Rais Samia asema amerekodi Filamu nyingine kuitangaza Tanzania nchini China

Rais Samia asema amerekodi Filamu nyingine kuitangaza Tanzania nchini China

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa uzinduzi wa Hoteli ya Kimataifa ya Kwanza Wilaya ya Kusini Unguja visiwani Zanzibar amesema kuwa akiwa mkoani Arusha hivi karibuni amerekodi filamu ya kutangaza utalii wa Tanzania nchini China kwa kushirikiana na msanii maarufu nchini China Jin Dong aliyekuwa hapa nchini ili kuvutia watalii kutoka nchini China.

China inatajwa kuwa na watalii wanaotembelea nchi mbalimbali duniani wanaofikia Milioni 10.

=====

WhatsApp-Image-2023-08-20-at-5.25.46-PM.jpeg

"Hivi karibuni nilikuwa Arusha Park na mtu anaitwa Jin Dong ni Mchina, huyu ni mcheza sinema maarufu sana kule China, nilikuwa naye Arusha Park "tuka-shoot" (tukarekodi) video pamoja inaitwa Karibu "Kijiji cha Milele", itakwenda kutafsriwa Kichina itaoneshwa kwao, itaingizwa maneno ya Kiswahili itaoneshwa kwetu na tunategemea itavuta wageni wengi Wachina.

Wachina wana watalii kama milioni 10 kwa mwaka wanaotoka kwenda kutembea, kati ya hao tukipata Milioni 3 tu si haba, lakini sasa tufanye kazi ya kujega mahoteli ili wakifika wahisi wako nyumbani." Rais Samia Suluhu Hassan.
 
Wenzetu wanatumia wachezaji wa mpira kupitia jersey na machapisho, yeye yuko busy kufanya filamu na kuwapa faida kubwa waandaaji!
Kazi kwelikweli
 
Wakuu kaeni Mkao wa kula, Royal tour nyingine itaachiwa wakati wowote na Rais Samia pamoja na Sterling wake kutoka China Jin Dong.

Wadau wa Utalii mnasemaje?
Screenshot_20230830-085308.jpg
 
Angeigiza na don yen ilikua bonge pira yaani...wamemdanganya mama, jing dong baada ya don yen. Daaah.
 
Back
Top Bottom