Rais Samia anavuna alichopanda, hana budi kuvumilia

Absolutely, YES...

Hakuna matusi wala uchafu kwenye kauli za Mdude. Wana ishu zao hawa...

Wanasiasa watawala hawapendi lugha anayotumia Mdude kuwasema na kuwakosoa. Na MDOMO au MANENO yana nguvu kubwa sana kubadilisha mambo/hali kisiasa kuliko risasi au polisi au jeshi au UWT...!

Kwa hiyo harakati hizi ni kwa ajili kuona Mdude na wengine wenye ujasiri wa kutumia midomo yao kukosoa watawala kwa lugha Kali, wanaacha na kukoma mara moja...

Lakini hawataweza kama ambavyo watawala waliopita hawakuweza...!!!
 
Jamii forums imeingiliwa na watu wa ajabu kweli kweli! Hivi Mdude alitolewa na Mama au alishinda?

Hao Mashekh wa uamsho Kama wlikuwa na kosa, kwanini hawakufunguliwa mashtaka kwa miaka 8?

Mleta mada wewe ni wa hovyo Sana. Samahani lakini.

scene iliopo nyuma iskilize tu, haswa haya mashehe, achana n huyu wa kumnyoa mbowe maaana ni fundi simu
 
Yeye pia ni mtu mzima, za kuambiwa achanganye na zake.
 
Two wrongs don't make a right. Rais asisamehe watu kwa vile baadhi yao wanaweza kumtukana? Magufuli was a dictator na hatutaki Tanzania irudi huko. Kama mnam-miss sana mfufueni 🤣
 
Ume-personalise governance, kisha ukasema uongo. Mdude wa Chadema ameshinda kesi mahakamani, hakusamehewa na Rais SSH. Ukisimamia hoja yako (uongo), tafsiri yake ni kuwa Rais SSH aliingilia uhuru wa mahakama kufanya maamuzi ya kumuachia Mdude. Jambo hili siyo kweli. Tafadhali jielimishe kabla ya kuandika kwa umma.
 
Mama kama unasoma huku mtandaoni,. Tunakuomba usiwachekee hawo watu wanaojiita wapinzani hawakawii kumwaga damu za watanzania ,. Tunakupenda sana ila hichi kikundi cha chadema wanataka kukudhalilisha mama wakazie
Kama ni mechi basi mama kaanza kutoa boko kipindi cha kwanza.
 

Hutaki mama afanye maamuzi kupitia mitandao, lakini ww pia unatumia mitandao hiyo hiyo kutaka mama afuate utakacho! Hii ndio akili ya kukimbizia mwenge. Hili suala la Mdude naona umelinzishia nyuzi kibao, na kote huko umepewa ukweli wako. Achana na hili jambo liko nje ya uwezo wako. Zile zama zenu za watu wasiojulikana zimepita na dhalimu, sasa hivi tafuta kazi ya halali boss.
 
Watu walioko karibu na mama wamtafutie series moja inaitwa TYRANT. Viongozi wanaokuja kutawala baada ya utawala unaosemekana kuwa wa kimabavu wana mengi ya kujifunza kupitia ile series.
 

Naona una msongo wa mawazo mpaka unaandika na uongo wa kijinga. Umeshapanick ww.
 
We ni kichaa, mdude aliachiwa na mama au na mahakama?
 
We huwezi kuwa mwansiasa kamwe.huijui siasa wewe hainaga adui Wa kudumu.
 

Hizi Id za wakati wa kampeni zilianzishwa na ccm kundi la kina Polepole na Bashiru, ili kupambana na kuchafua mijadala kipindi cha dhalimu. Id hizi zilikuwa za wanufaika wa utawala wa yule kiongozi muovu,kwa sasa mlichokuwa mnapata kipindi kile hamkipati baada ya dhalimu mwenzenu kwenda motoni. Mnachofanya sasa ni kucheza na akili ya mama ili kumchanganya afanye kama dhalimu.

Mlilipwa kwa kutegemea uovu, msitegemee huyo mama kurudi kwenye uovu ili awape ulaji tena. Kama ni kuteka watu na kuwaua mmefanya sana, na kama miradi yenu haikuwa imekamilika ndio basi tena. Sasa hivi nyie na lile genge lenu la watu waovu akina Polepole, Bashiru, Makonda nk mmekuwa wapole maana hamna njia ya kuwapatia tena vipato haramu. Polepole na kile kipindi chake cha kusaka sifa na ulaji, kimefutika baada ya utawala wa mtu muovu kuisha ghafla.
 

Hivyo kumbe Mdude alishikiliwa na JPM na kaachiliwa na Samia?

Eleweni kuea wananchi tumeamka. Hatutaki kuendelea kubambikiziwa kesi, hatutaki dhuluma, hatutaki kubebeshwa mizigo ya kodi ya wengine, tunataka mihimili ya utawala iliyo na huru kamili, tunataka usawa, tunataka uwajibikaji, tunataka mawazo yetu kusikilizwa nk.

Haya majibu ya matakwa hayo ni katiba mpya. Mwambieni mama wananchi wanataka katiba yao kuondokana na adha kama hizo.
 

sio kila wakati dola lazima ikwambie kila kitu..

Ni ngumu dola kukwambia kwanini Uamsho walikuwa jela...sia ajabu ukifunuliwa leo kwa siri ukaonyeshwa harakati zao ungeweza kuandamana na kutaka adhabu kali dhidi yao...
 
We huwezi kuwa mwansiasa kamwe.huijui siasa wewe hainaga adui Wa kudumu.
Inawezekana ww ukawa na upeo wa kisiasa zaidi ya Lisu ambae aliifanya siasa ni uadui mkubwa mpaka akaamua kushirikiana na wazungu katika swala la madini, lakini pia baada ya kuona swala la madini halina madhara kwa nchi akaamua kuwaomba hao hao wazungu watunyime misaada na kutuwekea vikwazo bila kujali kwamba vile vikwazo vingewaumiza zaidi raia wa chini wakiwemo ndugu zake, rafiki zake na wanachama wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…