Rais Samia anawezaje kujenga SGR kilometa 1,063 kwa TZS 10.1T na SG kwa TZS 6.55T?

Huyu mama aishi milele,

Mke wangu kalamba 250,000 daraja jipya,

Ndio kwa mara ya kwanza Sal Slip imebadilika tangu 2015.

Mimi na familia yangu tunamtaka huyuhuyu 2025,

Mbona anafanya yote yaliyofanywa na Magufuli na bado anaachia pesa hayati alikwama wapi?
Inflation cancels out pay rises
 
Ndo maana nasema hizo ni jitihada za kufanya spinning.

Dodoma haipaswi kujengwa kwa fedha hizo.

RC wa Dodoma lazima tafahamu hii kwanini ienezwe kwa mtindo huu?

Hatuwezi kuambiwa tunaongezewa tozo na hapohapo zipo fedha za kugharamia miradi kama ujenzi wa Dodoma.

Narudia kusisita kwa mama aangalie sana ushauri wa wapambe wenye nia tofauti kabisa na serikali ilopita ambayo iliweza kukusanya kodi na kulipia mahitaji ya wananchi bila kuhangaika.

Tuelezwe serikali ilopita ilifanyaje kuhakikisha fedha zinaenda kwenye elimu, walimu wanalipwa mishahara na watumishi wanaliowa mishahara yao ifikapo mwisho wa mwezi.

..labda wawe wanakopa kwa siri kama utawala uliopita.

..lakini itakuja kugundulika wakati wa kulipa, na wakati huo itakuwa ni tatizo la kiongozi mwingine.
 
Namsa
Wasalaam wanaJf,

Ukichukua gharama za miradi miwili tu mikubwa ya SGR na SG inayoendelea kwa sasa yaani Isaka -Mwanza 341km Tshs 3.02trl, Makutupora-Morogoro 422Km Tshs 4.4trl ,Morogoro -DSM 300Km Tshs 2.7trl na SG US$ 2.9BL Tshs 6.5trl Jumla yake ni Tshs 16.6trl achilia mbali miradi mingine yote ikiwemo mipya na ile iliyoachwa na Rais Magufuli yote mama anaziendeleza tena kwa BOQ zilezile,

Kinachonivutia zaidi ni hivi vicheko kwa haya makundi mbalimbali najiuliza Rais Samia amewezaje yote haya yaliyowashinda watangulizi wake wote? Mfano:,

1. Kicheko cha Rais Samia na wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Mpaka Rais Samia anaingia madarakani zaidi ya watoto wa masikini elfu 10 hawakupewa mikopo,Leo tayari ameongeza Tshs 106BL sawa na 23% yaani kutoka Tshs 464BL FY2020/21 hadi 570BL FY2021/22 na kufanya kila mtoto wa masikini aliyefaulu kwenda chuo kikuu kupatiwa mkopo bila kujali historia ya alikosomea huku akifuta kabisa ile 6% ya ada ya thamani ya mkopo ( Value Retention Fee-VRF ) kwenye mikopo hiyo na Sasa wanufaika watakatwa 9% ( single digits) FY2021/22 kutoka 15% ya FY2020/21,Kwa lugha rahisi take home za watu hawa zimepaa kwa 6% nivicheko kila kona ya nchi,
__________________________________

2. Kicheko cha Rais Samia na Wafanyakazi,Sote tunafahamu,kwa miaka mitano ( 5 ) mfululizo tumeshuhudia wafanyakazi wa Umma hawakupandishwa vyeo|madaraja,lakini ndani ya miezi hii michache mama ameshatoa Tshs 509BL,Yaani 449BL za madaraja|vyeo na 60BL za malimbikizo ya mishahara na tayari Pesa hizi zimeleta vicheko kwa wafanyakazi huku akipunguza kodi (PAYE) toka 9% FY2020/21 mpaka 8% hivi sasa,kwa lugha rahisi FY2021/22 ameongeza mishahara ya wafanyakazi wote wa Serikali na binafsi kwa 1% kwa kuwarudishia hiyo 1% ya mishahara yao, na kwakufanya hivyo serikali itatumia|itapoteza kiasi cha Tshs 14.1781BL fedha ambayo itarudishwa kwa wafanyakazi kama nyongeza,
__________________________________

