Rais Samia anarudi zama za siasa za chuki au anawajibu wanaombipu?

Hamna dikteta atakaye baki salama. Salmin Amour aliishia kupofuka macho, Mwendazake msiba wake ukageuka sherehe nchi nzima, Mr. Clean aliishia kuwa mlevi mbwa hadi akafia kwenye sinki la chooni akiwa amelewa chakari.
Namkumbusha tu bi Mkubwa , Bora ya mwisho mzuri kuliko mwanzo mzuri wenye mwisho mbaya.
Nilifikiri unasema ccm inakufa! Kumbe unaongea kufa kwa watu binafsi?
 
Nilimuomba Mama awe mkali kidogo hili genge la hawa Chadema lina hitaji kwenda nalo kwa akili kubwa kadili wao wanavyoleta uhuni.

Tupo katika mapambano na Covid 19 na wao wamekuwa wakihimiza serikali kuchukua hatua za kupambana na ugonjwa, serikali inawapa maelekezo wanakaidi sasa uhuni unatakiwa kudhibitiwa kwa namna yake.

Safi Mama sana Mama ni mwendo wa long balls sasa hakuna cha mwingi tutapoteza mechi Watanzania.
 
Magufuli alifanya huo ubatili mwisho wa siku Nchi aliyodhani ni yake ameiacha. Tumebak8 tunatamba na pumzi yetu sisi aliodhani hatustahili kuishi.

Endeleeni kumpaisha bichwa. Wengine wamepita na yeye atapita.
Waambie Chadema wapunguze uanaharakati watii sheria na maagizo ya mamlaka, huu uhuni hausaidii.
 
kwa hio unakubali kulikua na siasa za chuki eehhhhh?
 
Kuna features kadhaa kuhusu matukio makubwa mawili yaliyojiri siku chache zilizopita, la kukamatwa Mheshimiwa Mbowe na viongozi wengine kadhaa wa Chadema, na kabla ya hapo, kukamatwa kwa wafuasi kadhaa wa chama hicho, matukio yaliyojiri huko Mwanza.

Kwanza, hoja za jeshi la polisi na mkuu wa mkoa Mwanza kuzuwia kongamano kwa kigezo cha korona ni utopolo. Hilo halina mjadala.

Pili, kuzuwia kongamano hilo pamoja na lile la awali ni ukiukwaji wa haki za kidemokrasia na kikatiba. Freedom of association sio fadhila bali haki ya msingi kwa kila Mtanzania. Polisi wanapaswa kutoa ulinzi kwenye matukio husika na sio kuwa waamuzi wa endapo shughuli ifanyike au la.

Tatu, kama ilivyokuwa utawala uliopita, kuna double standards, ambapo CCM "wanapeta" tu ilhali ni kosa la jinai kwa Wapinzani japo kijaribu hayohayo CCM wanaruhusiwa kuyafanya.

Nne, kukamatwa kwa Mheshimiwa Mbowe na viongozi wengine wa Chadema kunatia doa taswira nzuri iliyoanza kujengeka kuwa Mama Samia anataka siasa za maelewano badala ya siasa za chuki zilizotawala zama za Mwendazake. Kuachiwa kwa Mdude na kugeuzwa hukumu ya Mbowe ni miongoni mwa ishara zilizotupa matumaini wengi kuhusu Mama Samia.

Tano, siasa za Tanzania na zero-sum game: Unfortunately siasa za Tanzania ni aidha ishinde CCM na Wapinzani wafeli au wapinzani wafaulu na CCM washindwe. Ni vigumu mno kupata suluhu kwenye masuala muhimu ya mustakabali wa kitaifa yanayohitaji mshikamano wa pande zote mbili.

Na ndio maana kwa mazingira ya sasa ni vigumu mno kwa madai ya Katiba mpya kuwa na ufanisi kwa sababu CCM wanajiona washindi wakikwamisha mchakato huo (unfortunately kwa vile ni chama tawala wana uwezo wa kukwamisha) na wanatafsiri kuwa kukwamisha huko ni "kuwapiga bao" Wapinzani

Ufumbuzi: win-win. Katiba ni kwa ajili ya Watanzania wote. Washindi ni Watanzania, sio chama fulani. Ikishindikana, waliofeli ni Watanzania wote, sio kundi flani.

