Rais Samia aongeza Saa 24 kwenye uokoaji Kariakoo

Kunadugu bado wako chini kabisa ila hawaongeibsbb hawana nguvu,,serikali injitahidi kupekua Kila kitu kiwaokoa
 
Kuna kitu sielewi, ina maana ukishapita muda huo ulioagizwa na Rais ni kwamba jengo litaporomoshwa lote kwa kuamini kwamba ambao bado wapo chini ya kifusi watakuwa wamekwisha fariki?
 
Saa 72 ni sawa na siku 3, hizi UN wamesisitiza kuwa ni muhimu sana na zinaweza kuokoa hadi 95% ya watu kwenye majanga. Katika muda huo wa siku tatu, maana yake kila anayekumbwa na majanga kuna vitu vya kuzingatia na UN wameweka baadhi ya vitu hivyo ktk tovuti yao 5 essentials for the first 72 hours of disaster response

Rais Samia amesema ameongeza saa 24 ili zoezi la uokoaji uendelee na watanzania wanapongeza suala hili nadhani hawajaelewa maana ya saa 72. Ndani ya saa 72 uwezekano wa kukuta watu wako hai ni mkubwa, sasa kuongeza saa 24 inathibitisha kwamba tumeshindwa kujipanga dhidi ya majanga hadi kuhitaji muda wa ziada ambao kimsingi haukoi watu bali unaokota maiti tu. Kwa saa 72 ilitakiwa kujua muktadha, kupeleka vifaa stahiki na watu wenye ujuzi ili kuokoa watu.

Na UN wanapoweka saa 72 za uokozi haimaanishi kuwa baada ya saa hizi msiendelee kuokota maiti. Mtaendelea ila kwa kujali mazingira siku tatu zinathibitisha uwezo wetu wa kukabiliana na majanga. Fikiria sasa maiti tayari zimeshaanza kuharibika badala ya kuongeza nguvu ili kuokoa watu na kuopoa maiti ili shughuli nyingine ziendelee tunaongeza muda.

Imekuwa ni aibu ninapoona watu wanasema rais ana huruma kaongeza muda. Utadhani kwamba UN wamewaambia baada ya saa 72 fukieni eneo la tukio. Hivi ni lini tutaiwajibisha serikali ili kuboresha namna ya kudeal na majnaga ili kupounguza idadi ya watu tunaowapoteza kwa uzembe tu.

Mtu yeyote mwenye tusi jipya aliseme hapa ili nitukane maana nimekereka sana kwa hizi akili za machawa
 
Wao wakifa wanataka tuwazungushe Tanzania nzima mwezi mzima, leo wapendwa wetu wanapewa masaa ya kuokolewa?Kweli inawezekana sisi ni zaidi ya maiti, mimi sikujua kama kunasheria ya kigaidi kama hii
Sheria za uchaguzi zinakanyagwa kwa manufaa yao Leo wanajifanya sheria za uokozi ndio wanazifuata kwa makini
 
Tukitegemea serikali kutupa data jua tumeisha.

Kuwe na platform ya kutoa taarifa ya raia ambao hawajaonekana tangu siku ya ajali ya jengo ili tupate estimated data.
 
Kwahiyo kumbe uokoaji una muda maalum kwamba ukipita tunaondoka eneo la tukio kuwe na Watu ama Lah?
Bila shaka wanamaanisha uokoaji wa walio hai.
Baada ya hapo zoezi litabadilika na kuwa na kuopoa miili ya wafu.
Baada ya hapo zoezi litakuwa na kuhamisha vifusi.

Kila hatua hapo kuna taratibu zake! Nawasilisha!
 
Masaa 24 ni madogo kuwaokoa Watu bado wapo Wangeongeza Masaa 72 mengine tena aka siku 3 au mpaka jumapili ingelikuwa ni vizuri sana. Kuliko kuweka masaa 24 ni madogo sana kuwaokoa watu kazi yake sio ndogo jamani kuna watu bado wapo ndani wanasubiri kuokolewa Rais anatoa Masaa 24 kuwaokoa watu? Duhhhhhh Majangaa kweli.


View: https://www.youtube.com/watch?v=t56sMX_8jMk&ab_channel=GlobalTVOnline
 
Mungu nisamehe mie mja wako, lakini akili inaniambia kinamna fulani kuzaliwa tz ni kama kalqana fulani hivi.

Pengine umeniepusha kuzaliwa somalia, ama haiti n.k.. Ila bongo napo sio kipolepole.
 
Bila shaka wanamaanisha uokoaji wa walio hai.
Baada ya hapo zoezi litabadilika na kuwa na kuopoa miili ya wafu.
Baada ya hapo zoezi litakuwa na kuhamisha vifusi.

Kila hatua hapo kuna taratibu zake! Nawasilisha!
Kwanini waongeze saa 24?
Kumbe zoezi linaendelea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…