Rais Samia anavuna alichopanda, hana budi kuvumilia

Rais Samia anavuna alichopanda, hana budi kuvumilia

Inawezekana ww ukawa na upeo wa kisiasa zaidi ya Lisu ambae aliifanya siasa ni uadui mkubwa mpaka akaamua kushirikiana na wazungu katika swala la madini, lakini pia baada ya kuona swala la madini halina madhara kwa nchi akaamua kuwaomba hao hao wazungu watunyime misaada na kutuwekea vikwazo bila kujali kwamba vile vikwazo vingewaumiza zaidi raia wa chini wakiwemo ndugu zake, rafiki zake na wanachama wake.
We kaza shingo yako,utakufa kwa kihoro ukimuona akisalimiana na Samia siku hiyo.
 
Hizi Id za wakati wa kampeni zilianzishwa na ccm kundi la kina Polepole na Bashiru, ili kupambana na kuchafua mijadala kipindi cha dhalimu. Id hizi zilikuwa za wanufaika wa utawala wa yule kiongozi muovu,kwa sasa mlichokuwa mnapata kipindi kile hamkipati baada ya dhalimu mwenzenu kwenda motoni. Mnachofanya sasa ni kucheza na akili ya mama ili kumchanganya afanye kama dhalimu.

Mlilipwa kwa kutegemea uovu, msitegemee huyo mama kurudi kwenye uovu ili awape ulaji tena. Kama ni kuteka watu na kuwaua mmefanya sana, na kama miradi yenu haikuwa imekamilika ndio basi tena. Sasa hivi nyie na lile genge lenu la watu waovu akina Polepole, Bashiru, Makonda nk mmekuwa wapole maana hamna njia ya kuwapatia tena vipato haramu. Polepole na kile kipindi chake cha kusaka sifa na ulaji, kimefutika baada ya utawala wa mtu muovu kuisha ghafla.
Wewe ni mtu mzima lkn inaonekana akili yako imemezwa na mahaba ya chama. Mdude ameshamwambia mama kuwa atatumia wembe ule ule aliotumia kumnyolea mtangulizi wake kumnyoa mama. Kwa ujumbe huu wa Mdude inaonesha kabisa Mdude haoni tofauti ya utawala wa mama na wa mtangulizi wake, lkn pia sio Mdude peke yake mwenye mawazo ya aina hii hata Lisu kaishaanza kumfananisha mama na mtangulizi wake. Sasa kuniambia mimi nisitegemee mama kurudi kwenye uovu huku viongozi wako including Lisu washaanza kumuona mama anaelekea kwenye uovu ni kukosa hoja. Kati ya mimi na Mdude ni nani ambae anategemea mama atakuwa muovu kama mtangulizi wake?
 
Hivyo kumbe Mdude alishikiliwa na JPM na kaachiliwa na Samia?

Eleweni kuea wananchi tumeamka. Hatutaki kuendelea kubambikiziwa kesi, hatutaki dhuluma, hatutaki kubebeshwa mizigo ya kodi ya wengine, tunataka mihimili ya utawala iliyo na huru kamili, tunataka usawa, tunataka uwajibikaji, tunataka mawazo yetu kusikilizwa nk.

Haya majibu ya matakwa hayo ni katiba mpya. Mwambieni mama wananchi wanataka katiba yao kuondokana na adha kama hizo.
Katiba inaweza kutungwa na watu wakaivunja vile vile kama zinavyovunjwa katiba zingine. Mbowe alivunja katiba ya chama chake mwenyew kwa kumruhusu Lowasa kugombea nafasi ya uraisi bila kufuata katiba wala taratibu za chama. Ebu fikiria mtu anakuja kwenye chama wiki hii wiki ijayo mwenyekiti anapokea hela na kumruhusu kugombea uraisi huku waliokijenga chama kwa jasho na damu kama dr Slaa na msomi prof Safari wakiandaliwa kuja kumdekia barabara huyo Lowasa. Slaa alipoomba katiba na utaratibu wa kumpata mgombea ufatwe aliitwa msaliti na mtu mwenye tamaa. Sasa mtu wa aina hii ya Mbowe akichaguliwa kuwa raisi anawezaje kushindwa kuvunja katiba na sheria kama alivyovunja kwa Lowasa na ukizingatia kipindi hicho yeye ndo atakuwa amiri jeshi mkuu!
 
