Rais Samia anasimamia fedha za Serikali vizuri kuliko Hayati Magufuli

Rais Samia anasimamia fedha za Serikali vizuri kuliko Hayati Magufuli

This is bool shit sijui this sijui that what the hell basi nenda kaishi kwake ili uendele kumsifia mnaboa achwe mfu alale pema na mama wawatu aishi Kwa Amani hii Nini hutopata uongozi Kwa kusifia nikwakufanya juhudi katika kazi
 
Kama umemsikiliza vizuri Utouh alipokuwa anaongea juzi, ni kwamba ingawa katika Halmashauri umetokea ubadhirifu mkubwa na labda wizi, lakini kwa ujumla, Serikali Kuu imeweza kupunguza ubadhirifu katika mwaka huu wa fedha kuliko mwaka jana, kufuatana na ripoti ya CAG Kichere.

Swali tu ni kwamba ni nani alikuwa rais katika ile Financial year iliyopita?

Kwa maana hiyo,kuhusu Financial ripoti ya CAG ya mwaka huu,Rais Samia anastahili pongezi,na sio kama ilivyo sasa watu wanatetemeka kwa hasira.
Unafiki utakutoa roho wewe, mchumia tumbo.
 
Ukweli ni kwamba wizi wa pesa ya umma ulipungua sana awamu ya 5 kwa watendaji wa kawaida, lakini kulikuwa na wizi wa kutisha kiasi ambacho haijawahi kutokea kwa watu walioruhusiwa kupora:

Trilioni 1.5.
Plea bargain - billions.
Maduka ya kubadilisha fedha - billions.
Unyang'anyi uliofanywa na Makonda na Sabaya - mamia ya mamilioni.

Awamu ya 5 uporaji wa pesa ulifanywa tu watu ambao yeye aliwaruhusu wapore watakavyo. Alizuia wengine kuiba ili wanaoiba wabakie wachache lakini wapore kwa kiasi kikubwa.
 
Ni kweli mkuu anasimamia ili waibe vizuri.

Hongereni sana.

Kasimamia vizuri upotevu wa 1.7 trilioni kwenye SGR.

1.2 isiyoidhinishwa na Bunge Wala matumizi yake kujulikana.

Ongezeko la dola milioni 46 kwenye invoice ya ndege.
 
Hivi hatuwezi kumsifu Samia bila kumpondea mtangulizi wake?.
P
Huwezi kusema viatu hivi ni bora zaidi kama hakuna vilivyo hafifu. Wala huwezi kusema kuwa mwaka huu nimepiga hatua bila kujua mwakajana na mwakajuzi ulikuwaje.

Hata wanaposema kuwa mwaka huu ufaulu umeongezeka, si lazima wataje ufaulu wa mwaka uliopita ulikuwaje?

Inatakiwa itajwe Serikali au utawala, lakini kwa bahati mbaya serikali ya awamu ya 5 ilijitambulisha zaidi kama Serikali ya mtu mmoja, ndiyo maana iwe jema au baya anabebeshwa mtu badala ya Serikali. Na udhaifu ule wa kuona Serikali ni mtu mmoja, wapo wanaoeundeleza mpaka sasa. Ndiyo hao utawasikia kuwa eti Rais Samia ametoa bilioni kadhaa kujenga barabara, ni ujinga na ulimbukeni uliokuwa umeanzishwa wakati wa awamu ya 5, na sasa kuna wajinga na wanafiki wanauendeleza. Serikali ndiyo inayotoa pesa, siyo Rais. Na pesa inayotolewa siyo ya Serikali bali ya umma/wananchi.
 
Kama umemsikiliza vizuri Utouh alipokuwa anaongea juzi, ni kwamba ingawa katika Halmashauri umetokea ubadhirifu mkubwa na labda wizi, lakini kwa ujumla, Serikali Kuu imeweza kupunguza ubadhirifu katika mwaka huu wa fedha kuliko mwaka jana, kufuatana na ripoti ya CAG Kichere.

Swali tu ni kwamba ni nani alikuwa rais katika ile Financial year iliyopita?

Kwa maana hiyo,kuhusu Financial ripoti ya CAG ya mwaka huu,Rais Samia anastahili pongezi,na sio kama ilivyo sasa watu wanatetemeka kwa hasira.
Kwa vichekesho zaidi pogia simu pappy hatonn
 
Bora ungesema Raisi Samia amejifunza vizuri kutoka kwa Hayati Raisi J.P.M kuhusu usimamizi mzuri wa Fedha za Mtanzania.

Punguza shutumu zisizo na miguu wala kichwa. Nchi hii ni yetu. Usimezeshwe chuki na maharamia.
Usimamizi upi mzuri aliokuwa nao.
 
Back
Top Bottom