Sita, Sambamba na hilo, confrontational politics ni ngumu japo wakati mwingine ndio only option. Katika mazingira ya sasa, sidhani kama mkutano kati ya Mama Samia na viongozi wa upinzani utakuwepo tena maana tayari "mstari umechorwa."

Saba, kwa upande mwingine, pengine Mama Samia hajatendewa haki kwenye hilo la mkutano na viongozi wa upinzani. Alikuwa na kila ruhusa ya kutamka kuwa "sihitaji kukutana na Wapinzani" na isingemuathiri kwa lolote, lakini akakubali.

Unfortunately, viongozi wa Chadema wanataka mkutano huo ufanyike mapema kadri iwezekanavyo, which is a valid point. However, kutokana na uzito wa mkutano huo, ni muhimu kuwe na maandalizi ya kutosha. On one side, hakutokuwa na tija endapo mkutano utaishia kuwa fursa ya Mama na wapinzani kunywa kahawa kisha kupiga picha pasipo kujadiliana masuala muhimu kwa taifa letu. On the other side, anayeombwa appointment, hapangiwi wala halazimishwi na mwomba appointment.

Ufumbuzi: kunahitajika ustahimilivu, assuming possibility ya mkutano huo bado ipo, though I highly doubt.

Nane, madai ya katiba mpya ni valid. Katiba Iliyopo ina mapungufu makubwa. Now, whether kinachohitajika ni katiba mpya au marekebisho kwenye katiba iliyopo, that's open to discussion.

However, approach ya kudai katiba ipo a bit flawed. Kws kuzingatia kuwa siasa zetu ni za zero-sum, it is virtually impossible kwa CCM kuridhia mchakato wa Katiba mpya, kwa sababu watakuwa wanajipiga bao. It essentially would fast-track safari ya wao kitoka madarakani.

Tisa, kuna kikwazo cha pili. Ni kwamba utamaduni wa siasa za Tanzania, na hata baadhi ya nchi kubwa, hutegemea sana utashi wa kiongozi aliyepo madarakani. Tumeona zama za Magufuli. Aliyotaka yawe yakawa. Aliyitaka yasiwe hayakuwa. Lakini hata Marekani, utashi wa Obama uliifanya Marekani kuwa "tofauti" na "Marekani ya Trump," na "ya Biden" ni tofauti pia. Na hili ni taifa lenye katiba imara na kongwe.

Ufumbuzi: pamoja na ugumu mwingi, only viable way ya kuwezesha mchakato wa Katiba ni kuhusisha utashi wa Mama Samia, kufanikiwa kuwavuta CCM waone kuwa ni win-win na sio zero-sum game, na suala la katiba kuwa la kitaifa zaidi kuliko "la chama kimoja."

Kumi, no si dhambi kwa Chadema kuongoza harakati za kudai Katiba mpya. However, on on side kuna kikwazo hicho cha CCM, lakini tatizo kubwa zaidi ni kwamba kuna watu watakaokwepa kuunga mkono katiba mpya kwa vile tu ni "sera ya chama flani." Ikumbukwe, zaidi ya nusu ya Watanzania si wafuasi wa chama chochote cha siasa.

Mwisho, ni jawabu la swali lililobeba kichwa cha habari. Je Mama Samia anairudisha Tanzania kwenye zama za siasa za chuki au huu ni utekelezaji wa kile alichotanabaisha mapema kuwa "ukinizingua nitakuzingua"?

Hilo moja, la pili, na linalohitaji tafakuri kubwa ni ukweli mchungu kuwa hata Mama Samia akiamua "kuachana na siasa za kistaarabu" na kuwa full tyrant, hakuna ww kumzuwia. Hakuna aliyeweza kumzuwia Mkapa kuukandamiza upinzani 1995 to 2005. Hakuna aliyeweza kumzuwia Jk kuuma na kupuliza ambapo hadharani alionekana mtu poa kwa wapinzani ilhali faraghani aliwahujumu. Na hakuna kilichoweza kumzuwia Shujaa Mwendazake kufanya siasa za chuki ambapo aliwanyanyasa wapinzani atakavyo.

Ukweli mwingine mchungu ni kwamba tangu jana ni "porojo" tu, Spaces, nk lakini hadi muda huu kinachosubiriwa ni "huruma ya serikali" kuwaachia Mheshimiwa Mbowe na wenzake. Katika mazingira haya ambayo watu ni mahiri sana wa kuongea na kujimwambafai kuliko kutenda, pengine ni muhimu kuwa na Plan B kabla ya kufanya jambo ambalo matokeo yake yanafahamika. Kwa tukio la Mwanza, ilifahamika bayana nini kingetokea, lakini ni wazi there was no plan B. Another zero-sum game?