Wewe mbilikimo tulia.
Yaani unataka Mdude amshukuru Rais Samia Suluhu kwa lipi?
Mambo yenu ya kutukuzana mliyaanzisha kwa Magufuli mpaka mkaanza kumwita Mungu yaishie hukohuko.
 
Wewe ni mtu mzima lkn inaonekana akili yako imemezwa na mahaba ya chama. Mdude ameshamwambia mama kuwa atatumia wembe ule ule aliotumia kumnyolea mtangulizi wake kumnyoa mama. Kwa ujumbe huu wa Mdude inaonesha kabisa Mdude haoni tofauti ya utawala wa mama na wa mtangulizi wake, lkn pia sio Mdude peke yake mwenye mawazo ya aina hii hata Lisu kaishaanza kumfananisha mama na mtangulizi wake. Sasa kuniambia mimi nisitegemee mama kurudi kwenye uovu huku viongozi wako including Lisu washaanza kumuona mama anaelekea kwenye uovu ni kukosa hoja. Kati ya mimi na Mdude ni nani ambae anategemea mama atakuwa muovu kama mtangulizi wake?

Tofautisha uovu na kuvunja sheria. Nyie mlikuwa mnafaidika na uovu wa magu ndio maana saa hii mnalilia. Alichosema Mdude ni mikwara ya kisiasa tu wala haina madhara yoyote. Huyo mama ungemshauri awakamate waliojiunganishia bomba la mafuta ndio kuna madhara, sio vijembe vya kisiasa. Tafuta kazi ya halali, hiyo ya kuteka na kuua watu haipo tena boss.
 
Maajabu hivi ni mwana CCM gani hakulionja joto la Magu? Nani hakuumia moyo juu ya yaliyokuwa yakifanyika,ni nani kati yenu alipona juu ya udharirishaji uliokuwa ukifanyika juu ya wana wa nchi hii? na vibaraka wapenda vyeo walevi wa madaraka akina sabaya,makonda and so on.

Kwa hali hiyo mnamtaka huyu mama nae aige ujinga huo ili iweje? ni dhihaka,matusi mangapi yametamkwa na wana CCM Katika kipindi hicho bila kukemewa na mtu yeyote! mmesahau hadi mlikuwa mnapendekeza akina nani wana faa kuuwawa,kuna kosa kubwa kama mtu binafsi kupitisha hukumu ya kifo juu ya raia mwenzake.

Enyi CCM Jaza Tumbo kweli mnamshauri huyu mama atende sawasawa na matendo ya mwendazake? Je, watoto wake wanayo mioyo ya kuhimili machungu wanayoyapata sasa watoto wa mwendazake juu ya matendo ya baba yao?

kWA HURUMA KABISA, namshauri mama asije akakubari ushauri wa kipumbavu kama huu kabla hajatekeleza hayo aitizame mioyo ya kizazi chake kama inaweza kuhimili mateso na moto utakao tokana na matendo yake mabaya akiwa jumba jeupe maana hapo yeye ni mpangaji tu,
Ngija ajifanye ana huruma sana. Cha m,uhumu hata angejipa muda kufanya uchunguzi lakini nhuruma yake na ni yakujitafutia umaarufu itamcost tena sio mbali. Atulie sasa afuatilie kujua ukweli kwanza hata kama kuawaachia afanye akijua ukweli!
 
Katiba inaweza kutungwa na watu wakaivunja vile vile kama zinavyovunjwa katiba zingine. Mbowe alivunja katiba ya chama chake mwenyew kwa kumruhusu Lowasa kugombea nafasi ya uraisi bila kufuata katiba wala taratibu za chama. Ebu fikiria mtu anakuja kwenye chama wiki hii wiki ijayo mwenyekiti anapokea hela na kumruhusu kugombea uraisi huku waliokijenga chama kwa jasho na damu kama dr Slaa na msomi prof Safari wakiandaliwa kuja kumdekia barabara huyo Lowasa. Slaa alipoomba katiba na utaratibu wa kumpata mgombea ufatwe aliitwa msaliti na mtu mwenye tamaa. Sasa mtu wa aina hii ya Mbowe akichaguliwa kuwa raisi anawezaje kushindwa kuvunja katiba na sheria kama alivyovunja kwa Lowasa na ukizingatia kipindi hicho yeye ndo atakuwa amiri jeshi mkuu!

