Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Tanzania ni nchi ya kwanza, kwa Afrika Mashariki na Kati, Kwa SADC, na kama sikosei ya pili kwa Afrika kuwa na Rais mwanamke. Tuna jambo kubwa sana, kwa kuwa hata Marekani hawajawahi kuwa na Rais mwanamke na jaribio lao la kufanya hivyo lilishindwa.
Hatujali kwamba Rais Samia alikuja kuwa Raisi wa kwanza mwanamke kwa Tanzania, Afrika Mashariki na SADC kwa namna ya kurithi na sio kwa kura ya moja kwa moja. Jambo la muhimu ni kwamba kwa sasa yeye ni Rais mwanamke mwenye mamlaka kamili ya uraisi, na hili linampa nafasi ya kipekee sana kujenga au kubomoa kufikiri kwa watu juu ya Rais mwanamke.
Sasa ukweli ni kwamba dunia imegawanyika sana kuhusu uwezo wa wanawake kupewa jukumu la uraisi. Kuna wengine wanapinga, wakidai raisi akiwa mwanamke mara nyingi mumewe ndio atakuwa anaendesha nchi. Wengine hudai Rais mwanamke anakuwa anaendesha mambo kwa hisia badala ya uhalisia.
Na wengine hudai rais mwanamke, ikitokea janga kama vita, atashindwa kabisa kuhimili changamoto za uongozi. Wengine hudai wanawake wana huruma sana, na inawafanya wasiwe viongozi thabiti hasa kwenye masuala ya kuwawajibisha viongozi wazembe na wasiofaa. Wengine hudai mkiwa na Rais mwanamke wateule wake kama mawaziri huwa hawamwogopi na kumpa staha inayostahili. Nk, nk.
Kwa wale wanaounga mkono kuwa na raisi mwanamke, wamedai kwamba mara nyingi wanawake hufuata haki na hivyo nchi itaendeshwa kwa utawala wa sheria. Wengine husema wanawake sio wahujumu uchumi na hawatumii nafasi zao kujineemesha. Wengine hudai sio rahisi kwa mwanamke akiwa Rais kuwakandamiza, kuwafunga na hata kuwaua wapinzani wake wa kisiasa, kitu ambacho wanaume hufanya kirahisi sana. Wengine hudai raisi mwanamke sio rahisi kurubuniwa kimapenzi na mwanaume na kuuza nchi kama ilivyo rahisi kwa raisi mwanaume kurubuniwa kimapenzi na mwanamke na kuuza nchi. nk.
Uhalisia ni kwamba, mara nyingu dunia, kutia ndani na wanawake wenyewe, huwa haina imani sana na maraisi wanawake, ni vigumu sana kwa mwanamke kushinda harakati za kugombea urais. Huo ndio ukweli.
Ndio maana basi nasema wazi, Rais Samia ana nafasi ya pekee sana kuuonyesha umma wa Watanzania, umma wa Afrika Mashariki, umma wa Afrika na dunia nzima kwa ujumla, kwamba unapaswa kubadilika katika kufikiri kwao (mind set) juu ya uwezo wa mwanamke kuwa na mamlaka ya uraisi.
Ni kwa msingi huu Rais Samia anapaswa kuelewa Rais wake sio wa kwake, sio wa CCM bali ni wa Tanzania, Afrika Mashariki, SADC na dunia kwa ujumla. Utendaji wake utakuwa na athari kubwa sana kwamba huko mbeleni Watanzania, Afrika Mashariki, SADC, Afrika na dunia nzima watakuwa na imani na Rais mwanamke au la. Hili litategemea sana anafanya nini katika uongozi wake. Anaweza kujenga au kubomoa suala la kuwa na Rais mwanamke. Anaweza kusababisha Tanzania na kwingineko waseme tunataka tuwe na Rais mwanamke tena, au waseme never, never, never again, tutakubali kuwa na Rais mwanamke.
Rais Saimia, the ball is in your court.