa, hajui aliamini kundi gani (wema hawafi ama sukuma gang )? Hofu yake kubwa ni kuwa aliowatumbua watautumia upinzani kumsulubu, na ndiyo maana amesahau 4R zake na kuanza kuwakamata hovyo wapinzani.
Nguvu kubwa kutaka kurejea tena ikulu inayotumika na rais Samia inatishia ushindi wake ktk uchaguzi ujao, 2025
N.B. Wakati wa kampeni za urais 2025 mkataba wa DP World utatembezwa kaya kwa kaya ili kila mwananchi ausome.