3. Kicheko cha Rais Samia na wasio Ajiriwa,mwisho ilikuwa FY2015/16 wakati wa Mzee JK alipoachilia ajira mpya elfu 52 trh 01|05|2015,Leo miaka mitano baadae na nimiezi michache ya Mama Samia tunashuhudia tena ajira mpya za serikali elfu 40 kwa gharama ya Tshs 239BL na 120BL kwaajili ya kubadili muundo wa Utumishi,maajabu zaidi ya mama tayari amesajili miradi mikubwa mipya 93 yenye thamani ya US$ 1.6BL karibu Tshs 3.23trl ambayo nayo itaajiri watu 23,600 na kumfanya ndani ya hivi vimiezi vichache kutoa jumla ya nafasi 53,600 za ajira achilia mbali miradi mingine mingi ya sekta binafsi|Umma inayoendelea kutoa ajira lengo likiwa ni ajira 8M mwaka 2025.
__________________________________

4. Kicheko cha Rais Samia Majimboni,Bila kujali ukubwa wa jimbo ameshatoa Tsh 132BL sawa na Tshs 500M kila Jimbo kwa majimbo yote 264 kama fedha za maendeleo ya Jimbo mbali na fedha za mfuko wa Jimbo,fedha hizi zimerudisha tabasamu kwa Wabunge hasa wa Majimbo,Mama ametoa tena Tshs 322.158BL kama bajeti ya nyongeza kwaajili ya Ujenzi wa Vyumba 10,000 vya madarasa Zahanati 555,Vituo vya afya 121,hakuishia hapo TARURA nao bajeti yao ameiongeza kwa 254% yaani kutoka 273BL FY 2020/21 hadi 966.43BL FY2021/22 kumaliza kila barabara korofi Vijijini|Mitaani,Nimwendo wa vicheko Tu,
__________________________________

5. Kicheko cha Rais Samia na wafanyabiashara|Wawekezaji, Mhe Samia Ndio rais pekee aliyetangaza hadharani hahitaji kodi za Kishetani na akafuta jumla ya kodi|tozo zote kandamizi zipatazo 232 bila kujali hasara ya Tshs 55.49997BL ambayo serikali yake itapata kwa kuondoa tozo|kodi hizo nia yake aongeze idadi ya walipa kodi kutoka 2.7M waliopo na matokeo najua wote tumeyaona ,Nchi hii tangu tupate uhuru sijawahi kusikia tozo|kodi zaidi ya 230 zikifutwa kwa kwamkupuo Kama ambazo mama ameachilia kicheko hiki kwani hataki kabisa Tax economy ,pamoja na kukataa kodi za kishetani na kuondoa tozo kandamizi bado Miradi yote ya Watangulizi wake anaiendeleza sawasawa ikiwemo SGR US$ 4.64BL au Tsh 10.2trl,SG US$ 2.9BL au Tshs 6.5trl,ndege Mpya,barabara zote ujenzi unaendelea, madaraja yote,meli zote pamoja na haya yote kufanyika bado Wafanyakazi wetu ni vicheko,Wafanyabiashara|wawekezaji wetu ni vicheko,bodaboda wetu ni vicheko, machinga wetu ni vicheko,wanafunzi wetu hasa wa elimu ya juu ni vicheko, wafugaji wetu ni vicheko,wakulima wetu ni vicheko, Wapinzani nao ni vicheko hata wewe unayesoma naamini, Tayari nawewe unakicheko chako umecheka na Mama Samia ,

" Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni mama deserves better Wazalendo wote tumtie moyo, mpaka mwaka 2030 tutashuhudia maajabu, Tuombe uzima Tu"
Namsapoti kwa mengi, ila treatment ya vyama vya upinzani bado sijamuelewa.
 