Una maana JPM alikuwa mtawala wa hovyo mvunja katiba sugu? What a legacy?

Sasa kawaambie waliokutuma kuwa wenye nchi sasa wanataka katiba itakayo kuwa na namna za wazi za kuwafurusha forth with watawala dhalimu wavunja katiba sugu kama JPM bila kuwapa hata siku moja zaidi ofisini.

Hii nchi imechezewa sana!

Habari ndiyo hiyo.
 
Tofautisha uovu na kuvunja sheria. Nyie mlikuwa mnafaidika na uovu wa magu ndio maana saa hii mnalilia. Alichosema Mdude ni mikwara ya kisiasa tu wala haina madhara yoyote. Huyo mama ungemshauri awakamate waliojiunganishia bomba la mafuta ndio kuna madhara, sio vijembe vya kisiasa. Tafuta kazi ya halali, hiyo ya kuteka na kuua watu haipo tena boss.
Uovu gani alioufanyia wa kuwanunulia ndege au\? wa kuwajengea madaraja? au kuwapelekea umeme kwa Bibi zenu ambapo nyie wenyewe hamkanyagi? au kwa kuwasomesha watoto wa watanzania bure. Tusubiri miaka miwili tu mtapata majibu yake.
 
Kaburi Pieter Botha wa Afrika kusini alifanya yote hayo tena kwa ubora mkubwa, lakini alipingwa kwa uovu wake, ww unataja hivyo vindege ndio unadhani ni pazia la kufunika uovu wake? Watoto wa Tanzania walisomeshwa bure kwa kodi za watanzania sio mshahara maana hata sasa wanasoma bure na hakuna uovu. Miaka miwili ipi na wakati mama analia uchumi umeanguka?
 
Chama cha siasa kikishindwa uchaguzi mara 3 kinageuka kuwa cha kigaidi.

Ndiko hii saccos chadema inakoelekea
2183704_IMG_1183.jpg
 
sio kila wakati dola lazima ikwambie kila kitu..

Ni ngumu dola kukwambia kwanini Uamsho walikuwa jela...sia ajabu ukifunuliwa leo kwa siri ukaonyeshwa harakati zao ungeweza kuandamana na kutaka adhabu kali dhidi yao...
Sio kwa dola hii chini ya CCM ambayo kwa yenyewe hivyo na hapo ilipo ina - struggle ku - survive kwa mbinu za ugaidi wa kidola (state sponsored terrorism)...

Sisi sote (ispokuwa wewe, labda) tunajua kuwa hii siyo dola iliyobena maslahi ya nchi hii na wananchi wake....

Ni dola ya watu wachache iliyoko hapo kwa ajili ya watu hao wachache. Dola ya namna hii haiwezi kufanya hivi unavyofikiri na kudhani. Dola ya namna hii, kila critic & criticism kwayo utakuwa gaidi tu...

Tuna akili, sio wajinga wa kiwango hiki cha kudanganywa. Tunaelewa kila kitu. Tunaelewa kila hadaa...
 
Una maana JPM alikuwa mtawala wa hovyo mvunja katiba sugu? What a legacy?

Sasa kawaambie waliokutuma kuwa wenye nchi sasa wanataka katiba itakayo kuwa na namna za wazi za kuwafurusha forth with watawala dhalimu wavunja katiba sugu kama JPM bila kuwapa hata siku moja zaidi ofisini.

Hii nchi imechezewa sana!

Habari ndiyo hiyo.
Kijana kama ww kufanywa puppet na mwenyekiti wa Chadema mwenye elimu ya form 4, ni aibu kwako na kwa wazazi wako.
 
