Rais Samia anarudi zama za siasa za chuki au anawajibu wanaombipu?

Kinachofanyika ni serikali kupambana na wajinga wachache wanaofikiri wao ndio watanzania na lazima wasikilizwe kwa chochote ikiwa pamoja na kudekezwa....leo wakipewa katiba mpya kesho watakuja na dai lingine, mwisho wanaweza kukwambia kila mwanaume awe na mme wake...... ni kama nyumbani tu, ukidekeza sana mtoto kuna mahala utajiona fala na kurudi kwenye viboko....Harakati za CDM zina mengi saaana yamejificha nyuma na wenye mahitaji yao huwezi kuwaona zaidi ya kuchochea kuni.......CDM ni kama mtoto aliyedekezwa sana sasa anafanya vitu vya hovyo nyumbani ili akae sawa anahitaji viboko kila kukicha...
 

Mmebaki kwenye siasa za hila za kizee mpaka mmegeuka kuwa vituko. Jana hiyo Mwanza kulikuwa na mechi ya mpira kati ya pamba ya Coastal union na hakuna aliyevaa barakoa. Hapo mlipo mnampeleka mama wa kambo kwenye siasa za mabavu, wakati hana uwezo wa kufanana na yule dhalimu kwa chochote.
 
Mbowe alipotoka dubai akatamba na chedema kidigitali hakubughudhiwa lakini kuna nyakati ni lazima tutambue kua wananchi wanahitaji utulivu pia mtaka yote pupa hukosa yote.Tujifunze kua na utulivu wakati wa kupenyeza ajenda za vyama vyetu kwa wananchi huku tukitambua ukweli kua wananchi wetu wamegawanyika kiitikadi hivyo wanahitaji kushawishiwa.
 
Uchambuzi wako leo umeenda shule. Hongera. Ni tofauti kabisa na ile thread ya Mdude uliyoanzanisha. Leo umetoa uchambuzi wa kisomi na unaakisi hali halisi!
 
Huu ni mtazamo wa kizee ile mbaya, mlikuwa mnadanganya wananchi kuwa nchi hii ni tajiri na kuna raslimali kibao, na porojo sijui wazungu wanatuonea wivu. Mbona hizo raslimali zetu hatuzioni zikiuzwa tuondokane na hii double taxation kwenye line za simu? Au hizi line zetu za simu ndio hizo raslimali wazungu wanazionea wivu?

Mmewadanganya ACT huko Zanzibar wameingia serikali ya umoja wa kitaifa sijui kuponya majeraha. Mbona kila uchafuzi wa marudio vilio vyao ni vilevile, badala ya kuona afadhali kuwa sasa wanafanya siasa zinazokubalika na ccm. Jana ACT wamemsusia Mwinyi sherehe za Iddy huko Pemba baada ya kupigwa kata funua. Ni hivi, ukweli ni kuwa ccm haiwezi tena kushindana kwa hoja, wamebaki kutegemea mabavu. Hiyo eti kuwa cdm wanafanya siasa zisizo za kistaarabu ni ghiliba kwa wajinga.
 
Huyu mama alikaa na Magufuli akaona namna alivyokuwa akiburuza watu sasa na yeye anaiga kile kile kilichomponza mtangulizi wake kwani ukikaa karibu na waridi utanukia waridi.

Ccm wanaamini kabisa kwamba katiba yoyote tofauti na hii yao ndio itakuwa kiyama chao hivyo watajaribu hujuma zote kuhakikisha kwamba wanaitetea ibaki.

Lakini bahati mbaya sana kwao ni kwamba wanapambana ktk wakati mgumu sana ambapo kuna kila dalili kwamba hawatafaulu na kifo cha ghafla cha Magufuli ni uthibitisho wa wazi kwamba kuna yatakayofanyika huko mbele ambayo hayata nufaisha lengo lao.
 

hahahahahaha Bwana Tindo....mama ili awe pembeni ya genge haramu basi akubaliane na CDM na awape katiba mpya.... Tindo, JK alijaribu kwenda sawa sana na upinzani kwa kufuata misingi ya demokrasia, kutoa uhuru wa vyombo vya habari, kuruhusu mikutano ya siasa, kuruhusi majadiliano na upinzani mpaka Ikulu....mwisho wa siku JK tukamuita dhaifu, boyz 2 men, anachekacheka tu, mara nchi imemshinda, mara mwanae anauza unga mara kakamatwa china, Dr slaa na TL wakawa wanatupiga uongo mwingi sana, tukaenda mbali tukasema nchi hii inahitaji dikteta na mtu mwenye maamuzo magumu...akaja JPM akaanza kutubinya huku na kule naye akawa hafai na wala hakuna aliyejaribu kufanya kongamano la katiba...leo mama tena naye hafai na manenoo meeengi...

