Rais Samia arusha dongo kwa Lissu, asema kashfa na matusi kwenye mikutano ya hadhara ni kwasababu ya kuzungumzwa hakuna

Rais Samia arusha dongo kwa Lissu, asema kashfa na matusi kwenye mikutano ya hadhara ni kwasababu ya kuzungumzwa hakuna

Yeye si alisema ana kifua na kwamba kazi ya kujibu watafanya chawa?mbona anakereka?atulie tu

Kama kuna wanaotoa matusi mahakama zipo,wapelekwe tuone.
Hivi wale wanaojiita Chawa wa Mama waliishia wapi? Au kwa kuwa hawakupewa mgao wa Dipii ndio wamesusa.
 
...
"Hatukutoa fursa ile watu wakavunje sheria, watu wakasimame kutukana, watu wakasimame kukashifu, watu wakasimame kuchambua dini za watu, lakini sishangangai kwanini haya yanatokea kwasabbu ya kuzungumzwa hakuna!.

"Tulianza oh na katiba, tukaenda ikakatika katikati... bandari, imeenda ah sasa imerudi tena katiba, inapokuwa hakuna na unalazimisha lazima ufanye jambo utazungumza yasiyokuwepo au yasiyo katika muelekeo huo." -
Rais Samia

Laiti angetoa mfano wa hayo "matusi" angeeleweka.

Aya ya mwisho anakiri kuwa siyo matusi bali hoja za kitaifa KATIBA na BANDARI. Mwungwana angetoa majibu
 
Samia kasema utawala wake unafuata sheria na katiba ya 77.

Polisi wanafanya kazi hadi jumapili na dhamana wanatoa na si ilivyokuwa kwa mtangulizi wake.
Hawa wanaharakati muda mwingine wanataka kukutoa kwenye reli uharibikiwe mtangulizi wa samia alikua sahihi kwa baadhi ya hawa wanasiasa wa upinzani.
 
Hawa wanaharakati muda mwingine wanataka kukutoa kwenye reli uharibikiwe mtangulizi wa samia alikua sahihi kwa baadhi ya hawa wanasiasa wa upinzani.
Infact ni Wahafidhina ndani ya CCM ndio wanataka kumharibia.
 
"Tumeruhusu mikutano ya hadhara tukiwa na nia vyama vya siasa vizungumze, wananchi wasikie sera zao, mipango yao, mada zao ili vyama vikue na virudishe wale waliowapoteza. Viweze kurudisha, vyama visimame viwe madhubuti tukienda kwenye uchaguzi kila chama kimejijenga vya kutosha na ndio maana ya kutoa fursa hii ya mikutano ya hadhara.

"Hatukutoa fursa ile watu wakavunje sheria, watu wakasimame kutukana, watu wakasimame kukashifu, watu wakasimame kuchambua dini za watu, lakini sishangangai kwanini haya yanatokea kwasabbu ya kuzungumzwa hakuna!.

"Tulianza oh na katiba, tukaenda ikakatika katikati... bandari, imeenda ah sasa imerudi tena katiba, inapokuwa hakuna na unalazimisha lazima ufanye jambo utazungumza yasiyokuwepo au yasiyo katika muelekeo huo." -
Rais Samia
Tunachosema ni kwamba bandari haiuzwi
 
Hii nchi kwa maneno matupu na makaratasi sisiemu haiwez kung'oka the only way is hard way mpaka kenge atokwe damu sikion ndipo atajua tupo sirious,ni upumbavu kutueleza kuleta katiba mpya hadi wananchi wapewe Elimu,wkt ule wanatuletea katiba ya samwel sitta wapi walitupa elimu?? Mambo wanayopitisha bungeni wananchi wameshrikishwa...ujinga mtupu!
 
Back
Top Bottom