Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 7,799
- 14,215
Habari zenu ndugu zangu,
Wakuu wenzangu, wakati Rais Samia anaingia madarakani wengi tulimshauri aache kufanya maamuzi kwa kufuata mashinikizo ya watu ndani ya mitandao ya kijamii. Kama ilivyo kawaida ya ushauri ni mshauriwa kufuata au kuacha kufuata anachoshauriwa.
Raisi akaamua kupuuza ushauri wetu kwa kuanza timua timua ya viongozi wote waliokuwa wanashutumiwa na wapinzani humu mitandaoni bila kujali uchapaji wao wa kazi. Lakini raisi hakuishia hapo katika kutaka kuwafurahisha wapinzani na wanaolalamika mitandaoni, Rais akauonesha umma wa Watanzania na dunia kwa ujumla kwamba kuna watu walikuwa wameonewa na kukamatwa bila makosa yoyote chini ya utawala wa awamu ya tano na hata ya nne pia. Akaamua kutengeneza mazingira ambayo yamewasaidia wengi kutoka ndani ya vifungo vyao walivyokuwa wamefungwa kutokana na kesi mbalimbali.
Kati ya wafungwa hao walioachiwa kutokana na mipango au jitihada za mama ni wale mashehe wa uamsho, na yule muhindi ambao walikamatwa wakati wa utawala wa JK. Pia yupo kijana anaeitwa Mdude ambae alikamatwa wakati wa utawala wa JPM. Wote waliokamatwa wameonesha shukran zao kwa raisi kutokana na jitihada alizofanya mpaka kuachiwa kwao, lakini huyu Mdude yeye ameonekana kutoshukuru kwa lolote, anachofanya yeye ni kutafuta njia ya kumchafua raisi kana kwamba haoni jitihada zake katika kuachiwa kwake.
Je, Mdude hafahamu kwamba bila mama kuweka jitihada zake na huruma wake mpaka leo angekuwa bado ananyea debe kama alivyokuwa ananyea wakati wa utawala uliyopita? Hata hivyo simlaumu Mdude bali hii itumike kama fundisho kwa mama. Asiwe anafanya mambo kwa kufuata mashinikizo ya mitandao, bila shaka Rais Samia ashapata jibu kwamba ni kwanini watu aina ya kina Mdude waliwekwa ndani na hawakuachiwa hivi hivi. Wakati mungine mtu unaweza kuwa sio katili, lakini watu wakakufanya ukawa katili.
Rais Samia sasa inambidi avumilie maana ni kama vile kinyago amekichonga mwenyewe afu leo kinamtafuna pia ajue siku zote shukrani ya punda ni mateke.
Asanteni.