beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,880
- 6,368
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema ili kupunguza mzigo wa kazi, huwa anawaambia Wasaidizi wake kufanya maamuzi kwenye masuala yaliyo ndani ya uwezo wao. Amesema huenda ni uoga, lakini wanapeleka maamuzi kufanywa ngazi ya juu
Ameeleza hayo katika mahojiano maalum na Jambo Tanzania (TBC) akifafanua, "Nawaambia anayekosea maamuzi nitamrekebisha, sitamfukuza. Nitakurekebisha mara ya kwanza, ya pili na ya tatu. Mara ya nne unaendelea kukosea nitajua huwezi kwenye hiyo nafasi"