Rais Samia arejea nchini akitokea Afrika Kusini kuhudhuria uapisho wa Rais Cyril Ramaphosa

Rais Samia arejea nchini akitokea Afrika Kusini kuhudhuria uapisho wa Rais Cyril Ramaphosa

Kunasafari ya kwenda Nairobi,kuna mradi wa NSSF wa kuzinduliwa,umeanzisha na makamba.

Chuo kikuu cha Nairobi nacho kina mzigo wake,wa kumvalisha Ile Kofi.

Itakuwa kofia ya Sita
 
kwani kuna mahali alikuwa akiwindwa huko angani?,
Kama wewe una mawazo ya kishetani na humuamini Mungu wala uwepo wa Mungu basi huwezi ukaelewa kwanini wanadamu wenye hofu ya Mungu humshukuru Mungu kila baada ya kufika salama kutoka safarini.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan,amerejea na kuwasili salama kabisa akiwa mwenye furaha, bashasha na tabasamu katika ardhi ya nchi yake usiku huu akitokea Afrika ya Kusini.

Ambako alikwenda kuhudhuria sherehe za uapisho wa Rais wa Taifa hilo Mheshimiwa Cyril Ramaphosa aliyechukua na kuapishwa kushika kiti cha Uraisi kwa Muhula wa pili.

Tunamshukuru sana Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema na Fadhila kwa kumsafirisha vyema Rais wetu na hatimaye kurejea na kufika salama kabisa Nchini akiwa mwenye afya njema na Tabasamu.

Tuendelee kumuombea Rais Wetu Mpendwa ili Mungu aendelee kumlinda,kumtetea na kumpigania wakati wote pamoja na kumjalia afya njema na nguvu za kuendelea kututumikia watanzania.Rais Samia ndio nuru na tumaini letu watanzania,ndio nyota ya matumaini na muongoza njia wetu katika kuelekea nchi ya ahadi.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.

View attachment 3020999
View attachment 3021001

---------

View attachment 3021005
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiondoka katika uwanja wa Ndege wa Waterkloof Pretoria nchini Afrika Kusini mara baada ya kuhudhuria hafla ya Uapisho wa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa iliofanyika Pretoria tarehe 19 Juni, 2024.
mchapakazi hodari na asie choka, kipenzi na fahari ya waTanzania..

God bless you Rais, comrade Dr Samia Suluhu Hassan...
 
Back
Top Bottom