Kweli mkuu, just imagine mtu kama Mdude badala ya kumshukuru raisi kwa kusimamia haki hadi yeye akatoka eti anaanza kumtengenezea na yeye beef mwisho wa siku mama kama walivyo binadam wengine uzalendo utamshinda na kuanza kutumia madaraka yake kumwadhibu yeye Mdude na wengine wa aina yake.

JK alikuwa mvumilivu na mwenye huruma lkn watu walimlazimisha kutumia madaraka yake matokeo yake watu wakaanza kulalamika sijui kina Mwangosi wameng'olewa kucha, sijui aliuwa watu katika bomu la soweto kule Arusha nk.
Mdude alitoka kwa huruma au kesi ilikosa USHAHIDI WA KUMTIA HATIANI,?

MAKOSA YA KUBAMBIKA (,KUSINGIZIA,, UONEVU, KUKOMOA)

Kwa vile SHERIA zetu ni mbovu, hata kama Mtuhumiwa ataonekana hana kesi ya kujibu, hana HAKI YA KUDAI FIDIA KWA USUMBUFU, MATESO, HASARA YA MALI NA MUDA ALIOPOTEZA KWA KUWEKWA NDANI.

KATIBA MPYA YENYE KUTOA HAKI KWA WOTE INAHITAJIKA SANA KWA SASA KULIKO WAKATI MWINGINE.

"WATANZANIA WANYONGE HAWA"
 
Habari zenu ndugu zangu,

Wakuu wenzangu, wakati Rais Samia anaingia madarakani wengi tulimshauri aache kufanya maamuzi kwa kufuata mashinikizo ya watu ndani ya mitandao ya kijamii. Kama ilivyo kawaida ya ushauri ni mshauriwa kufuata au kuacha kufuata anachoshauriwa.

Raisi akaamua kupuuza ushauri wetu kwa kuanza timua timua ya viongozi wote waliokuwa wanashutumiwa na wapinzani humu mitandaoni bila kujali uchapaji wao wa kazi. Lakini raisi hakuishia hapo katika kutaka kuwafurahisha wapinzani na wanaolalamika mitandaoni, Rais akauonesha umma wa Watanzania na dunia kwa ujumla kwamba kuna watu walikuwa wameonewa na kukamatwa bila makosa yoyote chini ya utawala wa awamu ya tano na hata ya nne pia. Akaamua kutengeneza mazingira ambayo yamewasaidia wengi kutoka ndani ya vifungo vyao walivyokuwa wamefungwa kutokana na kesi mbalimbali.

Kati ya wafungwa hao walioachiwa kutokana na mipango au jitihada za mama ni wale mashehe wa uamsho, na yule muhindi ambao walikamatwa wakati wa utawala wa JK. Pia yupo kijana anaeitwa Mdude ambae alikamatwa wakati wa utawala wa JPM. Wote waliokamatwa wameonesha shukran zao kwa raisi kutokana na jitihada alizofanya mpaka kuachiwa kwao, lakini huyu Mdude yeye ameonekana kutoshukuru kwa lolote, anachofanya yeye ni kutafuta njia ya kumchafua raisi kana kwamba haoni jitihada zake katika kuachiwa kwake.

Je, Mdude hafahamu kwamba bila mama kuweka jitihada zake na huruma wake mpaka leo angekuwa bado ananyea debe kama alivyokuwa ananyea wakati wa utawala uliyopita? Hata hivyo simlaumu Mdude bali hii itumike kama fundisho kwa mama. Asiwe anafanya mambo kwa kufuata mashinikizo ya mitandao, bila shaka Rais Samia ashapata jibu kwamba ni kwanini watu aina ya kina Mdude waliwekwa ndani na hawakuachiwa hivi hivi. Wakati mungine mtu unaweza kuwa sio katili, lakini watu wakakufanya ukawa katili.

Rais Samia sasa inambidi avumilie maana ni kama vile kinyago amekichonga mwenyewe afu leo kinamtafuna pia ajue siku zote shukrani ya punda ni mateke.

Asanteni.
haki haihitaji huruma ya m2 katiba mpya ni suluhisho la ujinga wote huu wa kuoneana
 
Wapinzani walitumiwa na JK kumchafua Lowasa, upinzani wetu ujinga mtupu
Yani upinzan wa tanzania ni wa hovyo sana, wanashindwa hata na wapinzani wa nchi kama Malawi au Zimbabwe wanajua kusimamia agenda na misimamo yao ya chama.
 
