Rais Samia anapaswa tu kutuliza kichwa 'Patience', bado amefanya mazuri mengi. Atulize tu spidi bado ni kiongozi mzuri

Rais Samia anapaswa tu kutuliza kichwa 'Patience', bado amefanya mazuri mengi. Atulize tu spidi bado ni kiongozi mzuri

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2015
Posts
6,236
Reaction score
15,677
Mimi ni mmoja wa watu ambao huamini kwamba, mtu akichafuka mguuni sio kwamba amechafuka mwili mzima.

Hivyo basi, uungwana ni kuzodoa uchafu wa mguuni lakini wakati huo huo kusifia utanashati pale pote pazuri tofauti na mguu ambao umechafuka.

Hii inaitwa kuwa 'positive' katika kuyatizama maisha ya mwanadamu. Na sababu kubwa ni kwamba ni ngumu sana kukutana na binadamu aliye kamilika.

Hivo basi, hatuwezi kumpima binadamu kwa ukamilifu wake, bali mimi naamini binadamu anapaswa kupimwa kwa usikivu wake juu ya mapungufu yake na nia yake ya kubadilika.

Kwa case ya Rais Samia, niseme tu kwamba bado naamini mpaka sasa kwa mizani yangu, amefanya mambo mazuri kwa Tanzania.

1. Issue ya investors confidence na makaripio kwa TRA kuwa smart - huwezi kudogoza hichi kitu hata kidogo. Ukweli usemwe private sector ilikuwa inaenda ku collapse totally.

2. Kukubali Covid + chanjo -- bila hii milestone at national level. Hii nchi diplomatically tulikuwa tunaenda kutengwa.. nimefurahia sana namna alivocheza hii siasa ya Covid-19. Huwezi kuona kwa jicho la kawaida its a win.

3. Huwezi pia kudogoza mahabusu walioachiliwa kwa kesi za kihuni.. Hawa watu wa makesi ya uhujumu na msukumo wa kisiasa wangeozea jela.. Truth

Kwa machache hayo namna kudos Rais Samia.

Lakini hapo hapo ni kweli kwamba kuna mambo ya msingi ambayo yanaweza kumpotezea dira ya uongozi wake na ni vitu nadhani ana control navyo..

1. Issue ya Mbowe na kesi ya ugaidi ni error kubwa sana na mimi naiona kama threats kubwa ukiangalia dunia inapokwenda kwa sasa viongozi wengi wa kidunia sasahivi wana misimamo ya ki Globalist... na Globalism ni purely Capitalist system... Dunia haiwez kumuelewa kwa kuonyesha wazi kukandamiza upinzani na hii itakuwa hatari sana.

kuna street smart za kufanya oppression but sio kwa style hii. Na nadhani hapa angejifunza kwa Magafuli, ukandamizaji wa namna hii hatashinda, Globalism haipendi ukandamizaji wa wazi hivi wa democrasia.. there is a street smart to oppress anatakiwa kujifunza.

2. Maneno mepesi mepesi hayalipi. Hii mambo ya kusema sijui mi mwanamke ooh sijui lazima nigombee.. ni kwamba inasema wazi kwamba yupo insecure. You are the president, we fanya mambo mazuri tu, watu wataandamana uwe Rais wa milele.. ila huwezi kuwa Rais kwa matakwa yako.. wewe mwenyewe angalia ulivokuwa Rais.. its a natural process..

So madam President.. just relax.. kuna mazuri umefanya ila ningependa nione unasikiliza na kubadilika maana bado una muda.

N. Mushi
Mtetezi wa wanyonge
 
Inawezekana hata hilo wazo la kugombea 2025 amepewa na wana kikundi wenzake wa kule Msoga, peke yake kwa ile body language yake miezi michache iliyopita alishachoka vurugu za Urais.

Anampa uwaziri Makamba halafu naye anatangaza nia kwa 2025 hapo inawezekana kuna mchezo unasukwa kwa ajili ya 2030.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
😂😂😂😂
hakuna namna lazima tutumie kila namna ili abadilike.. sasa kama uchaguzi unaibwa mchana peupe na wananchi wapo kimya, we unadhani kuna option gani ingine zaidi ya kumshauri kiongozi wa Ccm
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Inawezekana hata hilo wazo la kugombea 2025 amepewa na wana kikundi wenzake wa kule Msoga, peke yake kwa ile body language yake alishachoka vurugu za urais.
Duh.. lakini kama kambi ya Msoga ndo wana Engineer haya basi watakuwa sio wazalendo na nchi yao? Kwanini wafanye hivi???
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Duh.. lakini kama kambi ya Msoga ndo wana Engineer haya basi watakuwa sio wazalendo na nchi yao? Kwanini wafanye hivi???
Wana interest kwenye maeneo kadhaa hasa minerals, lazima wawe na uhakika wa security ya investment zao, na umeme, but also, Samia nae kwa nature ya makundi ya CCM lazima atafute kundi lake la kumlinda kwa interest zake 2025.
 
Wana interest kwenye maeneo kadhaa hasa minerals, lazima wawe na uhakika wa security ya investment zao, na umeme, but also, Samia nae kwa nature ya makundi ya CCM lazima atafute kundi lake la kumlinda kwa interest zake 2025.
Anyway sijui ni kweli kiasi gani ila kama itakuwa ni ukweli basi we are in big trouble... na hii ina maanisha tutegemee ukiukwaji wa haki za kimsingi na ukandamizaji kuendelea.

Namna pekee ya uporaji wa mali za nchi inaenda sambamba na kunyamazisha wanaokereka na wizi.
 
Maccm yote Mkuu hayana uzalendo Mkuu. Unakuwaje mzalendo na kushindwa kuitakia nchi yako mema kama kuwa na chaguzi HURU na za HAKI? Unakuwaje mzalendo halafu CAG Kichere anatishiwa maisha yake kwa kuandika ripoti iliyojaa wizi, ufisadi na ubadhirifu na hakuna yeyote yule ndani ya Serikali au maccm anasimama kuwakemea wahuni wanaotaka kumuua CAG Kichere?
1631815855487.jpeg

Duh.. lakini kama kambi ya Msoga ndo wana Engineer haya basi watakuwa sio wazalendo na nchi yao? Kwanini wafanye hivi???
 
Hayati Nyerere angerudi akute Haya angetutandika viboko nchi nzima. Majitu yanasifia tuu ujinga unawezaje kutafuta uongozi kwa kugawa watu badala ya kuwaunganisha?

Hakuna wazee werevu na wenye busara wa kukemea hiikitu ya hovyo??
 
Back
Top Bottom