Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu ukimsikiliza mh Rais Mama Samia Suluhu Hassan akizungumza, ukimuangalia namna anavyotenda utagundua kuwa amedhamiria na anayo kiu ya kuipekeka mbele nchi hii kimaendeleo.
Mh. Rais anayo kiu ya kuona kuwa, hakuna mama mjamzito anasafiri umbali mrefu kufuata kituo cha afya au zahanati. Anatamani na ana kiu ya kuona kuwa, mgonjwa akienda hospitali anapokelewa vizuri, anapata huduma nzuri na anapata dawa bila kuagizwa kwenda kutafuta maduka ya mitaani.
Mh. Rais anayo kiu ya kuona, hakuna mwanafunzi aliyemaliza darasa la Saba anakosa au kushindwa kwenda shule kwa wakati kwa kuwa madarasa hayatoshi. Anataka mwanafunzi aliyefaulu aendelee na masomo bila kikwazo chochote, anataka kuona hakuna mwanafunzi anayekaa chini kwa kukosa dawati, anataka kuona hakuna kijana anashindwa kupata elimu ya juu kwa kukosa mkopo.
Anataka na anayo kiu ya kuona watanzania wanapata maji safi na salama, anataka kuona huduma za umeme zinafika hadi vijijini ili kufungua fursa za ajira, anataka kuona ajira nyingi zinatengenezwa kwetu vijana na mikopo inatolewa kwa vijana.
Ndugu zangu ili hayo yote tuyafikie, ni lazima tupitie njia waliyopitia wenzetu. Njia hiyo siyo nyepesi, siyo tambalale, siyo fupi na wala siyo mteremko. Ni njia tutakayo pata maumivu kiasi, ni njia inayotutaka kuchangishana kutoka katika vipato vyetu, ili kuifikia Tanzania hiyo iliyo bora na yenye kutiririsha fursa mbalimbali.
Lazima tuvuje jasho, lazima tujitwishe mzigo wetu, lazima tuutimize wajibu wetu hata kama atajitokeza wakutusaidia basi atukute tupo njiani kuelekea kanani. Hivyo, tuendelee kumuunga mkono Mh. Rais katika juhudi za kuijenga nchi yetu.
Hakuna mbadala wa njia hii, tusipo pita njia hii tukubali kubaki hapa tulipo daima, tukubali kubaki tumekwama hapa, tukubali kuendelea na matatizo yetu na kulia lia kila siku. Kiongozi mwenye maono hawezi kukubali hilo, hivyo, lazima awajibike kuongoza njia. Mh Rais ameongoza njia ya kutupeleka waliko wenzetu, na hii ndio njia waliyo pitia nasi lazima tupitie, huwezi ukaacha kumpa dawa mtoto eti kwa kuwa ni chungu na analia wakati unajua ndio dawa ya ugonjwa wake. Hii ndio dawa ya kupata na kuyafikia maendeleo waliyopiga wenzetu, ni chungu lakini inaponya.