Rais Samia: Anayekosea maamuzi nitamrekebisha, sitamfukuza

Rais Samia: Anayekosea maamuzi nitamrekebisha, sitamfukuza

Marais wakiwa Waislamu Wanakuwa na utu Sana na ubinadamu, nakumbuka magufuli alimfukuza mtu mbele ya hadhila ya wananchi,yule mtumishi akaizirai hapohapo, au Kama alivyomfukuza NAPE NNAUYE! mpaka Leo uwezi kujua kosa la Nape lilikuwa nini Zaid ya roho yake mbaya tu
Na lukuvi nae kosa lake nini? Au pia roho mbaya?
 
Nashindwaga kuelewa mama kwa nini kila akiongea huwa anajipinga mwenyewe na kukoseakosea.
Alisema akienda sehemu akikuta bango moja, DC au RC umekwenda na maji.
Akasema yeye hataongea kwa mdomo, Bali kwa kalamu.
Leo anasema atakuuita na kukurekebisha
Urais wa kuokota ndio unaomchanganya.
 
Huyu mama kila akiongea anaharibu, anaonesha hawezi hata kuongea bila kujiuliza anachoongea kitaleta muonekano/mtazamo gani kwa jamii
Nimekaa kaa zenji, asilimia kubwa ya wazanzibari hawana sensitivity ya maneno wanayoongea, anaweza akaonge kitu ukabaki unaona aibu wewe!
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema ili kupunguza mzigo wa kazi, huwa anawaambia Wasaidizi wake kufanya maamuzi kwenye masuala yaliyo ndani ya uwezo wao. Amesema huenda ni uoga, lakini wanapeleka maamuzi kufanywa ngazi ya juu

Ameeleza hayo katika mahojiano maalum na Jambo Tanzania (TBC) akifafanua, "Nawaambia anayekosea maamuzi nitamrekebisha, sitamfukuza. Nitakurekebisha mara ya kwanza, ya pili na ya tatu. Mara ya nne unaendelea kukosea nitajua huwezi kwenye hiyo nafasi"
Hakuna kiongozi hapo......
 
Damu ya jpm inamlilia ndoa maana ameanza kuharibu mapema, 2025 anakazi sana ya kuwasahulisha watu kwa huu ulopokaji wake.
 
Chonde chonde "madereva" msiifate kauli hii ya kukosea mara nne mtatutoa uhai wetu na hasara kwa familia na taifa kwa ujumla.

Hatari sana hii sheikh....(in sheikh kipozeo voice)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna wakati huwa nasema yajayo yanafurahisha 😂 😂 😂 😂
 
  • Thanks
Reactions: nao
Mimi nilipita kwenye ukristo Mkiristo mwenyewe alituelekeza tutenganishe mambo yahusuyo dini dhidi ya mambo ya kidunia!
Kule kwenye uislamu cjawah kujua wao wanaamini nini kuhusu hilo.
Lakini walimwengu hawa wa leo,kudhan utaweza kuwaongoza pasipo kuungurumiana,kukoromeana na hata kutishiana km si kuachishana ugali,huenda ni kuandaa kuwaumiza wale raia wa chini tu.
Wabongo ni mithili ya panya mama,watakuguguna huku wakikupulizia hewa barid kwenye jeraha. Mwisho wa siku ww ndo utabaki na makovu ya majeraha maisha yako yote!!
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema ili kupunguza mzigo wa kazi, huwa anawaambia Wasaidizi wake kufanya maamuzi kwenye masuala yaliyo ndani ya uwezo wao. Amesema huenda ni uoga, lakini wanapeleka maamuzi kufanywa ngazi ya juu

Ameeleza hayo katika mahojiano maalum na Jambo Tanzania (TBC) akifafanua, "Nawaambia anayekosea maamuzi nitamrekebisha, sitamfukuza. Nitakurekebisha mara ya kwanza, ya pili na ya tatu. Mara ya nne unaendelea kukosea nitajua huwezi kwenye hiyo nafasi"
Utamrekebisha nini wakati mwenyewe unapotupeleka sipo. Umemsaliti mtangulizi wako umeungana kutetea wapigaji na wafanyabiashara fisadi. Mungu anakuona 😒
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema ili kupunguza mzigo wa kazi, huwa anawaambia Wasaidizi wake kufanya maamuzi kwenye masuala yaliyo ndani ya uwezo wao. Amesema huenda ni uoga, lakini wanapeleka maamuzi kufanywa ngazi ya juu

Ameeleza hayo katika mahojiano maalum na Jambo Tanzania (TBC) akifafanua, "Nawaambia anayekosea maamuzi nitamrekebisha, sitamfukuza. Nitakurekebisha mara ya kwanza, ya pili na ya tatu. Mara ya nne unaendelea kukosea nitajua huwezi kwenye hiyo nafasi"

2 Wafalme 7:1-20​

Mungu aende na Mama kwa KISHINDO KIKUU, kama alivyowahi kwenda na watu wanne wakati wa njaa kali na kupelekea watu hao kugundua uwepo wa chakula kingi cha kuweza kulisha Taifa zima
 
Back
Top Bottom