Gesi ya kupikia majumbani imepanda bei.

Mafuta ya kula yamepanda bei.

Tozo za miamala ziko juu.

Kesho tunaanza kulipia majengo kwenye LUKU, hii maana yake ni kwamba ukinunua umeme utapata units pungufu ili pesa nyingine iende kwenye kodi ya jengo hata kama jengo hilo unaloishi siyo mali yako.

Vyakula vimepanda bei.

Kodi za nyumba zimepanda bei.

Ndugu hivi bado unadiriki kusema Watanzania tumejaa vicheko???????????

Mimi nakwambia sasa hivi Watz wanalia mara 7 zaidi ya ilivyokuwa kipindi cha Mwendazake. Huyu Madam SSH nchi itamshinda kabla hata ya 2025.
Mbolea 1 bag ya urea ni 80000 mpunga gunia moja ni 36000 mpka 50000 je hiko kicheko anacho yye
 
Wasalaam wanaJf,

Ukichukua gharama za miradi miwili tu mikubwa ya SGR na SG inayoendelea kwa sasa yaani Isaka -Mwanza 341km Tshs 3.02trl, Makutupora-Morogoro 422Km Tshs 4.4trl ,Morogoro -DSM 300Km Tshs 2.7trl na SG US$ 2.9BL Tshs 6.5trl Jumla yake ni Tshs 16.6trl achilia mbali miradi mingine yote ikiwemo mipya na ile iliyoachwa na Rais Magufuli yote mama anaziendeleza tena kwa BOQ zilezile,

Kinachonivutia zaidi ni hivi vicheko kwa haya makundi mbalimbali najiuliza Rais Samia amewezaje yote haya yaliyowashinda watangulizi wake wote? Mfano:,

1. Kicheko cha Rais Samia na wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Mpaka Rais Samia anaingia madarakani zaidi ya watoto wa masikini elfu 10 hawakupewa mikopo,Leo tayari ameongeza Tshs 106BL sawa na 23% yaani kutoka Tshs 464BL FY2020/21 hadi 570BL FY2021/22 na kufanya kila mtoto wa masikini aliyefaulu kwenda chuo kikuu kupatiwa mkopo bila kujali historia ya alikosomea huku akifuta kabisa ile 6% ya ada ya thamani ya mkopo ( Value Retention Fee-VRF ) kwenye mikopo hiyo na Sasa wanufaika watakatwa 9% ( single digits) FY2021/22 kutoka 15% ya FY2020/21,Kwa lugha rahisi take home za watu hawa zimepaa kwa 6% nivicheko kila kona ya nchi,
__________________________________

2. Kicheko cha Rais Samia na Wafanyakazi,Sote tunafahamu,kwa miaka mitano ( 5 ) mfululizo tumeshuhudia wafanyakazi wa Umma hawakupandishwa vyeo|madaraja,lakini ndani ya miezi hii michache mama ameshatoa Tshs 509BL,Yaani 449BL za madaraja|vyeo na 60BL za malimbikizo ya mishahara na tayari Pesa hizi zimeleta vicheko kwa wafanyakazi huku akipunguza kodi (PAYE) toka 9% FY2020/21 mpaka 8% hivi sasa,kwa lugha rahisi FY2021/22 ameongeza mishahara ya wafanyakazi wote wa Serikali na binafsi kwa 1% kwa kuwarudishia hiyo 1% ya mishahara yao, na kwakufanya hivyo serikali itatumia|itapoteza kiasi cha Tshs 14.1781BL fedha ambayo itarudishwa kwa wafanyakazi kama nyongeza,
__________________________________

