Rais Samia anavuna alichopanda, hana budi kuvumilia

We kaza shingo yako,utakufa kwa kihoro ukimuona akisalimiana na Samia siku hiyo.
 
Wewe ni mtu mzima lkn inaonekana akili yako imemezwa na mahaba ya chama. Mdude ameshamwambia mama kuwa atatumia wembe ule ule aliotumia kumnyolea mtangulizi wake kumnyoa mama. Kwa ujumbe huu wa Mdude inaonesha kabisa Mdude haoni tofauti ya utawala wa mama na wa mtangulizi wake, lkn pia sio Mdude peke yake mwenye mawazo ya aina hii hata Lisu kaishaanza kumfananisha mama na mtangulizi wake. Sasa kuniambia mimi nisitegemee mama kurudi kwenye uovu huku viongozi wako including Lisu washaanza kumuona mama anaelekea kwenye uovu ni kukosa hoja. Kati ya mimi na Mdude ni nani ambae anategemea mama atakuwa muovu kama mtangulizi wake?
 
Katiba inaweza kutungwa na watu wakaivunja vile vile kama zinavyovunjwa katiba zingine. Mbowe alivunja katiba ya chama chake mwenyew kwa kumruhusu Lowasa kugombea nafasi ya uraisi bila kufuata katiba wala taratibu za chama. Ebu fikiria mtu anakuja kwenye chama wiki hii wiki ijayo mwenyekiti anapokea hela na kumruhusu kugombea uraisi huku waliokijenga chama kwa jasho na damu kama dr Slaa na msomi prof Safari wakiandaliwa kuja kumdekia barabara huyo Lowasa. Slaa alipoomba katiba na utaratibu wa kumpata mgombea ufatwe aliitwa msaliti na mtu mwenye tamaa. Sasa mtu wa aina hii ya Mbowe akichaguliwa kuwa raisi anawezaje kushindwa kuvunja katiba na sheria kama alivyovunja kwa Lowasa na ukizingatia kipindi hicho yeye ndo atakuwa amiri jeshi mkuu!
 
Wewe mbilikimo tulia.
Yaani unataka Mdude amshukuru Rais Samia Suluhu kwa lipi?
Mambo yenu ya kutukuzana mliyaanzisha kwa Magufuli mpaka mkaanza kumwita Mungu yaishie hukohuko.
Your browser is not able to display this video.
 

Tofautisha uovu na kuvunja sheria. Nyie mlikuwa mnafaidika na uovu wa magu ndio maana saa hii mnalilia. Alichosema Mdude ni mikwara ya kisiasa tu wala haina madhara yoyote. Huyo mama ungemshauri awakamate waliojiunganishia bomba la mafuta ndio kuna madhara, sio vijembe vya kisiasa. Tafuta kazi ya halali, hiyo ya kuteka na kuua watu haipo tena boss.
 
Ngija ajifanye ana huruma sana. Cha m,uhumu hata angejipa muda kufanya uchunguzi lakini nhuruma yake na ni yakujitafutia umaarufu itamcost tena sio mbali. Atulie sasa afuatilie kujua ukweli kwanza hata kama kuawaachia afanye akijua ukweli!
 

Una maana JPM alikuwa mtawala wa hovyo mvunja katiba sugu? What a legacy?

Sasa kawaambie waliokutuma kuwa wenye nchi sasa wanataka katiba itakayo kuwa na namna za wazi za kuwafurusha forth with watawala dhalimu wavunja katiba sugu kama JPM bila kuwapa hata siku moja zaidi ofisini.

Hii nchi imechezewa sana!

Habari ndiyo hiyo.
 
Uovu gani alioufanyia wa kuwanunulia ndege au\? wa kuwajengea madaraja? au kuwapelekea umeme kwa Bibi zenu ambapo nyie wenyewe hamkanyagi? au kwa kuwasomesha watoto wa watanzania bure. Tusubiri miaka miwili tu mtapata majibu yake.
 
Uovu gani alioufanyia wa kuwanunulia ndege au\? wa kuwajengea madaraja? au kuwapelekea umeme kwa Bibi zenu ambapo nyie wenyewe hamkanyagi? au kwa kuwasomesha watoto wa watanzania bure. Tusubiri miaka miwili tu mtapata majibu yake.

Kaburi Pieter Botha wa Afrika kusini alifanya yote hayo tena kwa ubora mkubwa, lakini alipingwa kwa uovu wake, ww unataja hivyo vindege ndio unadhani ni pazia la kufunika uovu wake? Watoto wa Tanzania walisomeshwa bure kwa kodi za watanzania sio mshahara maana hata sasa wanasoma bure na hakuna uovu. Miaka miwili ipi na wakati mama analia uchumi umeanguka?
 
sio kila wakati dola lazima ikwambie kila kitu..

Ni ngumu dola kukwambia kwanini Uamsho walikuwa jela...sia ajabu ukifunuliwa leo kwa siri ukaonyeshwa harakati zao ungeweza kuandamana na kutaka adhabu kali dhidi yao...
Sio kwa dola hii chini ya CCM ambayo kwa yenyewe hivyo na hapo ilipo ina - struggle ku - survive kwa mbinu za ugaidi wa kidola (state sponsored terrorism)...

