Rais Samia anavuna alichopanda, hana budi kuvumilia

Kwa hiyo tuseme huyu Mama (Samia Suluhu) anafanya yale yale ya Mwendazake John P. Magufuli?

Kwamba, mahakama haikuzingatia sheria katika kutoa hukumu ya Mdude Chadema isipokuwa ilifuata maagizo ya Rais na kwa hiyo alitoka kwa "hisani ya Rais Samia Suluhu?"

Kumbe ndo maana mnamwandama hivi kiasi cha kutaka kumfanya kuwa mtumwa wa "hisani ya Rais Samoa" siyo?

Tukisema kuwa Rais Samia aweza kuwa Magufuli wa kike msishangae na ndiyo maana Mdude Chadema anasema "...wembe uliomnyoa Magufuli ndiyo huohuo utamnyoa na huyu mama!"

Kiukweli, kama mambo ndo yako hivi, basi Mimi naunga mkono hoja, wembe uleule uliomnyoa yule basi umnyoe na huyu.
Ama kweli "usitukane mamba kabla haujavuka mto". Waliopanga kumpa mwendawazimu wembe amnyoe adui yao, ndio hao hao leo wanalalamika kunyolewa wao!!
 
Habari zenu ndugu zangu,

Wakuu wenzangu, wakati Rais Samia anaingia madarakani wengi tulimshauri aache kufanya maamuzi kwa kufuata mashinikizo ya watu ndani ya mitandao ya kijamii. Kama ilivyo kawaida ya ushauri ni mshauriwa kufuata au kuacha kufuata anachoshauriwa.

Raisi akaamua kupuuza ushauri wetu kwa kuanza timua timua ya viongozi wote waliokuwa wanashutumiwa na wapinzani humu mitandaoni bila kujali uchapaji wao wa kazi. Lakini raisi hakuishia hapo katika kutaka kuwafurahisha wapinzani na wanaolalamika mitandaoni, Rais akauonesha umma wa Watanzania na dunia kwa ujumla kwamba kuna watu walikuwa wameonewa na kukamatwa bila makosa yoyote chini ya utawala wa awamu ya tano na hata ya nne pia. Akaamua kutengeneza mazingira ambayo yamewasaidia wengi kutoka ndani ya vifungo vyao walivyokuwa wamefungwa kutokana na kesi mbalimbali.

Kati ya wafungwa hao walioachiwa kutokana na mipango au jitihada za mama ni wale mashehe wa uamsho, na yule muhindi ambao walikamatwa wakati wa utawala wa JK. Pia yupo kijana anaeitwa Mdude ambae alikamatwa wakati wa utawala wa JPM. Wote waliokamatwa wameonesha shukran zao kwa raisi kutokana na jitihada alizofanya mpaka kuachiwa kwao, lakini huyu Mdude yeye ameonekana kutoshukuru kwa lolote, anachofanya yeye ni kutafuta njia ya kumchafua raisi kana kwamba haoni jitihada zake katika kuachiwa kwake.

Je, Mdude hafahamu kwamba bila mama kuweka jitihada zake na huruma wake mpaka leo angekuwa bado ananyea debe kama alivyokuwa ananyea wakati wa utawala uliyopita? Hata hivyo simlaumu Mdude bali hii itumike kama fundisho kwa mama. Asiwe anafanya mambo kwa kufuata mashinikizo ya mitandao, bila shaka Rais Samia ashapata jibu kwamba ni kwanini watu aina ya kina Mdude waliwekwa ndani na hawakuachiwa hivi hivi. Wakati mungine mtu unaweza kuwa sio katili, lakini watu wakakufanya ukawa katili.

Rais Samia sasa inambidi avumilie maana ni kama vile kinyago amekichonga mwenyewe afu leo kinamtafuna pia ajue siku zote shukrani ya punda ni mateke.

Asanteni.
Too low.
 
tunataka katiba mpya
 
Wakati mungine mtu unaweza kuwa sio katili, lakini watu wakakufanya ukawa katili

(Hapa nimekuelewa sana) Na ndio wengi walikua hawamuelewi Magu. Hawa wanaojiita wapinzani wanahitaji style ya magu ili mambo yaende.
Uongozi unataka ngozi ngumu kama una ngozi nyepesi haukufai
 
Sauti ya watu sauti ya Mungu usipowqsikiliza ni lazima uanguke
 
Kama mnaamini hivyo, kulikuwa na maana gani ya Mdude kuongea yale aliyoongea? Je Mdude hajui wala haoni kama mama hakurupuki wala hatishiki kama ulivyoandika hapa? Je kama anajua ni kwanini kajaribu kumtishia kumnyoa kwa wembe alotumia kumnyolea mtangulizi wake? Naomba twende hoja kwa hoja ndugu yang.
Mtu matured na civilized anyimwi usingizi na kelele za watu wasio na dola.
Wapiga kelele wapo duniani nzima.
 
Andiko lako linatupa ujumbe kwamba wanaofungwa jela na tawala hizi za kiimla ni kwamba kimsingi sio wakosaji mbele ya sheria ila ni kutaka kuwakomoa na pia kufanya uwe mfano kusudi wengine waogope. Ndivyo nilivyo kuelewa.
 
Mtu matured na civilized anyimwi usingizi na kelele za watu wasio na dola.
Wapiga kelele wapo duniani nzima.
Wewe unafikiri akina Gaddafi, Saddam, Mobutu, Amin, Bokassa, Doe, Mugabe, Siad Barre wao hawakuwa na dola.!!

Mkiwa mnakuja humu, msiwe mnalewa kwanza viroba, jua dunia hii inakotoka. Hata Magufuli alikuwa na dola lakini leo kabaki tu kwenye hadithi kama ya sungura alivyomdanganya tembo akakanyaga moto.
 
Viroba vipo kwani
 
Back
Top Bottom