Tujitafakari na kuangalia au kufikiri nini tunataka, kwangu mimi Katiba siona kama ina umuhimu kwa sasa zaidi ya matatizo meeengi tuliyonayo yanayohitaji suluhu, hebu tuachane na upande wa wanasiasa tusimame kama raia kudai haki zetu za msingi sio kuendeshwa na mitazamo ya wanasiasa kwa maslahi yao..
 
Ghana ilifanya second armed struggle kumuondoa Nkwame Nkurumah kwa kujivisha ukoloni mweusi kwa weusi baada ya wazungu Leo hii Ghana Ni nchi yenye ustawi sawia na usio na shaka juu ya democracy

God blessing Africa continent.Amen
Bado wana matatizo yao mkuu, siyo kwamba democracy yao ipo perfect 100%, hamna democracy iliyo kamili 100%. Wachina wakaona wasiwe wanafiki waachane na hii democracy ya kuiga west
 

Tindo, binafsi sishabikii chama chochote cha siasa maana siamini katika fikra za wanasiasa oya oya....1995 sikupiga kura maana nilikuwa naijua sinema, 2000 sikupiga kura maana sikuona aliye serious na kuijua sinema, 2005 sikupiga kura, 2010 sikupiga kura, 2015 nilikwenda kupiga kura na kumchagua JPM baada ya kukubaliana na baadhi ya mitizamo yake hasa TZ ya viwanda na undava dhidi ya wapumbavu na wajinga... 2020 sikupiga kura, nilitofautiana mitazamo na JPM dhidi ya approach zake toward Tanzania ya viwanda na ujenzi wa mastructure hovyo hovyo bila kuwa strategically, nilikubaliana naye kw undava wake na ujeuri, maamuzi magumu na kutengeneza dola inayoogopwa na kuheshimika.. 2020 upinzania haukuwa na mgombea serious zaidi ya oya oya na makelele tu...naomba pia nikwambia hili " fanya research yako mwenyewe privately upate kumjua mbowe ni nani na ukirudi nyuma kidogo kwenye ule ugomvi wake na ZZK unaweza kusmell kitu na ukirudi nyuma kidogo ukazama katikati ya mistari ya hutaki unaacha utasmell kitu pia"..

Back to the topic, sio kila anayepingana mtazamo na CDM atakuwa CCM hapana anaweza kuwa chauma, anaweza kuwa ACT anaweza kuwa UDP....na sio kila harakati za CDM lazima ziungwe mkono na kila chama au kila mtu hapana pia...inaonekana pia hujui kwanini ACT walikubaliana na CCM na aliyekuwa nyuma ya makubaliano ni nani, jaribu pia kuunganisha historia ya Zanzibar vs siasa za Zanzibar....Kuna mengi sana bwana tunahitaji kuyafahamu pamoja na kuichukia kwetu CCM....kwa sasa naamini kwenye kuipa pressure CCM ikatuogopa wananchi kuliko kuamini agenda na harakati za wanasiasa..
 
Bado wana matatizo yao mkuu, siyo kwamba democracy yao ipo perfect 100%, hamna democracy iliyo kamili 100%. Wachina wakaona wasiwe wanafiki waachane na hii democracy ya kuiga west

Watu huwa wanapenda kutolea mifano mataifa mengine kwa kusikia bila kufanya uchunguzi...eti "Ghana wana democracy" watu wanawaza democracy ya uchaguzi ambayo hata Ivory coast ipo, Senegal ipo, Mali ipo, Liberia ipo nk...hiyo Ghana juzi tu hapa walikuwa kwenye mgogoro wa uchaguzi, mtu anaitolea mfano Ghana eti imeendelea dah kweli tembea uone......
 
Hata JPM hakuwa na siasa za chuki ila hakutaka siasa uchwara kama hizi za akina Mbowe!
Chadema ndiyo walimbadilisha JPM baada ya kuanza siasa za kijinga za kupinga kila kitu. Lisu akafie mbali na huo ujinga aliouanzisha.
Mama amekuwa nice kwa chadema akitegemea mambo yatabadilika na mahusiano yawe mazuri, nadhani alisahau kuwa chadema ya sasa siyo chama cha siasa, ni genge tu la wahuni wasio na maadili yoyote ya kuendesha siasa za kistaarabu.
Waliombipu wamelikoroga, sasa walinywe.
 