3. Kicheko cha Rais Samia na wasio Ajiriwa,mwisho ilikuwa FY2015/16 wakati wa Mzee JK alipoachilia ajira mpya elfu 52 trh 01|05|2015,Leo miaka mitano baadae na nimiezi michache ya Mama Samia tunashuhudia tena ajira mpya za serikali elfu 40 kwa gharama ya Tshs 239BL na 120BL kwaajili ya kubadili muundo wa Utumishi,maajabu zaidi ya mama tayari amesajili miradi mikubwa mipya 93 yenye thamani ya US$ 1.6BL karibu Tshs 3.23trl ambayo nayo itaajiri watu 23,600 na kumfanya ndani ya hivi vimiezi vichache kutoa jumla ya nafasi 53,600 za ajira achilia mbali miradi mingine mingi ya sekta binafsi|Umma inayoendelea kutoa ajira lengo likiwa ni ajira 8M mwaka 2025.
__________________________________

4. Kicheko cha Rais Samia Majimboni,Bila kujali ukubwa wa jimbo ameshatoa Tsh 132BL sawa na Tshs 500M kila Jimbo kwa majimbo yote 264 kama fedha za maendeleo ya Jimbo mbali na fedha za mfuko wa Jimbo,fedha hizi zimerudisha tabasamu kwa Wabunge hasa wa Majimbo,Mama ametoa tena Tshs 322.158BL kama bajeti ya nyongeza kwaajili ya Ujenzi wa Vyumba 10,000 vya madarasa Zahanati 555,Vituo vya afya 121,hakuishia hapo TARURA nao bajeti yao ameiongeza kwa 254% yaani kutoka 273BL FY 2020/21 hadi 966.43BL FY2021/22 kumaliza kila barabara korofi Vijijini|Mitaani,Nimwendo wa vicheko Tu,
__________________________________

5. Kicheko cha Rais Samia na wafanyabiashara|Wawekezaji, Mhe Samia Ndio rais pekee aliyetangaza hadharani hahitaji kodi za Kishetani na akafuta jumla ya kodi|tozo zote kandamizi zipatazo 232 bila kujali hasara ya Tshs 55.49997BL ambayo serikali yake itapata kwa kuondoa tozo|kodi hizo nia yake aongeze idadi ya walipa kodi kutoka 2.7M waliopo na matokeo najua wote tumeyaona ,Nchi hii tangu tupate uhuru sijawahi kusikia tozo|kodi zaidi ya 230 zikifutwa kwa kwamkupuo Kama ambazo mama ameachilia kicheko hiki kwani hataki kabisa Tax economy ,pamoja na kukataa kodi za kishetani na kuondoa tozo kandamizi bado Miradi yote ya Watangulizi wake anaiendeleza sawasawa ikiwemo SGR US$ 4.64BL au Tsh 10.2trl,SG US$ 2.9BL au Tshs 6.5trl,ndege Mpya,barabara zote ujenzi unaendelea, madaraja yote,meli zote pamoja na haya yote kufanyika bado Wafanyakazi wetu ni vicheko,Wafanyabiashara|wawekezaji wetu ni vicheko,bodaboda wetu ni vicheko, machinga wetu ni vicheko,wanafunzi wetu hasa wa elimu ya juu ni vicheko, wafugaji wetu ni vicheko,wakulima wetu ni vicheko, Wapinzani nao ni vicheko hata wewe unayesoma naamini, Tayari nawewe unakicheko chako umecheka na Mama Samia ,

" Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni mama deserves better Wazalendo wote tumtie moyo, mpaka mwaka 2030 tutashuhudia maajabu, Tuombe uzima Tu"
Asante sana kwa kutufahamisha,tusioyajuwa.Endelea kutufahamisha.
 
Huyu mama aishi milele,

Mke wangu kalamba 250,000 daraja jipya,

Ndio kwa mara ya kwanza Sal Slip imebadilika tangu 2015.

Mimi na familia yangu tunamtaka huyuhuyu 2025,

Mbona anafanya yote yaliyofanywa na Magufuli na bado anaachia pesa hayati alikwama wapi?
Huyu ndio Rais,anayetufaa wananchi wote,kuanzia matajiri,wenye kipato cha kati,maskini,wanyonge.Uongozi wake,haubagui mwananchi ni Rais wa wote.
 