Sisi sote (ispokuwa wewe, labda) tunajua kuwa hii siyo dola iliyobena maslahi ya nchi hii na wananchi wake....

Ni dola ya watu wachache iliyoko hapo kwa ajili ya watu hao wachache. Dola ya namna hii haiwezi kufanya hivi unavyofikiri na kudhani. Dola ya namna hii, kila critic & criticism kwayo utakuwa gaidi tu...

Tuna akili, sio wajinga wa kiwango hiki cha kudanganywa. Tunaelewa kila kitu. Tunaelewa kila hadaa...
 
Kijana kama ww kufanywa puppet na mwenyekiti wa Chadema mwenye elimu ya form 4, ni aibu kwako na kwa wazazi wako.
 
Mdude alitoka kwa huruma au kesi ilikosa USHAHIDI WA KUMTIA HATIANI,?

MAKOSA YA KUBAMBIKA (,KUSINGIZIA,, UONEVU, KUKOMOA)

Kwa vile SHERIA zetu ni mbovu, hata kama Mtuhumiwa ataonekana hana kesi ya kujibu, hana HAKI YA KUDAI FIDIA KWA USUMBUFU, MATESO, HASARA YA MALI NA MUDA ALIOPOTEZA KWA KUWEKWA NDANI.

KATIBA MPYA YENYE KUTOA HAKI KWA WOTE INAHITAJIKA SANA KWA SASA KULIKO WAKATI MWINGINE.

"WATANZANIA WANYONGE HAWA"
 
haki haihitaji huruma ya m2 katiba mpya ni suluhisho la ujinga wote huu wa kuoneana
 
Wapinzani walitumiwa na JK kumchafua Lowasa, upinzani wetu ujinga mtupu
Yani upinzan wa tanzania ni wa hovyo sana, wanashindwa hata na wapinzani wa nchi kama Malawi au Zimbabwe wanajua kusimamia agenda na misimamo yao ya chama.
 
Masheikh wa uamsho walikaa jela zaidi ya miaka 9. Walikaa miaka 3 chini ya utawala wa Kikwete na miaka 6 chini ya utawala wa Magufuli, lakini wamekuja kutoka katika miezi 3 tu ya utawala wa mama. Mdude ana zaidi mwaka au miaka. Alikaa jela zaidi ya mwaka au miaka chini ya utawala wa Magufuli, lakini na yeye amekuja kutoka katika kipindi cha miezi hiyo hiyo 3 tu ya mama. Haihitaji shule au akili nyingi kujua ni kwann Mdude hakuweza kushinda kesi miaka yote hiyo aliyokaa jela kabla ya mama kuingia madarakan, lkn ameweza kushinda katika miezi mitatu tu ya mama kuingia madarakan tena baada ya mama kumbadilisha mwanasheria mkuu wa serikali. Haihitaji shule au akili kujua ni kwanini mama alimbadilisha mwanasheria mkuu wa serikali na baada ya hapo Mdude akaweza kushinda kesi na pia masheikh kuachiwa. Najua hauwezi kuongea au kuandika kinyume na yale ambayo mwenyekiti wako wa chama anataka uyaandike hapa JF maana ukiandika ukweli hatokulipa ujira wako, lkn nina imani moyoni unaujua ukweli na nafsi inakusuta mwenyew kwa haya unayoandika hapa. Namalizia kwa huu msemo "Mnyoge mnyongeni lakini haki yake mpeni" Kama mama asingekuwa raisi au asingebadilisha mwanasheria mkuu wa serikali nina imani Mdude na masheikh wa uamsho wangekuwa bado wananyea debe kwa kupigwa kulenda na kuambiwa kwamba ushahidi bado haujakamilika kwahiyo waendelee kuzuiliwa mpaka pale ushahidi utapopatikana.
 
haki haihitaji huruma ya m2 katiba mpya ni suluhisho la ujinga wote huu wa kuoneana
Unajidhalilisha sana dada yang kwa kukubali kufanywa puppet na wanasiasa wachovu kama Lisu, Zito, Mbowe na wengine wa aina yao. Nikikwambia uniandikie vifungu vitano tu vya katiba ambavyo ww na hao waliokutuma mnaona havifai hautoweza. Kilichofanyika ni kukukaririsha tu kwamba katiba haifai lkn kiuhalisia hauna unalolijua kuhusu hiyo katiba isiyofaa. Aibu sana kuona msichana kama ww njaa yako imekufanya uuze utu wako. Na tumegundua kwamb wapinzani wanapigia chapuo swala la katiba ili waje wapige pesa katika kila kikao watachokuwa wanakaa kwa ajili ya kuitengeneza katiba.
 
Wakati mungine mtu unaweza kuwa sio katili, lakini watu wakakufanya ukawa katili

(Hapa nimekuelewa sana) Na ndio wengi walikua hawamuelewi Magu. Hawa wanaojiita wapinzani wanahitaji style ya magu ili mambo yaende.

Wee kuna kiumbe mgumu kama binadamu. Ukimpiga anasema umemuonea, ukimuacha anasema umemuogopa. Aliyemuumba tu ndiye anayemjua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…