Rais Samia aongeza Saa 24 kwenye uokoaji Kariakoo

Wazungu wamebarikiwa sn, ingekuwa wazanzibar wenzake wapo huko chini angeishia masaa 96? zoezi linatakiwa liende mpk hata wiki 2 hata kama ni maiti tuzione
 
Nadhani kwenye hili hekima itumike tu, (time frame is uncalled for), nafahamu Tanzania tunatumia sheria ya, Law of limitations, ndiyo maana nimependekeza busara zitumike kwa kuangalia mazingira halisi ya janga
 
Akili za kukariri hizi, kuna watu luluki wametoka hai hapo au hata TRA, Brela wana list ya biashara zilizomo humo.

Mpaka sasa serikali ingekuwa walau na idadi ya calculated guess ya watu waliotakiwa kuwe mule ndani. Wangeongea na wafanya biashara waliotoka wazima wangekuwa na picha bado nani ajapatikana, alikuwa floor ipi, then upate picha ya wateja wanaokuwa mule mida ile ya asubuhi etc kuhusu kupata rough estimate unadhani kuna miili mingapi bado.

Kufanya maamuzi tu ya kukisia mtu mwenyewe hata nchini hayupo, yaani mpaka sasa hatujasikia hata wakitoa rough estimate ya watu wanaodhani walikuwa ndani, inakwambia jinsi walikvyokuwa hawajajiandaa na mambo kama haya.
 
Jengo Moja tu uokoaji unafanyika kwa zaidi ya siku ya tatu hadi leo hii, Je, endapo kama lingetokea tetemeko la Ardhi na kusababisha labda majengo mia Moja kuporomoka hivi tungeweza kweli kufanya uokoaji hata wa mtu mmoja???
Ama kweli Rais wa zamani wa Afrika ya Kusini Bw. Pieter Botha alikuwa mkweli kabisa pale aliposema kuwa "Black people are good for nothing apart from indulging in sex and having so many wives."
 
Tuna viongozi wa hovyo sn
 
Hapa tulipigwa haswa kwa huyu maza ni aibu tupu
 

Jamani naona hii habari sijailewa vizuri.

Ninavyoelewa shughuli ya uokoaji hapashwi kuwa na muda maalamu bali hali halisi ndiyo uwa kigezo cha kuendelea na kuokoa au kuacha.
Mwenye kuelewa zaidi atujuze
 
Yaani walio field wenyewe hawakuona umuhimu wa kuongeza siku?
 
Kumbe pia kuna jambo la kujifunza kwa hapo baadae kwenye magorofa kuwe na entrance counter, mashine ya kuhesabu idadi ya walio ingia na kutoka inayoweza kuzirusha taarifa maana na yenyewe pia inaweza ikafukiwa na kifusi
 
Mheshimiwa Rais.

Tumeona agizo lako la kumtaka waziri mkuu aongeze muda wa uokozi kwa masaa 24 zaidi. Pamoja na nia yako njema hata hivyo sijajua ni vigezo gani umetumia vya kuongeza masaa 24 peke yake.

Kwa kawaida binadamu anaweza kukaa bila kula kwa zaidi ya siku hata 7 (hususan wanawake). Sasa tukiangalia tangu ajali itokee, hadi leo hazijazidi hata siku 4. Kwa hiyo huenda kuna watu wako hai chini ya kifusi. Ukiongeza masaa 24 pekee kisha ukasitisha zoezi, huenda wakafa watu wengi ambao hawatapatikana ndani ya hizo saa 24 ila pengine wangepatikana kama siku za uokozi zngeongezeka.

Kwa hiyo nakusihi, Zoezi la Uokozi lindelee kwa siku angalau 10 ili tuwe na uhakika kuwa Sayansi ya Uhai imezingatiwa hata tukisitisha zoezi.

Natanguliza salam

Ni mimi Missile of the Nation
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…