Hiyo paragraph yako ya kwanza maoni yako ni yale yale ya bendera fuata upepo. Huyo JK alipewa ukweli wake, unajaribu kuongea kama vile JK alionewa au alitenda haki sana. JK hakumfanyia yoyote hisani maana nchi haikuwa yake. Na kimsingi alijifaidisha yeye na familia yake, na genge lake. Magufuli aliingia kwa pupa na alikuwa hafanyi Siasa, bali alikuwa mlevi wa madaraka, na kwasababu ya pupa yake kageuka kuwa ivumayo haidumu. Tunamshukuru Mungu kwa kutuondolea yule mtu muovu bila damu kumwagika.

Huyu mama wa kambo alianza vizuri, ila naona amegeuka kuwa mgema akisifiwa. Isitoshe huyu mama hana maamuzi yoyote ya kwake, maana ni urais wa urithi.Hivyo anaongoza kwa kutaka kumuiga Magufuli wakati wala hapatii, na isitoshe hakuna uhakika kuwa style ya Magufuli ilikuwa inakubalika na wengi, kwani hakuwa anaheshimu uchaguzi.

Unasema tujiunge kudai haki zetu, kwani hao wapinzani wamezuia wananchi kudai haki zao? Au unajichanganya nini boss. Au hao wananchi wanasubiri mpaka wapinzani wanyamaze na wao ndio waanze kudai hizo haki zao?
 

Nyie ndio mlimsifia kwa kila kitu aliishia kupika data. Magu hakubadilishwa na mtu yoyote bali alikuwa na kichaa na mtu mwenye roho chafu.
 
Mama nae hataki kujaribiwa,wala hataki kupelekwa pelekwa,wala hataki kuchukuliwa powa.
Hilo la Mbowe tulitegemea kwani Mbowe alitamka wazi kuwa hakuna muda wa kusubiri,wakati mama nae anasema tusubiri.
Tatizo kubwa hapa si Chadema au vyama vya upinzani kuhusu mchakato wa kupata katiba mpya,tatizo kubwa hatujui msimamo wa chama tawala.
 

Sisi wananchi tunangoja nini kuipa hiyo ccm pressure, au tunasubiri mpaka hivyo vyama vya upinzani vife kwanza? Hebu niambie wananchi mnangoja nini, na mpaka lini mtaanza?
 
Kinachoendelea sasa hivi ni kielelezo halisi cha nchi kukosa mwelekeo.

Nilitegemea ccm iliyosheheni wasomi ije na hoja kinzani juu ya hoja za wasomi badala yake inakuja na mabomu na mbwa wa polisi.

Nchi inayoongozwa na watu wanaofikiri kama ccm ya sasa hawawezi kuongoza nchi kwa mwelekeo sahihi.
 
Sisi wananchi tunangoja nini kuipa hiyo ccm pressure, au tunasubiri mpaka hivyo vyama vya upinzani vife kwanza? Hebu niambie wananchi mnangoja nini, na mpaka lini mtaanza?

wakati haujafika na ukifika utaona tu CCM inavyotaka madarakani kila rahisi kabisa mpaka utashangaa....hili zingatia, watanzania bado hawajaichoka CCM kama unavyofikiri ila siku wakiichoka ni week moja tu CCM tunaisahau na hata hawa polisi unaowaona leo hii wanaweza kumkamata yeyote na kuweka ndani bila kikwazo hawataweza tena...

refer, maandamano ya TL baada ya uchaguzi....kile ni kipimo tosha kuwa CCM bado haijachokwa kama tunavyofikiri... Arab spring haikufanywa na wanasiasa, Mapinduzi ya sudan dhidi ya Bashiru hayakufanywa na wanasiasa...ni wananchi wenyewe walipoamua baada ya majaribio kadhaa ya wanasiasa kushindwa...

Fanya uchunguzi wa kina mtaani kwanini watanzania hawajaamua kujisacrifice kuitoa CCM....na hata uwaite barabarani hawaji na wakisikia mabomu wanajifungia ndani...fanya simple research isiyo na ushabiki kitaa...
 
Ungekuwa neutral tungekuamini, siku hizi unafuata upepo unakoelekea na wewe unakwenda huko huko. Umeona watu wamekukandia maandiko yako mawili yaliyopita umejirejesha uonekane unaijua haki. Kaa hivyo hivyo ushushe heshima yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…