Kuna video hapa chini inayoeleza hoja hizo zote kwa upana

Kati kati ya nane na tisa pale However....ni kwanini unafikiri Chama Cha Mapinduzi aka CCM walianzisha mchakato wa katiba enzi zile chini ya JK?

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Umejaribu kuandika vizuri ingawa kua sehemu hazija kaa vema (to me anyway). Bottomline ni kuwa Africa needs a second wave of armed strugle! Kinachoitwa uhuru wa watangulizi wanaojiita wapigania uhuru akina Nyerere and team ni WAKOLONI WEUSI AGAINST WEUSI WENZAO. Kilichofanyika ni kubadirisha makucha ya weupe na kuyaweka kwa weusi. Trend in Africa actually mtu anaweza kusema afadhali ya Mkoloni!
Hivyo huko mbele hata iwe miak 1000, kutakuwa na vita kila mahali Africa kupinga ukoloni wa WEUSI vs WEUSI
Ambayo hata Ulaya wazungu na Uchina huko waliifanya, waliupiga mwingi sana wao kwa wao kupeana adabu hadi wakanyoka na kustaarabika hapo walipo

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Kuna features kadhaa kuhusu matukio makubwa mawili yaliyojiri siku chache zilizopita, la kukamatwa Mheshimiwa Mbowe na viongozi wengine kadhaa wa Chadema, na kabla ya hapo, kukamatwa kwa wafuasi kadhaa wa chama hicho, matukio yaliyojiri huko Mwanza.

Kwanza, hoja za jeshi la polisi na mkuu wa mkoa Mwanza kuzuwia kongamano kwa kigezo cha korona ni utopolo. Hilo halina mjadala.

Pili, kuzuwia kongamano hilo pamoja na lile la awali ni ukiukwaji wa haki za kidemokrasia na kikatiba. Freedom of association sio fadhila bali haki ya msingi kwa kila Mtanzania. Polisi wanapaswa kutoa ulinzi kwenye matukio husika na sio kuwa waamuzi wa endapo shughuli ifanyike au la.

Tatu, kama ilivyokuwa utawala uliopita, kuna double standards, ambapo CCM "wanapeta" tu ilhali ni kosa la jinai kwa Wapinzani japo kijaribu hayohayo CCM wanaruhusiwa kuyafanya.

Nne, kukamatwa kwa Mheshimiwa Mbowe na viongozi wengine wa Chadema kunatia doa taswira nzuri iliyoanza kujengeka kuwa Mama Samia anataka siasa za maelewano badala ya siasa za chuki zilizotawala zama za Mwendazake. Kuachiwa kwa Mdude na kugeuzwa hukumu ya Mbowe ni miongoni mwa ishara zilizotupa matumaini wengi kuhusu Mama Samia.

Tano, siasa za Tanzania na zero-sum game: Unfortunately siasa za Tanzania ni aidha ishinde CCM na Wapinzani wafeli au wapinzani wafaulu na CCM washindwe. Ni vigumu mno kupata suluhu kwenye masuala muhimu ya mustakabali wa kitaifa yanayohitaji mshikamano wa pande zote mbili.

Na ndio maana kwa mazingira ya sasa ni vigumu mno kwa madai ya Katiba mpya kuwa na ufanisi kwa sababu CCM wanajiona washindi wakikwamisha mchakato huo (unfortunately kwa vile ni chama tawala wana uwezo wa kukwamisha) na wanatafsiri kuwa kukwamisha huko ni "kuwapiga bao" Wapinzani

Ufumbuzi: win-win. Katiba ni kwa ajili ya Watanzania wote. Washindi ni Watanzania, sio chama fulani. Ikishindikana, waliofeli ni Watanzania wote, sio kundi flani.

Sita, Sambamba na hilo, confrontational politics ni ngumu japo wakati mwingine ndio only option. Katika mazingira ya sasa, sidhani kama mkutano kati ya Mama Samia na viongozi wa upinzani utakuwepo tena maana tayari "mstari umechorwa."

Saba, kwa upande mwingine, pengine Mama Samia hajatendewa haki kwenye hilo la mkutano na viongozi wa upinzani. Alikuwa na kila ruhusa ya kutamka kuwa "sihitaji kukutana na Wapinzani" na isingemuathiri kwa lolote, lakini akakubali.

