Rashda Zunde
JF-Expert Member
- May 28, 2022
- 204
- 231
Kutokana na uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, Tanzania sasa ipo kwenye nafasi nzuri ya kuimarika katika sekta za uwekezaji, biashara na utalii kutokana na maridhiano ya kisiasa.
Miongoni mwa vitu vinavyovutia wawekezaji ni pamoja na sera za kudumu zisizobadilika pamoja na amani na utulivu wa kisiasa katika nchi.
Kwa hali hiyo, ni dhahiri Tanzania inaenda kufaidika kama nchi kutokana na ongezeko la wawekezaji litakalotokana na utulivu wa uhakika wa biashara.
Juhudi za Rais Samia Suluhu za kujenga taifa lenye umoja, mshikamano na uzalendo zinajenga mazingira rafiki kwa biashara ya ndani na nje ya nchi hali itakayolifanya taifa kupata mapato zaidi.
Kitendo cha Rais Samia kukubali kutengeneza taifa lisilo na mipasuko kinatuma ujumbe wa mshikamano na uzalendo.
Siku zote uvumilivu wa kisiasa ambao Rais Samia ameuonesha unatakiwa kuigwa na viongozi wote wa vyama vya siasa ili kufanikisha kupatikana kwa Tanzania bora kwa kila mtu.
Rais Samia ni wa Watanzania wote bila kujali itikadi za kisiasa, imani za kidini, tofauti za makabila na hata ngozi zetu. Huyu ni mama yetu sote hivyo hatuna budi kumuunga mkono katika kuijenga Tanzania iliyo bora.