Mdude alitoka kwa huruma au kesi ilikosa USHAHIDI WA KUMTIA HATIANI,?

MAKOSA YA KUBAMBIKA (,KUSINGIZIA,, UONEVU, KUKOMOA)

Kwa vile SHERIA zetu ni mbovu, hata kama Mtuhumiwa ataonekana hana kesi ya kujibu, hana HAKI YA KUDAI FIDIA KWA USUMBUFU, MATESO, HASARA YA MALI NA MUDA ALIOPOTEZA KWA KUWEKWA NDANI.

KATIBA MPYA YENYE KUTOA HAKI KWA WOTE INAHITAJIKA SANA KWA SASA KULIKO WAKATI MWINGINE.

"WATANZANIA WANYONGE HAWA"
Masheikh wa uamsho walikaa jela zaidi ya miaka 9. Walikaa miaka 3 chini ya utawala wa Kikwete na miaka 6 chini ya utawala wa Magufuli, lakini wamekuja kutoka katika miezi 3 tu ya utawala wa mama. Mdude ana zaidi mwaka au miaka. Alikaa jela zaidi ya mwaka au miaka chini ya utawala wa Magufuli, lakini na yeye amekuja kutoka katika kipindi cha miezi hiyo hiyo 3 tu ya mama. Haihitaji shule au akili nyingi kujua ni kwann Mdude hakuweza kushinda kesi miaka yote hiyo aliyokaa jela kabla ya mama kuingia madarakan, lkn ameweza kushinda katika miezi mitatu tu ya mama kuingia madarakan tena baada ya mama kumbadilisha mwanasheria mkuu wa serikali. Haihitaji shule au akili kujua ni kwanini mama alimbadilisha mwanasheria mkuu wa serikali na baada ya hapo Mdude akaweza kushinda kesi na pia masheikh kuachiwa. Najua hauwezi kuongea au kuandika kinyume na yale ambayo mwenyekiti wako wa chama anataka uyaandike hapa JF maana ukiandika ukweli hatokulipa ujira wako, lkn nina imani moyoni unaujua ukweli na nafsi inakusuta mwenyew kwa haya unayoandika hapa. Namalizia kwa huu msemo "Mnyoge mnyongeni lakini haki yake mpeni" Kama mama asingekuwa raisi au asingebadilisha mwanasheria mkuu wa serikali nina imani Mdude na masheikh wa uamsho wangekuwa bado wananyea debe kwa kupigwa kulenda na kuambiwa kwamba ushahidi bado haujakamilika kwahiyo waendelee kuzuiliwa mpaka pale ushahidi utapopatikana.
 
haki haihitaji huruma ya m2 katiba mpya ni suluhisho la ujinga wote huu wa kuoneana
Unajidhalilisha sana dada yang kwa kukubali kufanywa puppet na wanasiasa wachovu kama Lisu, Zito, Mbowe na wengine wa aina yao. Nikikwambia uniandikie vifungu vitano tu vya katiba ambavyo ww na hao waliokutuma mnaona havifai hautoweza. Kilichofanyika ni kukukaririsha tu kwamba katiba haifai lkn kiuhalisia hauna unalolijua kuhusu hiyo katiba isiyofaa. Aibu sana kuona msichana kama ww njaa yako imekufanya uuze utu wako. Na tumegundua kwamb wapinzani wanapigia chapuo swala la katiba ili waje wapige pesa katika kila kikao watachokuwa wanakaa kwa ajili ya kuitengeneza katiba.
 
Wakati mungine mtu unaweza kuwa sio katili, lakini watu wakakufanya ukawa katili

(Hapa nimekuelewa sana) Na ndio wengi walikua hawamuelewi Magu. Hawa wanaojiita wapinzani wanahitaji style ya magu ili mambo yaende.

Wee kuna kiumbe mgumu kama binadamu. Ukimpiga anasema umemuonea, ukimuacha anasema umemuogopa. Aliyemuumba tu ndiye anayemjua.
 
Back
Top Bottom