Unfortunately, viongozi wa Chadema wanataka mkutano huo ufanyike mapema kadri iwezekanavyo, which is a valid point. However, kutokana na uzito wa mkutano huo, ni muhimu kuwe na maandalizi ya kutosha. On one side, hakutokuwa na tija endapo mkutano utaishia kuwa fursa ya Mama na wapinzani kunywa kahawa kisha kupiga picha pasipo kujadiliana masuala muhimu kwa taifa letu. On the other side, anayeombwa appointment, hapangiwi wala halazimishwi na mwomba appointment.

Ufumbuzi: kunahitajika ustahimilivu, assuming possibility ya mkutano huo bado ipo, though I highly doubt.

Nane, madai ya katiba mpya ni valid. Katiba Iliyopo ina mapungufu makubwa. Now, whether kinachohitajika ni katiba mpya au marekebisho kwenye katiba iliyopo, that's open to discussion.

However, approach ya kudai katiba ipo a bit flawed. Kws kuzingatia kuwa siasa zetu ni za zero-sum, it is virtually impossible kwa CCM kuridhia mchakato wa Katiba mpya, kwa sababu watakuwa wanajipiga bao. It essentially would fast-track safari ya wao kitoka madarakani.

Tisa, kuna kikwazo cha pili. Ni kwamba utamaduni wa siasa za Tanzania, na hata baadhi ya nchi kubwa, hutegemea sana utashi wa kiongozi aliyepo madarakani. Tumeona zama za Magufuli. Aliyotaka yawe yakawa. Aliyitaka yasiwe hayakuwa. Lakini hata Marekani, utashi wa Obama uliifanya Marekani kuwa "tofauti" na "Marekani ya Trump," na "ya Biden" ni tofauti pia. Na hili ni taifa lenye katiba imara na kongwe.

Ufumbuzi: pamoja na ugumu mwingi, only viable way ya kuwezesha mchakato wa Katiba ni kuhusisha utashi wa Mama Samia, kufanikiwa kuwavuta CCM waone kuwa ni win-win na sio zero-sum game, na suala la katiba kuwa la kitaifa zaidi kuliko "la chama kimoja."

Kumi, no si dhambi kwa Chadema kuongoza harakati za kudai Katiba mpya. However, on on side kuna kikwazo hicho cha CCM, lakini tatizo kubwa zaidi ni kwamba kuna watu watakaokwepa kuunga mkono katiba mpya kwa vile tu ni "sera ya chama flani." Ikumbukwe, zaidi ya nusu ya Watanzania si wafuasi wa chama chochote cha siasa.

Mwisho, ni jawabu la swali lililobeba kichwa cha habari. Je Mama Samia anairudisha Tanzania kwenye zama za siasa za chuki au huu ni utekelezaji wa kile alichotanabaisha mapema kuwa "ukinizingua nitakuzingua"?

Hilo moja, la pili, na linalohitaji tafakuri kubwa ni ukweli mchungu kuwa hata Mama Samia akiamua "kuachana na siasa za kistaarabu" na kuwa full tyrant, hakuna ww kumzuwia. Hakuna aliyeweza kumzuwia Mkapa kuukandamiza upinzani 1995 to 2005. Hakuna aliyeweza kumzuwia Jk kuuma na kupuliza ambapo hadharani alionekana mtu poa kwa wapinzani ilhali faraghani aliwahujumu. Na hakuna kilichoweza kumzuwia Shujaa Mwendazake kufanya siasa za chuki ambapo aliwanyanyasa wapinzani atakavyo.

Ukweli mwingine mchungu ni kwamba tangu jana ni "porojo" tu, Spaces, nk lakini hadi muda huu kinachosubiriwa ni "huruma ya serikali" kuwaachia Mheshimiwa Mbowe na wenzake. Katika mazingira haya ambayo watu ni mahiri sana wa kuongea na kujimwambafai kuliko kutenda, pengine ni muhimu kuwa na Plan B kabla ya kufanya jambo ambalo matokeo yake yanafahamika. Kwa tukio la Mwanza, ilifahamika bayana nini kingetokea, lakini ni wazi there was no plan B. Another zero-sum game?

