Rais Samia arejea nchini akitokea Afrika Kusini kuhudhuria uapisho wa Rais Cyril Ramaphosa

Rais Samia arejea nchini akitokea Afrika Kusini kuhudhuria uapisho wa Rais Cyril Ramaphosa

Ndugu zangu Watanzania,

Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan,amerejea na kuwasili salama kabisa akiwa mwenye furaha, bashasha na tabasamu katika ardhi ya nchi yake usiku huu akitokea Afrika ya Kusini.

Ambako alikwenda kuhudhuria sherehe za uapisho wa Rais wa Taifa hilo Mheshimiwa Cyril Ramaphosa aliyechukua na kuapishwa kushika kiti cha Uraisi kwa Muhula wa pili.

Tunamshukuru sana Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema na Fadhila kwa kumsafirisha vyema Rais wetu na hatimaye kurejea na kufika salama kabisa Nchini akiwa mwenye afya njema na Tabasamu.

Tuendelee kumuombea Rais Wetu Mpendwa ili Mungu aendelee kumlinda,kumtetea na kumpigania wakati wote pamoja na kumjalia afya njema na nguvu za kuendelea kututumikia watanzania.Rais Samia ndio nuru na tumaini letu watanzania,ndio nyota ya matumaini na muongoza njia wetu katika kuelekea nchi ya ahadi.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.

View attachment 3020999
View attachment 3021001

---------

View attachment 3021005
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiondoka katika uwanja wa Ndege wa Waterkloof Pretoria nchini Afrika Kusini mara baada ya kuhudhuria hafla ya Uapisho wa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa iliofanyika Pretoria tarehe 19 Juni, 2024.

PIA, SOMA:

Lucas, mama amerudi?
 
Rais a-deligate power basiii atuma mabalozi au makamu wake ili wakati mwingine kupunguza gharama.
Hapo mamilioni yametokomea kisa Nini hasa? SA wanaoipinga Israel watatupa faida gani hasa? Labda unga😞
Tuko kwenye majanga ya Albino kuuwawa na WIZI mkubwa kupitia sukari badala atulie nyumbani anakimbilia kwenye masherehe!! Huyu mkuu wa kaya vipiii???
 
Rais a-deligate power basiii atuma mabalozi au makamu wake ili wakati mwingine kupunguza gharama.
Hapo mamilioni yametokomea kisa Nini hasa? SA wanaoipinga Israel watatupa faida gani hasa? Labda unga😞
Tuko kwenye majanga ya Albino kuuwawa na WIZI mkubwa kupitia sukari badala atulie nyumbani anakimbilia kwenye masherehe!!
Ziara za Mheshimiwa Rais zimekuwa na tija kubwa sana. Hata Rais wa Marekani tu husafiri na kufanya ziara katika nchi mbalimbali na kualika pia viongozi kutoka maeneo mbalimbali Duniani.maana huwezi ukajifungia ndani tu kama mgonjwa halafu utegemee kupata fursa za kiuchumi kama vile uwekezaji na wawekezaji
 
Lucas mbona swala la sukari hujaligusia mzalendo wetu.Ww uko busy na safari za mama ama ww sukari haikuhusu uzalendo sio kusifia tu na kukemea mabaya.
Ni kaliba ya misukule yote kung'ang'ana na walichopandikizwa na kufutiwa wasikumbuke kingine chochote cha maana
 
Uongozi ni hekima,busara ,maono na akili ya uongozi.na wala siyo nguvu za mwili .mbona Marekani na wingi wao wa vijana wenye Elimu kubwa na nzuri kutoka vyuo bora ulimwenguni kwote lakini wagombea wake wote wawili kutoka vyama vikubwa wote ni wazee wenye umri mkubwa? Ramaphosa ana miaka mingapi na Joe Biden ana miaka mingapi?
Marekani hata wewe ukiwa raisi mambo yanaenda tu, tofautisha Africa na Marekani viimeachana kwa mbali mno.
 
Ni kaliba ya misukule yote kung'ang'ana na walichopandikizwa na kufutiwa wasikumbuke kingine chochote cha maana
Nakukemea Kwa jina la YESU aliye hai.
Mungu akupe neema ya kujua hilo jina unalolitumia misawa na kumtangaza yule muovu anayeisumbua Dunia...
 
Back
Top Bottom