Hii nchi ngumu sana,

Mimi nimeandika mambo halisi yaliyofanywa na Rais wa nchi tena kwa muda mchache sana,Wewe unatukana tu

Mnaotukana bila kukanusha wala kukubali nilichoandika mnaani gani?

Sema sio kweli SGR haijengwi,

Sema sio kweli SG haijengwi,

Sema sio kweli hajatoa ajira,

Sema sio kweli watu wamepandishwa madaraja,

Sema sio kweli daraja la Busisi na Nyerere halijengwi,

Sema sio kweli tozo 232 zimefutwa,

Sema sio kweli VRF ya 6% bado ipo,

Sema PAYE sio 8%

Sema sio kweli wanafunzi 10,000 wamelamba mikopo,

Sema sio kweli SGR Isaka -Mwanza Km 341 haijaanza kwa 3.02trl ,

Sema sio kweli SGR Dar-Moro Km 300 iko 77% na wakandarasi wamelipwa Cash 2.7trl,

Sema sio kweli kipande cha Moro-Dodoma km 442 kiko kwenye 30% na watu wanalipwa cash Tshs 4.4trl,

Sema sio kweli SG mama kashindwa kutoa US$2.8BL ,

Sema sio kweli Nyasi za bandia VAT yake imefutwa,

Sema sio kweli kurasimisha ardhi sasa ni 1% tu,

Sema sio kweli ndege hazinunuliwi,

Sema sio kweli meli hazinunuliwi,

Sema sio kweli Mama amemaliza mpango wa Hoima na vijana 10,000 watalamba ajira,

NJOONI NA HOJA SIO POROJO,

MAMA ANAVUNJA REKODI ZOTE ZILIZOWEKWA KAMA UNABISHA SEMA WAPI KAKWAMA.
Acha bangi Dogo kuandika propaganda ni kaxi rahisi,
 
Umetufinguwa macho,mleta uzi.Tumepata kiongozi msomi,lazima maendeleo yawepo.
 
Wewe ni mpuuzi kweli, value retention fee iko palepale licha ya tamko, kashusha asilimia 1 paye,ongezeko ni 2500 bila kuangalia mshahara wa mtu.Umepandishwa daraja vitu vimepanda,mitozo kibao hadi kwenye luku huku unashangilia kama zuzu, hii nchi imejaa majitu manafiki na yenye phd za kujipendekeza
 
Umewezaje kupoteza muda wako kujaza utopolo kama huu
 
Wewe ni mpuuzi kweli, value retention fee iko palepale licha ya tamko, kashusha asilimia 1 paye,ongezeko ni 2500 bila kuangalia mshahara wa mtu.Umepandishwa daraja vitu vimepanda,mitozo kibao hadi kwenye luku huku unashangilia kama zuzu, hii nchi imejaa majitu manafiki na yenye phd za kujipendekeza

Kama ulikatwa kimakosa nenda kalalamike HR wako, Over
 
Wewe mwenyewe umeandika mavi,

Kwanini tusiwe na ustaarabu,

Sema ni wapi ameongopa umkosoe sio,

Sisi wengine huyu mama ametunusuru na mengi tunampenda sana,

Asante sana kwa kunisaidia kufafanua jambo matusi hayatusaidii kwa lolote,
 
tarehe 20 mwezi wa 8 tozo ya kodi ya jengo inaanza kukatwa kwenye luku 😅

teechnicaly ni service charge iliyoondolewagwa baada ya kuonekana kuwa ni mzigo kwa wananchi

leo imetangazwa serikali imepata mkopo wa 2+ trillion from world bank

plus tozo za miamala bado hujasahau tozo za line za simu

endelea kuota
 
Unasemaje juu ya ongezeko la bei ya mbolea? Kuna kicheko kwa wakulima?
 
Back
Top Bottom