Kuna video hapa chini inayoeleza hoja hizo zote kwa upana

Kiukweli kabisa kazi ya rais ni kuheshimu katiba na kiapo chake.
Hapaswi kufanya maamuzi ya jazba, kukomoa, kujitutumua , maana kufanya hivyo ni udhaifu
 
Hamna dikteta atakaye baki salama. Salmin Amour aliishia kupofuka macho, Mwendazake msiba wake ukageuka sherehe nchi nzima, Mr. Clean aliishia kuwa mlevi mbwa hadi akafia kwenye sinki la chooni akiwa amelewa chakari.
Namkumbusha tu bi Mkubwa , Bora ya mwisho mzuri kuliko mwanzo mzuri wenye mwisho mbaya.
Kuna nn Burundi ni baada ya kutoka tu huko
 
Asante sana Kwa kuniwakilisha.

Kwa kuongezea tu ni hv:

CHADEMA wanajitahidi sana kucheza generational politics ilhali CCM yangu inafanya siasa za wakati wa nyuma sana.

The fact ni kwamba, siasa za upinzani zitakuja kushinda huko mbele tuendako kwa sababu ndani ya CCM kutatokea hujuma za wenyewe kwa wenyewe as time goes on.

Nijuavyo deep state ni kwamba wana CCM wengi hawaridhishwi na muenendo wa siasa za CCM dhidi ya wapinzani.

Reference nzuri zaidi: The Rise of Kigogo2014 wa twitter
Umeongea vitu vizito na vinavoumia (ukweli mchungu)Haya mambo hayako mbali yatakua kweli.
 
Hamna dikteta atakaye baki salama. Salmin Amour aliishia kupofuka macho, Mwendazake msiba wake ukageuka sherehe nchi nzima, Mr. Clean aliishia kuwa mlevi mbwa hadi akafia kwenye sinki la chooni akiwa amelewa chakari.
Namkumbusha tu bi Mkubwa , Bora ya mwisho mzuri kuliko mwanzo mzuri wenye mwisho mbaya.
Hivi mr clean ni nani bro [emoji3064]
 
Kiukweli kabisa kazi ya rais ni kuheshimu katiba na kiapo chake.
Hapaswi kufanya maamuzi ya jazba, kukomoa, kujitutumua , maana kufanya hivyo ni udhaifu

..Nadhani tatizo la CCM ni hofu kwamba katiba mpya itawaondoa madaraka.

..Naamini wakikaa na kufanya uchambuzi wa kina watagundua kwamba hata katiba mpya ikija upo uwezekano mkubwa wa wao kuendelea kuwa madarakani.

..Njia ya hujuma na ukatili dhidi ya wapinzani naamini ni risky na unsustainable. Naamini ni vigumu kutawala kwa mkono wa chuma kuliko kutawala kwa haki na usawa kwa Watz wote.
 
Uko sahihi, Kukimbizana na wapinzani daily kwanza kunawapotezea watawala muda wa kufanya shughuli za maendeleo na eventually hata vyombo vya usalama vitawaambia tu kuwa hizi opearation za kuoneaonea wapinzani hazi values zozote za kijeshi bali ni civilian issues zinazoweza kumalizwa na watawala kwa kutimiza wajibu wao
Wapinzani wanachopaswa kufanya ni kuapply pressure na pressure bila kukoma, ipo siku kitaeleweka tu
 
Ghana ilifanya second armed struggle kumuondoa Nkwame Nkurumah kwa kujivisha ukoloni mweusi kwa weusi baada ya wazungu Leo hii Ghana Ni nchi yenye ustawi sawia na usio na shaka juu ya democracy

God blessing Africa continent.Amen
Sidhani kama unajua unachozunguza.
 
Anawajibu wanaombipu!

Hata JPM hakuwa na siasa za chuki ila hakutaka siasa uchwara kama hizi za akina Mbowe!

Magufuli alikuwa na chuki tena ya wazi. Usitegemee utamtumia huyu mama kumsafisha Magufuli. Huyu mama wa kambo yeye kapata urais wa kurithi, kibaya zaidi akabebana na genge la Magufuli, hivyo hana namna zaidi ya kuburuzwa na genge la Magufuli. Akitaka ajitenge na hiki kinachoendelea ni kutupilia mbali hilo genge haramu. Ifahamike hata huyo Magufuli mwenyewe alikuwa hamshirikishi mama wa kambo kwenye mambo mengi, yeye anaendekeza nini hilo genge haramu?
 
Back
Top Bottom